Watu 544 wapatikana na virusi vya corona huku 13 wakiaga dunia – Aman

Watu 544 wamepatikana na virusi vya corona baada ya sampuli za watu 2,653 kupimwa chini ya saa 24.

Idadi hiyo sasa inafanya taifa kuwa na watu  22, 597 walio na virusi hivyo kufikia sasa.

Aidha wagonjwa wengine 13 wametangazwa kufariki na kufikisha watu 382 waliofariki kufikia sasa kutokana na ugonjwa huo

Katibu wa utawala wa wizara ya Afya  Rashid Aman amesema kuwa watu 263 waliokuwa wamelazwa katika hospitali tofauti nchini wameruhusiwa kwenda nyumbani na kufikisha watu  8,740 waliopona.

Image

Aman pia amethibitisha kuwa wahudumu  wanane  wa afya hadi kufikia sasa wamefariki kutokana na virusi hivyo huku  wa hivi punde kupoteza maisha yake akiwa Mariam  Awuor kutoka kaunti ya Kisii.

Kati ya visa hivyo vipya Nairobi imeandikisha visa 412 , Kiambu 27, Machakos 17, Kajiado 17, Garissa 16, Uasin Gishu 14, Mombasa 9, Nakuru 8, Nyeri 5, Narok 5, Makueni 4 Laikipia 2, Muranga, Kilifi, Busia, Embu, Bungoma, kisii, Kwale na  Meru  zote zikiwa zimeandikisha kisa kimoja.

Wakati huo huo Aman akana madai kuwa kuna baadhi ya wahudumu wa afya ambao wamekosa kulipwa mishahara yao akisema serikali kuu pamoja na zile za kaunti  nchini zimekuwa zikishirikiana ili kufanikisha malipo ya wahudumu hao  .

Image

Serikali ya Homa Bay yasubiri ripoti ya kubaini kilichosababisha kifo cha Mariam Awuor

  Ameongeza kuwa serikali imeweka mikakati mwafaka ya kuajiri wahudumu zaidi ili kusaidiana na wenzao wanaokabiliana na janga hilo.

Amesisitiza umuhimu wa wakenya kuendelea kuzingatia masharti yaliyowekwa na wizara ya afya kama njia ya kupunguza msambao wa corona.

Akisoma takwimu hizo mpya za maambukizi ya corona, Aman ametuma risala za rambirambi kwa familia ya Mariam Awuor ambaye alitangazwa kufariki kutokana na virusi hivyo.

 

 

Watu 247 wapatikana na virusi vya corona

Akitoa taarifa ya kila siku kuhusiana na virusi vya corona ,katibu msimamizi katika wizara ya afya Rashid Aman amesema watu 247 waoatikana na virusi hivyo na kufikisha idadi nchini kuwa 7,188.

Watu 39 wameruhusiwa kuondoka hospitalini na kufikisha watu 2,149 waliopona.

Wagonjwa wawili wamefariki na kufikisha watu 154 waliofariki kutokana na virusi hivyo.

Image

Kati ya visa hivyo vipya,wakenya ni 242 huku watu 5 wakiwa raia wa kigeni.

Wanaume ni 164 huku wanawake wakiwa 63,waathiriwa wakiwa kati ya miaka 1 na 100.

Nairobi imesajili visa 154 kati ya visa vipya vilivyosajili huku kaunti ya Mombasa ikiwa na watu 35.

Kaunti zingine zilizoathirika ni  Kajiado 15, Busia 12, Kiambu 12, Uasin Gishu 4, Machakos 4, Garissa 4, Murang’a 2, Nakuru 2, Siaya 2, Lamu 1, & Nyamira 1.

Wakati uo huo Aman amewataka wazazi kuwapeleka wasichana wa miaka 10 kupata chanjo ya HPV.

