Raheem Sterling afungia Arsenal bao lake la kwanza

Sterling alifungua ukurasa wake katika Arsenal kwa bao la kipindi cha pili katika mechi ya awamu ya Carabao tatu uwanjani Emirates.

Muhtasari

• Declan Rice aliweka Arsenal kifua mbele baada ya dakika 16 huku Nwaneri akifungia Arsenal bao la pili dakika ya 37 na bao lake la kwanza kwa klabu hiyo.

Raheem Sterling
Raheem Sterling

Raheem Sterling alifunga bao lake la kwanza la Arsenal na Jack Porter akawa mchezaji mwenye umri mdogo zaidi kuwahi kuanza mechi katika timu ya Arsenal katika ushindi wa 5-1 dhidi ya Bolton kwenye Kombe la Carabao usiku wa Jumatano, huku Liverpool ikifuzu hatua ya 16 bora kwa ushindi wa 5-1 dhidi ya West Ham.

Sterling alifungua ukurasa wake katika klabu ya Arsenal tangu alipohamia Emirates kutoka Chelsea siku ya mwisho ya uhamisho kwa bao la kipindi cha pili katika mechi ya awamu ya tatu ya dimba la Carabao uwanjani Emirates.

Mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 29 atatumai bao lake litakuwa mwanzo wa safari yake pevu baada ya hali tete akiwa Chelsea.

Meneja wa Arsenal Mikel Arteta alikuwa amefanya mabadiliko saba kutoka sare ya 2-2 Jumapili dhidi ya mabingwa wa Ligi ya Primia Manchester City, ikiwa ni pamoja na kumpa kipa chipukizi Porter mechi yake ya kwanza iliyovunja rekodi ya Arsenal badala ya David Raya aliyejeruhiwa.

Akiwa na umri wa miaka 16 na siku 72, Porter alikuwa mchezaji mwenye umri mdogo zaidi kuwahi kuanza kuichezea Arsenal, akimpiku Cesc Fabregas, aliyekuwa na umri wa miaka 16 na siku 177 alipocheza dhidi ya Rotherham mwaka 2003.

Porter alikuwa mchezaji wa pili mwenye umri mdogo zaidi katika Arsenal kwa ujumla baada ya Ethan Nwaneri, ambaye alikuwa na umri wa miaka 15 na siku 181, alipocheza mechi yake ya kwanza mwaka 2022.

Declan Rice aliweka Arsenal kifua mbele baada ya dakika 16 huku Nwaneri akifungia Arsenal bao la pili dakika ya 37 na bao lake la kwanza kwa klabu hiyo.

Nwaneri alifunga tena dakika nne baada ya kipindi cha pili kwa mkwaju wa yadi 12.

Sterling alifunga bao dakika ya 64, akiunganisha krosi maridadi ya Saka huku Kai Havertz akitia kimyani bao la tano.