Jadon Sancho afurahia kurudi Wembley kwenye fainali ya UEFA.

Sancho atakuwa anarejea ugani Wembley Jumamosi hii tangu kupoteza penalti kwenye fainali ya Euro 2020 akidai kuwa haijafutika akilini.

Muhtasari

•Jadon Sancho amefurahia kushiriki kwenye fainali ya UEFA  tangu arejee Dortmund kwa mkopo kutoka katika kipindi kigumu huko Manchester United.

•Dortmund watavaana na Real Madrid Jumamosi kwenye fainali ya UEFA Jumamosi 1,Juni,2024

Jadon Sancho
Jadon Sancho
Image: X

Jadon Sancho amefurahia kukumbana na Real Madrid kwenye fainali ya UEFA akidai kuwa hiyo ni changamoto tosha kwake ili kuimarisha mchezo wake.

Sancho mwenye umri wa miaka 24, aliye kwa mkopo kutoka Manchester United amekuwa mchezaji wa muhimu kwa klabu yake ya zamani ,Dortmund .Sancho alicheza mechi tatu pekee msimu huu akiwa Manchester United, mara yake ya mwisho ikiwa ni  mwezi Agosti kabla ya kujiunga na Dortmund.

Hata hivyo, ni mmoja wa  wachezaji muhimu katika jitihada za wajerumani  kwenye mtanange wa Wembley  fainali ya ligi ya mabingwa Jumamosi. Kuibuka tena kwa Sancho chini ya bosi Edin Terzic kumeongeza mapenzi kwenye hafla hiyo.

Kwenye mahojiano na waandishi wa habari,Sancho amefichua kuwa  ni furaha kushiriki kwenye fainali ya UEFA.

"Sidhani kama mtu yeyote angetarajia hii ,kufika kwenye fainali ya ligi ya mabingwa. Nimefurahi sana...nimebarikiwa..." mshambulizi huyo alisema.

Aidha amefichua kuwa amekuwa akifanya mazoezi kwa wingi ili kujiimarisha na kuwa mchezaji bora;

"Nimekuwa nikijishughulisha tu, nikijaribu kuwa mchezaji bora. Kufanya zoezi ziada. Kila kitu ninachofanya ni kwa ajili ya timu na ninawashukuru  wafanyakazi kwa kunikaribisha tena..."

Pambano hilo pia linampa Sancho fursa ya kufuta msiba wa fainali ya Euro 2020 wakati timu yake ya Uingereza iliposhindwa na Italia kwa mikwaju ya penalti.Marcus Rashford, Bukayo Saka na Sancho walikosa nafasi kwa upande wa Gareth Southgate na walinyanyaswa na wabaguzi wa rangi mtandaoni baadaye.

Licha ya wimbi kubwa la upendo kutoka kwa umma kujaribu kumpembeza, Sancho alikiri makovu bado yanazidi na hajasahau katu.

“Ilikuwa ngumu. Upinzani haukuwa mzuri. Nikiwa London, si katika miaka milioni moja ningefikiria tungepokea hiyo. Ni kumbukumbu ninajaribu kuzuia lakini haifutiki kichwani."