Vincent Kompany,McKenna,Thomas Frank miongoni mwa wakufunzi watarajiwa Chelsea

Klabu hio ilimwachisha kazi mkufunzi wao Mauricio Pochettino usiku wa Jumanne 21,2024

Muhtasari

•Chelsea kumtaja mkufunzi wao hivi karibuni

•Pochettino aliachishwa kazi baada ya madai ya kutoelewana na wakubwa wake.

Kocha Mauricio Pochettino
Chelsea FC// Kocha Mauricio Pochettino
Image: Chelsea TV

Chelsea ipo mawindoni kumtafuta mkufunzi mpya, baada ya Mauricio Pochettino kuondoka,usiku wa kuamkia Jumatano.

Kulingana na ripoti za mwanahabari maarufu,Fabrizio Romano,kulikuwepo na kutokuelewana baina ya mkufunzi Pochettino na wasimamizi wa klabu hio.Dira,mipango ya baadaye kati ya Pochettino na wasimamizi wake haikuambatana hivo kumuachisha kazi mara moja.

Inasemekana kuwa Pochettino alitaka ahusishwe kwenye mambo ya uhamisho wa wachezaji ila wakubwa wake hawakupendelea jambo hilo.

Wachezaji kadhaa wameonyesha kutofurahishwa na kufurushwa kwa kocha huyo akiwemo Nicholas Jackson.Ikizingatiwa kuwa hisia za mkufunzi huyo na wachezaji wake zilikuwa zimeimarika hivi majuzi.

Kwa sasa klabu inaamini kumtaja kocha anayeamini vipaji vya vijana wadogo,umilisi wa asilimia kubwa uwanjani utasaidia timu hiyo kufika viwango vya juu.

Hakuna mawasiliano rasmi yaliyofanyika baina ya Thomas Tuchel,Antonio Conte,Jose Mourinho na Hansi Flick ambao kwa sasa wapo huru licha ya uvumi kuenea.

Aidha,mkufunzi wa Brentford Thomas Frank,Kieran McKenna wa Ipswich town na Vincent Kompany wamehusishwa ila hakuna chapisho rasmi kwa sasa.

Wagombea zaidi watajadiliwa kati ya wamiliki na wakurugenzi wa klabu hio ili kufanya maamuzi ya mwisho.Je,ungependelea kocha yupi aje stamford Bridge?