Michael Antonio awatahadharisha Manchester City

Mshambulizi wa West Ham awaonya Manchester CIty kuhusu taji la EPL 23/24

Muhtasari

•Mshambulizi wa West ham atoa maoni yake kuhusu  bingwa  mtarajiwa wa primia

•Ligi kuu ya primia kutamatika jumapili 19, 2024

Michael Antonio
Image: Hisani

Mshambulizi wa klabu ya West ham yenye makaazi jijini London na raia wa Jamaica, Michael Antonio ameelezea maoni yake kuhusu ni nani atakayenyakua taji kuu la primia msimu huu iwapo mechi ya mwisho itaamua  baina ya wapambanaji wawili.

Kwenye majadiliano kati yake na wachapishaji wa gazeti la 'The Footballer's Football ', Antonio amesema kuwa Arsenal  wana uwezo wa kunyakua taji hilo kwa kuwa West Ham wapo katika harakati  ya kuwania mashindano ya bara ulaya .

'Mechi ya mwisho ya msimu huu, sisi [West Ham ]tuna kitu cha kuchezea pia,tunajaribu kuingia ulaya...'

West Ham watachuana na Manchester City kwenye mechi ya mwisho ya  msimu jumapili 19. Iwapo wataibuka na ushindi nayo Arsenal iwanyoroshe Everton , basi maneno yake Michael Antonio yatakwenda sawa .Arsenal itakuwa mbele ya manchester city kwa alama moja,hivo kutawazwa mabingwa.

Kwa sasa West Ham wanashikilia nafasi ya tisa kwa alama 52, na iwapo chelsea na manchester united watakosa kushinda mechi zao , basi  West Ham watakuwa wataajikatia tiketi ndani ya  mashindano ya bara Ulaya.

Je , Manchester City watapokonywa taji na wanabunduki, Arsenal ?