Emerging Stars wasajili ushindi wa kwanza katika kombe la COSAFA

"Zambia haikuwa timu rahisi na tulijua tukitaka kushinda mchezo huu tunatakiwa kufunga mabao ya mapema, tunatakiwa kufanya kazi zaidi na mechi ijayo tutakuwa tofauti," alisema.

Muhtasari

•Kenya waliweka kasi ya juu tangu mwanzo, na juhudi zao zilizaa matunda dakika ya 8 pale Patrick Otieno alipochezewa vibaya  kwenye eneo la hatari.

•Kocha mkuu wa Emerging Stars Ken Odhiambo aliipongeza timu hiyo kwa mwanzo mzuri dhidi ya Zambia.

Timu ya Emerging Stars
Image: Hisani

Emerging Stars ilianza kampeni ya Kombe la COSAFA kwa ushindi wa 2-0 dhidi ya mabingwa watetezi Zambia Alhamisi, Juni 27, 2024 kwenye Uwanja wa Nelson Mandela Bay.

Kenya waliweka kasi ya juu tangu mwanzo, na juhudi zao zilizaa matunda dakika ya 8 pale Patrick Otieno allipochezewa vibaya  kwenye eneo la hatari.

Mchezaji wa Gor Mahia Austine Odhiambo alipiga hatua kwa kujiamini na kufunga penalti hiyo, na kuifanya Kenya kuongoza mapema.

Nguvu ya ushambuliaji ya timu hiyo iliendelea kung’ara huku mshambulizi wa Posta Rangers, Patrick Otieno akifunga bao la pili dakika ya 18, na kuwaacha mabingwa hao wakipambana kupanda.

Kipindi cha kwanza kilipokamilika, Kenya walidumisha ubabe wao, hadi mapumziko wakiwa na faida nzuri ya 2-0 dhidi ya Chipolopolo.

Kipindi cha pili kilishuhudia Kenya wakiendeleza msimamo wao thabiti wa ulinzi na udhibiti wa mchezo. Licha ya majaribio ya Zambia kuungana, ulinzi wa Kenya ulisimama kidete, ukinyima fursa zozote za kurejea tena.

Ushindi huo uliifanya Kenya kumaliza siku ya ufunguzi wakiwa kileleni mwa Kundi B kwa tofauti ya mabao baada ya Zimbabwe kuwalaza Comoro 1-0 katika mechi nyingine iliyochezwa mapema siku hiyo.

Kocha mkuu wa Emerging Stars Ken Odhiambo aliipongeza timu hiyo kwa mwanzo mzuri dhidi ya Zambia.

"Zambia haikuwa timu rahisi na tulijua tukitaka kushinda mchezo huu tunatakiwa kufunga mabao ya mapema, tunatakiwa kufanya kazi zaidi na mechi ijayo tutakuwa tofauti," alisema.

Kenya itasafiri hadi Wolfson Stadium Jumapili Juni 30, kumenyana na Comoro, kabla ya kucheza mechi yao ya mwisho ya kundi dhidi ya Zimbabwe Jumanne Julai, 2024.