Man City washinda taji la nne la ligi ya England huku Foden akifunga mara mbili

Vijana wa Pep Guardiola waliifunga West Ham mabao 3-1 kwenye Uwanja wa Etihad.

Muhtasari

•City walinusurika hofu ya dakika za lala salama wakati West Ham ilipopata bao la pili lililokataliwa na VAR baada ya mchezaji kuunawa mpira.

•Sasa timu ya Guardiola imepata kitu ambacho hakuna upande mwingine imefanikiwa tangu ligi ya Uingereza ilipoanzishwa.

Image: BBC

Manchester City iliifunga West Ham mabao 3-1 kwenye Uwanja wa Etihad na kuwa timu ya kwanza kushinda taji la ligi ya Uingereza misimu minne mfululizo.

Huku City wakihitaji ushindi ili kuwa na uhakika wa kuwazuia Arsenal, ambao walianza siku ya mwisho wakiwa nyuma kwa pointi mbili lakini wakiwa na tofauti nzuri ya mabao, Phil Foden aliweka kikosi cha Pep Guardiola mbele baada ya dakika mbili pekee.

Nyota huyo wa Uingereza aliongeza jingine kabla ya mapumziko na ingawa Mohammed Kudus alirudisha goli moja, kiungo Rodri alirejesha tofautiya mabao mawili kwa wenyeji kupitia shuti kali kutoka kwenye eneo la hatari baada ya dakika 59.

City walinusurika hofu ya dakika za lala salama wakati West Ham ilipopata bao la pili lililokataliwa na VAR baada ya mchezaji kuunawa mpira.

Hata hivyo, ushindi wao haukuwa na shaka kamwe

Kwani ulikamilisha mwendo wa kushangaza wa ushindi 19 na sare nne tangu kushindwa kwao kwa mara ya mwisho kwenye ligi, huko Aston Villa mnamo 6 Desemba.

City sasa wameshinda mataji sita kati ya saba iliyopita ya Premier League. Muhula uliopita, waliungana na Huddersfield, Arsenal, Liverpool na Manchester United, mara mbili, kushinda ligi kuu miaka mitatu mfululizo.

Sasa timu ya Guardiola imepata kitu ambacho hakuna upande mwingine imefanikiwa tangu ligi ya Uingereza ilipoanzishwa mwaka 1888, miaka 136 iliyopita.