Visa vilivyosajiliwa katika kaunti ya Nairobi vimetokea maeneo, yafuatayo Kibra (35), Westlands (28), Dagoretti North (16), Kasarani (13), Embakasi East (12), Starehe (10), Langata (8), Makadara (6), Embakasi South (5), Embakasi West (4), Kamukunji (4), Roysambu (4), Dagoretti South (3), Ruaraka (3), & Embakasi Central (2).

Unashauriwa kula vyakula bora ili kujizuiya na maradhi ya kuambukizana

Unataka kujiepusha na maradhi ya kuambkukizana kama Corona?,Naam unashauriwa kula vyakula bora kama njia ya kuongeza uwezo wako wa kuwa na madini ya kutosha mwilki ya kuzuiya kuambukizwa maradhi ambayo yanaweza kusambaa kutoka kwa mtu mmoja hadi mwengine.

Kando na wosia wa kuvalia barakoa na kuosha mikono kila mara,maafisa wa afya sasa wanawataka wananchi kuangazia mlo bora haswa kwa watu ambao wana maradhi  mengine kama Kisukari,Ukimwi .

“People living with non-communicable diseases should eat healthily by consuming a healthy diet based on locally available foods. A balanced diet is critical for preventing and managing non-communicable diseases and their complications during this pandemic period and beyond,” Dr Aman.

AMAN 1

Uncle Willy,Tuko na wewe! Omanga amwambia Ruto

Aman amewataka wananchi kula zaidi matunda na kupunguza idadi ya vyakula ambavyo vina sukari nyingi na kuendelea kufanya mazoezi.

“Consume plenty of vegetables from all the subgroups including spinach, kales, and cabbages. Eat a variety of fruits that are in season and readily available in the market, oranges, bananas watermelon and others. Also, eat plenty of protein food too such us beans,”

Amesema ili kufahamisha wananchi umuhimu wa kuendelea kuzingatia lishe bora kama njia ya kupunguza idadi ya magonjwa yanasambaa kutoka kwa mtu mmoja hadi mwengine.

 

Watu 268 wapatikana na virusi vya corona- Aman

Watu 268 wamepatikana na virusi vya corona baada ya kufanyiwa vipimo na kufikisha watu 6941 walioathirika na virusi hivyo nchini.

Kati ya visa hivyo vipya hii leo, wakenya ni 159 huku raia wa Kigeni wakiwa 9.

Watu wengine 20 wameruhusiwa kuondoka hospitalini na kufikisha watu 2,109 waliopona.

Nairobi inaongoza na visa 175 huku mitaa ya Dagoreti North ikiwa na watu 34 na mtaa wa Kibra ikiwa na 29.

Image

Watu 3 wamefariki kutokana na virusi hivyo na kufikisha watu 152 waliofariki kufikia sasa kutokana na virusi hivyo.

Kufikia sasa Kenya imewapima watu 176,059 kuhusiana na virusi hivyo.

Aman amesema asilimia kubwa ya watu waliofariki kutokana na virusi hivyo nchini walikuwa na matatizo mengine ya afya.

Mombasa imesajili visa 28,kaunti ya Busia ikiwa na visa 18 Kiambu 11, Kajiado 9, Migori 9, Uasin Gishu 8, Machakos 6, Narok (2), Makueni (1), & Muranga (1).

 

 

 

 

Watu 176 wapatikana na virusi vya corona- DKT Rashid Aman

Dkt Rashi Aman amesema baada ya sampuli za watu 2,419 kufanyiwa vipimo chini ya saa 24 kuhusiana na virusi vya corona,watu 176 walipatikana na virusi hivyo na hivyo kufikisha wagonjwa 6,366 walioathirika kutokana na corona.

Wakati uo huo watu 26 waliokuwa wamelazwa hospitalini wameruhusiwa kuondoka hospitalini baada ya kupata nafuu na kufikisha watu 2,039 waliopona.

Aidha wagonjwa wanne wamefariki na kufikisha watu 148 waliopoteza maisha kutokana na virusi hivyo.

