Harry Kane azungumza baada ya watoto wake kuhusika katika ajali ya gari nchini Ujerumani

Harry Kane amesema watoto wake 'wako sawa' baada ya ajali ya gari nchini Ujerumani

Muhtasari

•Ajali hiyo ilitokea Jumatatu karibu na Munich, ambapo nahodha huyo wa Uingereza anachezea Bayern Munich.

Image: BBC

Watoto watatu wakubwa wa Harry Kane wamepelekwa hospitalini wakiwa na majeraha madogo baada ya kuhusika katika ajali ya magari matatu nchini Ujerumani.

Ajali hiyo ilitokea Jumatatu saa 17:15 BST karibu na Munich, ambapo nahodha huyo wa Uingereza anachezea Bayern Munich.

Mkuu wa zimamoto wa eneo hilo aliambia BBC kwamba wote waliohusika walikuwana "bahati sana" kwani hakuna aliyejeruhiwa vibaya.

Msemaji wa Kane aliongeza: "Hawajambo na walikwenda hospitali kwa uchunguzi wa kawaida tu."

Mshambulizi huyo alikuwa ametoka tu kutua London kwa ajili ya mechi ya timu yake ya robo fainali ya Ligi ya Mabingwa dhidi ya Arsenal siku iliyofuata wakati ajali hiyo ilipotokea, gazeti la Ujerumani la Bild liliripoti.