PSG 2-3 Barcelona: Raphinha ampiku Kylian Mbappe huku vijana wa Barca wakivunja rekodi

Mechi za kwanza za robo fainali ya Ligi ya Mabingwa zimekamilika.

Muhtasari

•Vijana wa Barcelona walifanikiwa kutoka nyuma na kupata ushindi wa 3-2 kabla ya mkondo wa pili Jumanne ijayo.

•Atletico Madrid nao waliishinda Borussia Dortmund2-1 na kuwa na faida ndogo baada ya mkondo wa kwanza.

Image: BBC

Mechi za kwanza za robo fainali ya Ligi ya Mabingwa zimekamilika.

Na, safari ya Barcelona kwenda Paris St-Germain ilikuwa ya kufana kwani washindi mara tano walitoka nyuma na kupata ushindi wa 3-2 kabla ya mkondo wa pili Jumanne ijayo.

Winga wa zamani wa Leeds, Raphinha aling'ara jijini Paris, huku Kylian Mbappe akishindwa kutamba.

Pia kulikuwa na baadhi ya vijana waliovunja rekodi katika upande wa Barcelona, ambao walionyesha mchezomzuri mbele ya umati wa watu wa Parisi wenye chuki walipokuwa wakiwafuata.

Winga wa Brazil Raphinha hakuwahi kufunga katika Ligi ya Mabingwa kabla ya mechi ya Jumatano mjini Paris, lakini usingejua kuhusu ubora wake karibu na lango.

Kwa bao lake la kwanza, alitumia makosa ya Gianluigi Donnarumma .

Bao lake la pili, ambalo lilifanyaBarcelona kusawazisha , lilionyesha ustadi wa hali ya juu alipotazama pasi iliyokatwa ya Pedri ikija begani mwake kabla ya kulifunga kwamguu wake wa kushoto.

Atletico Madrid nao waliishinda Borussia Dortmund2-1 na kuwa na faida ndogo baada ya mkondo wa kwanza wa robo fainali ya Ligi ya Mabingwa.

Kikosi cha Diego Simeone kilianza vyema uwanjani Estadio Metropolitano naye Rodrigo de Paul akawaweka mbele dakika ya nne baada ya kutumia vyemapasi ya Ian Maatsen .

Wageni walionekana kuwa na wasiwasi sana mapema na ilipoonekana wametulia kwenye mchezo, mchanganyiko mwingine katika safu yaulinzi ulimruhusu beki wa pembeni Samuel Lino kuipatapasi ya Antoine Griezmann na kuifungia Atletico bao la pili kwa utulivu.