Image

Kati ya visa hivyo vipya ,wanaume ni 100,huku wanawake wakiwa 76.

Waathiriwa ni wa kati ya miaka 3 hadi 78.

Visa 99 vimetokea kaunti ya Nairobi huku kaunti ya Mombasa ikisajili visa 20 kati ya vile vilivyosajiliwa hii leo.

 

 

Watu 120 zaidi wapatikana na virusi vya corona- Rashid Aman

Watu 120 zaidi wamepatikana na virusi vya corona baada ya kufanyiwa vipimo chini ya saa 24 na kufanya taifa la Kenya kusajili idadi ya jumla ya watu  6190 walioathiriwa na virusi hivyo.

Watu hao wamepatikana baada ya sampuli za watu 2,221 kufanyiwa vipimo.

Wakati huo huo watu 42 wameruhusiwa kuondoka hospitalini na kufikisha watu 2,014 waliopona virusi vya corona.

Aidha mgonjwa mmoja amefariki na kufikisha watu 144 waliopoteza maisha kutokana na virusi hivyo hatari.

 

Kati ya visa hivyo vipya, Wanaume ni 86 huku wanawake wakiwa 36.

Nairobi imesajili visa 67 kati ya visa hivyo vipya huku kaunti ya Mombasa ikisajili visa 17.

Kufikia sasa tangu kuripotiwa kwa virusi hivyo nchini, kaunti zifuatazo ndizo zilizosajili idadi kubwa ya watu walioambukizwa virusi hivyo, Nairobi 3031, Mombasa 1445, Busia 407, Kajiado 242 na Kiambu 222.

 

MHARIRI; DAVIS OJIAMBO

Watu 213 wamepatikana na virusi vya corona nchini- Aman

Kenya sasa ina wagonjwa 4,257 wa corona baada ya watu wengine 213 kupatikana na virui hivyo  baada ya kufanyiwa vipimo chini ya saa 24.

Kulingana na Aman kaunti ya Nairobi inaongoza na visa 136 huku Mombasa ikiwa na 32.

Kati ya visa hivyo vipya, wakenya ni 198, raia wa kigeni 15.

Kulingana na jinsia, Aman amesema wanaume ni 151 huku wanawake wakiwa 62.

Aman amesema kuwa watu 106 waliokuwa wameathirika na virusi hivyo wameruhusiwa kuondoka hospitalini baada ya kupata nafuu na kufikisha watu 1,459 waliopona.

Waathiriwa hao ni wa kati ya miaka mmoja hadi 73.

Watu wengine 10 wamefariki na kufikisha idadi ya wale walioaga nchini kuwa 117.

Image

Wakati uo huo Aman amewataka wakenya kuendelea kuwa ange kutokana na hatua ambapo virusi hivyo vya corona vinaendelea kusambaa nchini.

Amewataka wakenya kuendelea kuheshimu masharti yaliyowekwa na wezara ya afya kama njia ya kupunguza maambukizi.

 

Wakenya 184 wamepatikana na virusi vya corona nchini- Rashid Aman

Katika kikao cha kila siku kwa taifa kuhusiana na virusi vya corona nchini,katibu msimamizi katika wizara ya afya Dr Rashid Aman amesema watu 184 wamepatikana na virusi hivyo hatari.

Kutokana na takwimu hizo mpya sasa Kenya ina wagonjwa 4044 walioambukizwa corona.

Wanaume ni 129 huku wanawake wakiwa 55.

Nairobi ina 111 ,Mombasa 19,Kajiado 14 Meru 13 ,Busia 6.,Nakuru 4,Machakos 3,Kwale 1,Kisumu 1,Garrissa 1,Taita Taveta 1,Vihiga 1.

Kufikia sasa majimbo 40 yameandikisha visa hivyo vya corona.

Watu 27 wameruhusiwa kuondoka hospitalini na kufikisha watu 1,354 waliopona.

Wagonjwa wawili wamefariki na kufikisha watu 107 waliofariki.

