Messi aonyesha upendo kwa Ronaldo katika inayodaiwa kuwa mechi ya mwisho kumenyana

Lionel Messi alichapisha video yake akimkumbatia Christiano Ronaldo.

Muhtasari

•Messi alitangulia kufunga kwenye mechi hiyo ya kusisimua katika dakika ya 3 kabla ya Ronaldo  kutia penalti wavuni katika dakika ya 34 na bao nyingine dakika 22 baadae na kufunga kipindi cha kwanza.

• Messi alichapisha video yake akimkumbatia Ronaldo kwenye ukurasa wake wa Instagram, pengine kama kiashiria kwamba hana kinyongo na mshambuliaji huyo mwenzake.

wakati wa mechi ya kirafiki kati ya PSG na Riyadh All Stars Alhamisi usiku
Messi na Ronaldo wakati wa mechi ya kirafiki kati ya PSG na Riyadh All Stars Alhamisi usiku
Image: HISANI

Wanasoka wawili bora zaidi kuwahi kucheza duniani, Lionel Messi na Christiano Ronaldo wote walifunga huku PSG ya Ufaransa ikiichapa Riyadh All Stars wa Saudi Arabia 5-4 katika mechi ya kirafiki iliyochezwa kwenye Uwanja wa Kimataifa wa King Fahd, nchini Saudi Arabia siku ya Alhamisi usiku.

Messi alitangulia kufunga kwenye mechi hiyo ya kusisimua katika dakika ya 3 kabla ya Ronaldo  kutia penalti wavuni katika dakika ya 34 na bao nyingine dakika 22 baadae na kufunga kipindi cha kwanza.

Kipindi cha pili kilishuhudia mabao mengi huku Marquinhos, Sergio Ramos, Kylian Mbappe na Hugo Ekitike wakifunga bao moja kila mmoja na kufanikisha ushindi wa PSG. Jahn Hyun-soo na Talisca walifungia Riyadh-All stars mabao mengine mawili huku Juan Bernat wa PSG akionyeshwa kadi nyekundu kwenye mchuano huo.

Mechi kati ya timu hizo mbili huenda ikawa mchuano wa mwisho ambao washambuliziMessi na Ronaldo ambao kwa muda mrefu wamekuwa wakilinganishwa kwa muda mrefu na kuchukiliwa kuwa mahasidi wanakutana.

Ronaldo ambaye kwa sasa anachezea klabu ya Al Nassr nchini Saudi Arabia ana umri wa miaka 37 huku Messi akiwa na miaka 35. Kwa kawaida, umri wa kustaafu katika soka huwa 40 ingawa wachezaji wengi hustaafu kabla.

Licha ya kudhaniwa kuwa mahasidi wakubwa, Messi na Ronaldo walikumbatiana kabla ya mechi hiyo ya kirafiki. Wawili hao walionekana kufurahiya kukutana na na walionyesha tabasamu huku wakisalimiana.

Baada ya mchuano huo, Messi alichapisha video yake akimkumbatia Ronaldo kwenye ukurasa wake wa Instagram, pengine kama kiashiria kwamba hana kinyongo na mshambuliaji huyo mwenzake.

Ronaldo pia alipakia video na picha kadhaa kutoka kwa mechi hiyo.

Image: INSTAGRAM// LIONEL MESSI