Kunani? Jadon Sacho afuta kauli mbaya alizotoa dhidi ya kocha Erik ten Haag

Sancho alikuwa amemkosoa kocha ten Hag baada ya kumsema vibaya katika mahojiano.

Muhtasari

•Jadon Sancho alichukua hatua hiyo siku ya Jumanne, takriban wiki moja na nusu tu baada ya kumkosoa ten Hag.

•Katika taarifa yake, Sancho alitupilia mbali madai ya meneja wake na kusema kwamba alijitolea vyema katika mazoezi.

ten Hag alikosoa mchezo wa Jadon Sancho
Image: HISANI

Winga wa klabu ya Manchester United Jadon Sancho amefuta kauli mbaya alizotoa dhidi ya meneja Erik ten Hag mapema mwezi huu.

Mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 23 ambaye amekumbwa na masaibu mengi katika klabu ya United alichukua hatua hiyo siku ya Jumanne, takriban wiki moja na nusu tu baada ya kumkosoa ten Hag. Alikuwa amezamia kwenye Twitter kumkosoa kocha huyo wa Uholanzi baada ya kumsema vibaya katika mahojiano.

Mapema mwezi huu, Jadon Sancho alijibu kwa uchungu mwingi baada ya kocha Erik ten Hag kudai kuwa alishindwa kufikia viwango vya mazoezi vinavyohitajika kwa kushirikiswa kwenye kikosi cha kucheza dhidi ya Arsenal.

Image: TWITTER// JADON SANCHO

Katika taarifa yake, Sancho alitupilia mbali madai ya meneja wake na kusema kwamba alijitolea vyema katika mazoezi.

Mchezaji huyo wa Uingereza alisema madai ya kocha wake ni ya uongo na kuwataka mashabiki wasiamini yote wanayosikia.

"Naomba msiamini kila mnachosoma. Sitaruhusu watu kusema mambo ambayo si ya kweli kabisa, nimejiendesha vizuri sana katika mazoezi wiki hii. Naamini kuna sababu nyingine za jambo hili ambazo sitazizungumzia, Nimekuwa mbuzi wa kafara kwa muda mrefu jambo ambalo si sawa!” Sancho alisema.

Licha ya kutochaguliwa kwenye mechi dhidi ya Wanabunduki, mchezaji huyo wa kimataifa wa Uingereza mwenye umri wa miaka 23 hata hivyo alidokeza kuwa anaheshimu maamuzi yaliyofanywa na wakufunzi.

Aidha, aliweka wazi kuwa licha ya kudhalilishwa, ataendelea kutia juhudi zake zote kwa ajili ya Mashetani Wekundu.

"Ninachotaka kufanya ni kucheza mpira huku nikitabasamu na kuisaidia timu. Naheshimu maamuzi yote yanayofanywa na wakufunzi, nacheza na wachezaji wa ajabu na nashukuru kufanya hivyo jambo ambalo najua kila wiki ni changamoto. Nitaendelea kupigania beji hii hata iweje!" alisema.

Baada ya timu yake kushindwa na wanabunduki Jumapili jioni, ten Hag alieleza kwa nini mchezaji huyo wa kimataifa wa Uingereza hakuchaguliwa kwenye mechi hiyo.

Kocha huyo kutoka Uholanzi alisema kwamba Sancho alishindwa kufikia viwango vya mazoezi vinavyohitajika ili kuchaguliwa

"Jadon hakuwepo, kutokana na uchezaji wake kwenye mazoezi, hatukumchagua. Lazima ufikie kiwango kila siku katika Manchester United ili tuweze kufanya maamuzi kwenye mstari wa mbele, kwa hivyo kwa mchezo huu hakuchaguliwa, " Hag kumi alisema.

Jadon Sancho alichaguliwa katika mechi tatu za ufunguzi wa msimu wa Ligi Kuu, akitokea benchi kila mara.