Dominic Solanke kurejea mechi ya debi dhidi ya Arsenal Jumapili

Alipata jeraha mechi yake ya kwanza katika timu ya Spurs

Muhtasari

• Dominic Solanke alipata jeraha mechi ya ufunguzi wa ligi mnamo tarehe 19 Agosti dhidi ya Leicester.

Kocha wa timu ya Tottenham Hotspur
Ange Postecoglou Kocha wa timu ya Tottenham Hotspur
Image: X//Tottenham Hotspur

Kocha wa Tottenham Hotspurs Ange Postecoglou amedokeza kuwa mshambuliaji Dominic Solanke huenda atarejea kikosini katika mechi ya Jumapili dhidi ya Arsenal.

Vile vile kocha Ange amesema kuwa Micky van de Ven alirejea mazoezini wiki mbili zilizopita baada ya kukosa mechi ya pili ya Tottenham ya msimu huu dhidi ya Newscastle.

Meneja wa Hotspurs amesema kuwa Micky yuko sawa na tayari kucheza katika mechi ya debi ya Londan Kaskazini dhidi ya Arsenal.

"Dom pia ameimarika na amefanya mazoezi wiki hili lote. Bado tuna siku mbili na matumaini kuwa atafaulu katika mazoezi na atakuwepo." Alisema kocha Ange.

Dominic Solanke alipata jeraha katika mechi yake ya kwanza kuchezea Tottenham mwanzoni mwa msimu wa 2024/25 mnamo tarehe kumi na tisa Agosti. Mechi hiyo ilikuwa dhidi ya Leicester iliyoishia kwa sare ya kufungana bao moja. 

Tottenham Hotspurs inashikilia nafasi ya kumi kwenye jedwali kwa alama 4 baada ya kutoka sare mechi moja, kushindwa moja na Newscastle na kushinda Everton mabao manne. 

Wakati huo, Tottenham imetangaza ushirikiano mpya wa matangazo ya mtandaoni na kampuni ya AIMS