EURO 2024:Droo ya hatua ya kumi na sita bora

Mechi za hatua ya kumi na sita bora kwenye mashindano ya Euro 2024 zitaanza Jumamosi ,Juni 29 hadi Julai 2,2024

Muhtasari

•Belgium watamenyana na France kwenye mechi inayotazamiwa kuwa kali kati hatua ya kumi na sita bora.

•Switzerland watafungua hatua ya kumi na sita bora dhidi ya mabingwa watetezi Italy,Jumamosi Juni 29.

Uhispania washerehekea bao dhidi ya Italia
Image: HISANI

Droo ya hatua ya kumi na sita bora kwenye mashindano ya kombe la bara Ulaya ,Euro 2024 imekamilika baada ya mechi za makundi kufikia mwisho Juni 26.

Timu zilizomaliza nafasi ya kwanza na ya pili kwenye hatua ya makundi zimejikatia tiketi huku timu nne zikiongezwa zilizomaliza katika nafasi ya tatu almaarufu kama 'best losers'.

Kikosi cha Gareth Southgate kitamenyana na Slovania baada ya kumaliza nafasi ya kwanza kwenye kundi lao Jumapili 30.

Mabingwa watetezi Italy watakuwa na kibarua dhidi ya Switzerland waliomaliza kwenye nafasi ya pili,kundi A nyuma ya Ujerumani,ambao sasa wapo mawindoni kwa taji hilo wakiwa wenyeji wa michuano hio na watatifuana na Denmark

Hatimaye ushindi wa  Georgia  wa 2-0 dhidi ya Ureno usiku wa Jumatano ulliwakikishia kufuzu kwenye hatua ya kumi na sita bora baada ya kumaliza wa pili kwenye kundi F na watakwaruzana dhidi ya Uhsipania.

Romania watacheza na Uholanzi katika mechi yao ya kwanza ya mtoano ya mashindano kwa miaka 24 huku kikosi cha aliyekuwa meneja wa Manchester United ,Ralf Rangick Autria kikimaliza udhia dhidi ya Uturiki.

Mechi inayotazamiwa kuwa na mvuto zaidi itawahusisha mabingwa wa kombe la dunia wa mwaka 2018 ,Ufaransa watakapotoana kivumbi dhidi ya Ubelgiji.

Hii hapa ni droo kamili:

                        Italy vs Switzerland

                       Germany vs Denmark

                        England vs Slovakia

                       Spain vs Georgia

                        France vs Belgium

                        Portugal vs Slovenia

                        Romania vs Netherlands

                        Austria vs Turkey

Mechi hizo za hatua ya kumi na sita bora zinatazamiwa kuanza Jumamosi ,Juni 29 hadi Julai 2,2024.