•Bellingham amekuwa mchezaji muhimu wa Real kufuatia uhamisho wake wa pauni milioni 89 kutoka Borussia Dortmund msimu uliopita wa joto.
Kiungo wa kati wa Uingereza na Real Madrid Jude Bellingham ameshinda tuzo ya Laureus World Sports Breakthrough of the Year 2024.
Mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 20 amekuwa mchezaji muhimu wa Real kufuatia uhamisho wake wa pauni milioni 89 kutoka Borussia Dortmund msimu uliopita wa joto.
Alifunga bao la ushindi dhidi ya Barcelona kwenye El Clasico Jumapili na kufikisha mabao 17 kwenye La Liga msimu huu.
Bellingham pia aliisaidia Real Madrid kuishinda Manchester City kwa mikwaju ya penalti katika robo fainali ya Ligi ya Mabingwa wiki iliyopita.
Tuzo ya Laureus ya Mwanaspoti Bora wa Dunia ilikwenda kwa mchezaji tenisi Novak Djokovic kwa mara ya tano, huku kiungo wa kati wa Uhispania na Barcelona, Aitana Bonmati akishinda tuzo ya upande wa wanawake.
Bonmati, ambaye kwa sasa anashikilia Ballon d'Or, aliisaidia klabu yake kushinda Liga F, Kombe la Uhispania na Ligi ya Mabingwa ya Wanawake mnamo 2022-23.