Kocha wa zamani wa Wolves, Julen Lopetegui kuchukua nafasi ya Moyes klabuni West Ham

Habari hizi zinakuja baada ya West Ham kuchapwa mabao 5-0 na Chelsea kwenye uwanja wa Stamford Bridge siku ya Jumapili, huku joto la shinikizo likizidi kuongezeka dhidi ya ukufunzi wa Mskoti huyo.

Muhtasari

• Moyes, ambaye kipindi chake cha pili London Mashariki kilianza Desemba 2019, ameifanya timu yake kushuka hadi nafasi ya tisa kwenye jedwali la Premier League.

West Ham wafikia maelewano ya kumsaini kocha mpya
West Ham wafikia maelewano ya kumsaini kocha mpya
Image: Hisani

Julen Lopetegui "amekubali masharti" ya kuwa meneja mpya wa West Ham, kulingana na ripoti.

Bosi huyo wa zamani wa Wolves, 57, anatarajiwa kuchukua nafasi ya David Moyes msimu wa joto baada ya kukubali ofa ya The Hammers.

Pande zote mbili sasa zinakamilisha mikataba.

Mtaalamu wa masuala ya Uhamisho Fabrizio Romano alivunja habari hiyo, akitweet: "Julen Lopetegui amekubaliana na West Ham kuwa kocha mkuu mpya kuchukua nafasi ya David Moyes kuanzia msimu ujao. Lopetegui amekubali pendekezo la #WHUFC, tayari kuendelea na hatua rasmi. Maelezo yakikamilika kisha mikataba itasainiwa lakini makubaliano yatakuwepo."

Habari hizi zinakuja baada ya West Ham kuchapwa mabao 5-0 na Chelsea kwenye uwanja wa Stamford Bridge siku ya Jumapili, huku joto la shinikizo likizidi kuongezeka dhidi ya ukufunzi wa Mskoti huyo.

Moyes, ambaye kipindi chake cha pili London Mashariki kilianza Desemba 2019, ameifanya timu yake kushuka hadi nafasi ya tisa kwenye jedwali la Premier League.

Hawajashinda mchezo wowote kati ya sita zilizopita katika mashindano yote.

Lakini uchezaji wa Moyes katika klabu ya West Ham umekuwa wa mafanikio kwa kuwaongoza kutwaa ubingwa wa Ligi ya Europa Conference, pamoja na kumaliza katika nafasi ya tano mfululizo.