Droo ya raundi ya 4 ya Kombe la Carabao yatangazwa, Arsenal yapata mpinzani mwepesi zaidi

Ratiba ya raundi ya nne ya Kombe la Carabao linaloshirikisha Vilabu vya Uingereza imetoka

Muhtasari

•Droo ya hatua inayofuata ilifanywa kufuatia kukamilika kwa hatua ya 32 mnamo Jumatano usiku.

•Mechi mbili za mwisho zilichezwa Jumatano huku mechi moja kati ya Newcastle na AFC Wimbledon ikiahirishwa.

Carabao Cup
Image: HISANI

Ratiba ya raundi ya nne ya Kombe la Carabao linaloshirikisha Vilabu vya Uingereza imetoka.

Droo ya hatua inayofuata ilifanywa kufuatia kukamilika kwa hatua ya 32 mnamo Jumatano usiku.

Mechi mbili za mwisho zilichezwa usiku wa Jumatano huku mechi moja kati ya Newcastle United na AFC Wimbledon iliyokuwa ichezwe Jumanne ikiwa imeahirishwa. Mchuano huo sasa utachezwa tarehe Mosi  mwezi Oktoba 2024 na mshindi atamenyana na klabu ya Chelsea.

Droo ya mechi za raundi ya nne itakayochezwa tarehe Oktoba 30, 2024 ni kama ifuatavyo;

o Southampton vs Stoke: 30/10/2024

o Manchester United vs Leicester: 30/10/2024  

o Brighton vs Liverpool: 30/10/2024

o Brentford vs Sheffield Jumatano: 30/10/2024

o Tottenham vs Manchester City: 30/10/2024

o Preston North End vs Arsenal: 30/10/2024

o Aston Villa vs Crystal Palace: 30/10/2024