Mkufunzi wa Arsenal Mikel Arteta akubali mkataba mpya hadi 2027

Meneja wa Arsenal Mikel Arteta amekubali kutia saini mkataba mpya wa miaka mitatu na klabu hiyo.

Muhtasari

•Mhispania huyo alitarajiwa kumaliza kandarasi yake mwishoni mwa msimu huu lakini sasa anatarajiwa kusalia hadi 2027.

Mikel Arteta, meneja wa Arsenal.
Mikel Arteta, meneja wa Arsenal.
Image: Facebook

Meneja wa Arsenal Mikel Arteta amekubali kutia saini mkataba mpya wa miaka mitatu na klabu hiyo.

Mhispania huyo alitarajiwa kumaliza kandarasi yake mwishoni mwa msimu huu lakini sasa anatarajiwa kusalia hadi 2027.

The Gunners walimteua Arteta, ambaye alikuwa akifanya kazi kama kocha chini ya Pep Guardiola katika klabu ya Manchester City wakati huo, kuchukua nafasi ya Unai Emery kama kocha mwezi Desemba 2019.

Aliiongoza Arsenal kushinda fainali ya Kombe la FA mwishoni mwa kampeni ya 2019-2020 na kutwaa taji lake la kwanza kuu kama meneja.

Mkataba mpya wa Arteta unatarajiwa kuthibitishwa kabla ya mechi ya Jumapili ya London kaskazini huko Tottenham.

Arsenal wamemaliza katika nafasi ya pili nyuma ya Manchester City katika Ligi ya Premia katika misimu miwili iliyopita huku mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 42 akijaribu kuiongoza klabu hiyo kutwaa taji lao la kwanza la ligi kuu tangu 2003-04.

Baada ya mechi tatu msimu huu Arsenal wanashika nafasi ya nne, wakiwa wameshinda mechi zao mbili za kwanza dhidi ya Wolves na Aston Villa kabla ya kulazimishwa sare na Brighton.

Kiungo wa kati wa zamani, Arteta alicheza mechi 150 akiwa na The Gunners wakati wa uchezaji wake na pia alikuwa nahodha wa timu hiyo.