Visa vipya vilivyosajiliwa katika kaunti ya Busia vimetokana na madereva wa malori waliofanyiwa vipimo.

Aman amesikitikia idadi kubwa ya vifaa gushi vya kupima virusi hivyo nchini akisema ni sharti serikali sasa ianze kupiga msasa katika maduka majula yanayoendelea kuwauzia wakenya vifaa hivyo.

Amesema ni sharti watu wafanyiwe vipimo katika vituo vilivyodhibitishwa na serikali.

 

 

Watu 72 wameruhusiwa kuondoka hospitalini- Rashid Aman

Katibu msimamizi katika wizara ya afya Dr Rashid Aman amesema watu 72 waliokuwa wamelazwa hospitalini baada ya kuambukizwa virusi vya corona sasa wameruhusiwa kwenda nyumbani baada ya kupata nafuu.

Kufikia sasa, Kenya imeandikisha watu 1164 waliopona kutokanana virusi hivyo.

Wakati uo huo watu 90 wamepatikana na virusi hivyo na kufikisha watu 3305 walioambukizwa.

Watu 62 ni wanaume huku wanawake wakiwa 28.

Image

Kaunti ya Nairobi iko na visa 36 huku Mombasa ikiwa na 34.

Visa 12 vilivyoandikishwa katika kaunti ya Busia ni madereva wa Malori waliotokea katika mpaka wa Malaba.

Watu wanne wanaripotiwa kuaga dunia kutokana na virusi hivyo na kufikisha watu 96 waliofariki.

Aman wakati uo huo amezindua mpango wa wananchi kujitokeza na kutoa damu ili kusaidia kuongeza idadi ya damu katika hosptali mbalimbali nchini.

Kufikia sasa Kenya imewapima watu 108,666 kuhusiana na virusi hivyo.

 

Watu 175 wameruhusiwa kuondoka hospitalini baada ya kupata nafuu dhidi ya corona

Katibu msimamizi katika wizara ya afya nchini Rashid Aman amesema kwa mara nyingine tena serikali imewaruhusu watu 175 kutoka hospitalini baada ya kupata nafuu na kufikisha watu 1048.

Wakati uio huo watu wengine 105 wamepatikana na virusi vya corona baada ya kufanyiwa vipimo na kufikisha watu 3094.

Image

Kati ya visa hivyo vipya vya maambukizi ,wakenya ni 96 huku raia wa kigeni wakiwa 9.

Visa vilivyosajiliwa katika kaunti ya Kisumu na Busia vimetokana na madereva wa malori waliofanyiwa vipimo.

Aidha mtu mmoja amepoteza maisha yake kutoka na virusi hivyo na kufikisha watu 89 waliofariki.Image

Aman amesema kutokana na ongezeko la madereva wa masafa marefu kuendelea kuandikisha idadi  kubwa,serikali imeanza kuweka mikakati ya kusaidia kaunti hiyo ili kuzuiya maambukizi.

Nairobi imeandikisha visa 43 huku kaunti ya Busia ikiandikisha 18.

Aman pia amezindua mradi wa kuanza kuwahudumia wagonjwa wa corona nyumbani ambao hali yao ya afya si mbaya ikilinganishwa na baadhi ya wagonjwa wengine.

Kufikia sasa Kenya imwapima watu 102,956 kuhusiana na virusi vya corona.

Katika takwimu za hii leo wanaume ni 77 huku wanawake wakiwa 28.

Waathiriwa ni wa umri wa kati ya miaka miwili  na 77.

Visa hivyo vimetokea maeneo yafuatayo Nairobi, 43 Busia, 18 Mombasa, 11 Turkana, 7 Migori, 6 Kwale & Kiambu, 5 cases each, Kilifi, Machakos na Taita Taveta 3 , Kisumu, 2 Uasin Gishu, Siaya, Kajiado na  Garissa, ikisajili kisa kimoja.