Man United kuwauza karibu wachezaji wote wa kikosi cha kwanza

Mashetani Wekundu wako tayari kusikiliza ofa kwa takribani timu yao yote ya kikosi cha kwanza msimu huu wa joto.

Muhtasari

•Kati ya wachezaji wa kawaida wa meneja Erik ten Hag, chipukizi Rasmus Hojlund, Kobbie Mainoo na Alejandro Garnacho wanafikiriwa kubakizwa.

•Haijabainika jinsi maslahi yatakavyokuwa katika kikosi chochote cha United, wala ada wanazoweza kuitisha.

Image: BBC

Manchester United wako tayari kusikiliza ofa kwa takribani timu yao yote ya kikosi cha kwanza msimu huu wa joto huku Sir Jim Ratcliffe akijaribu kuigeuza klabu hiyo kupigania mataji na kuheshimiwa tena

Inafahamika kuwa Marcus Rashford yumo kwenye orodha hiyo, ingawa vyanzo vya klabu vinasisitiza kwamba wanapendelea kumbakisha mshambuliaji huyo wa Uingereza na kushirikiana naye kurejesha kiwango kilichomletea mabao 30 kwa mara ya kwanza msimu uliopita.

Paris St-Germain hapo awali walikuwa wakihusishwa na Rashford na wanatazamiwa kumpoteza nyota wao Kylian Mbappe, ingawa vyanzo hapo awali viliitenga PSG iliofuzu katika nusu fainali ya Ligi ya Mabingwa dhidi kumnunua mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 26.

Kati ya wachezaji wa kawaida wa meneja Erik ten Hag, chipukizi Rasmus Hojlund, Kobbie Mainoo na Alejandro Garnacho wanafikiriwa kubakizwa.

Ingehitaji ofa kubwa kabla United kufikiria kumuuza nahodha Bruno Fernandes, mlinda lango Andre Onana na beki wa pembeni Diogo Dalot, ambaye alisaini mkataba mpya wa miaka mitano chini ya miezi 12 iliyopita.

Kiasi halisi cha biashara wanayofanya hatimaye kiko wazi kuhoji. Haijabainika jinsi maslahi yatakavyokuwa katika kikosi chochote cha United, wala ada wanazoweza kuitisha.

Wamekuwa wakishindwa kuwauza wachezaji katika siku za nyuma. Uhamisho wa Daniel James kwa pauni milioni 25 kwenda Leeds mnamo 2021 ilikuwa mara ya mwisho kuchangisha pauni milioni 20 kutoka kwa mchezaji.

Kuna uwezekano watalazimika kumaliza nafasi ya sita kwenye ligi ya Premia au kuifunga Manchester City kwenye fainali ya Kombe la FA ili kufuzu kwa Ligi ya Europa.

Kwa sasa wako nafasi ya sita, pointi moja mbele ya Newcastle, ambao watacheza nao Old Trafford mnamo Mei 15.