Champions League: Uzito wa fainali kati ya Real Madrid na Borussia Dortmund huko Wembley

Ancelotti – meneja aliyepata ufanisi mkubwa kwa mataji manne anafahamu kwamba hakuna uhakikisho wa ushindi.

Muhtasari
  • Tofauti na Dortmund, ambao wamekuwa na kibarua kigumu nyumbani lakini wakatamba Ulaya, mabingwa wa Uhispania wamekuwa na hali tofuati katika hatua za mbele za amshindano hayo.

Meneja wa Real Madrid Carlo Ancelotti anasema wachezaji wake watahisi msisimko wa fainali ya ligi ya mabingwawatakapokutana na Borussia Dortmund huko Wembley.

Washindi hao mara 14 ya ligi hiyo wanakutana Jumamosi usiku na timu hiyo ya Ujerumani walioibuka katika nafasi ya tano kwenye ligi ya Bundesliga msimu huu.

Ancelotti – meneja aliyepata ufanisi mkubwa kwa mataji manne anafahamu kwamba hakuna uhakikisho wa ushindi.

"Fainali ya ligi ya mabingwa ni mashindano muhimu na hatari mnoe," anasema Ancelotti.

"Lazima uwe na bahati nzuri, ucheze vizuri na uwe muangalifu saa zote lakini unapofika kwenye fainali ushindi upo karibu kiasi cha kwamba unakuwa na wasiwasi".

Tofauti na Dortmund, ambao wamekuwa na kibarua kigumu nyumbani lakini wakatamba Ulaya, mabingwa wa Uhispania wamekuwa na hali tofuati katika hatua za mbele za amshindano hayo.

Real imewafunga Manchester City kwa mikwaju ya penalti katika mechi ya timu nane za mwishona kufunga magoli mawili katika awamu ya pili ya nusu fainali na kusongea juu ya Bayern Munich.

"Ni upanga wa pande mbili ni lazima tuishangilie vilivyo alafu wasiwasi unaanza tukihofia huenda kitu kikaharibika kwasababu tuko karibu sana kukifikia kitu muhimu sana katika soka." Ancelotti, alieleza siku ya Ijumaa