Bunge lawapa mzigo walipa ushuru ili kuwalipa pensheni wabunge wa zamani

Walipa ushuru watalazimika kubeba mzigo zaidi  ili kufadhili pensheni ambayo serikali inataka kuwalipa wabunge wa zamani mbao walihudumu kati ya mwaka wa 1984 na 2001

Bunge litapiga kura leo kufanyia marekebisho sheria ya malipo ya uzeeni ili kuwapa wabunge hao wa zamani  pensheni watakayolipwa kila mwezi maisha yao yote.

Maseneta 25 wakula njama ya kuyakataa mapendekezo ya Uhuru na Raila

Marekebisho hayo yaliofanywa kwa sheria ya  malipo ya  uzeeni kwa wabunge  yatapitishwa kwa urahisi bungeni. Pensheni hiyo ya kila mwezi  itaongezwa kutoka shilingi 2000 kwa sasa hadi shilingi 125,000 kila mwezi.

Malipo ya fedha hizo huenda yakarejeshwa nyuma hadi Julai mwaka wa 2010  hatua ambayo  huenda ikailazimu serikali kutoa mamilioni ya pesa kutekeleza pensheni hiyo.

Nitakushughulikia vilivyo! Wetangula na wenzake wamuonya Eseli Simiyu

Iwapo rais Uhuru Kenyatta ataidhinisha mswada huo kuwa sheria wabunge 290 huenda wakaanza kulipwa kiasi cha chini ya shilingi 100,000 kama pensheni kila mwezi

Ofisi ya bajeti bungeni  imeashiria kwamba serikali huenda ikawalipa wabunge hao wa zamani shilingi milioni 15.1 kila mwezi.

 

 

Senate yapiga marufuku mikutano ya kamati kuzuia maambukizi ya Covid 19

Hakuna seneta atakayekubaliwa kwenda bungeni kwa mikutao ya kamati ya senate kuanzia wiki ijayo kama njia moja ya kuzuia usambaaji wa virusi vya corona .

Tangazo hilo linajiri siku  chache tu baada ya bunge la taifa kupunguza shughuli zake kwa hofu ya wafanyikazi na wbaunge kuambukizwa ugonjwa huo. Spika wa senate Ken Lusaka  amesema mikutano yote inayowalazimu maseneta kukutana ana kwa ana imefutiliwa mbal kwa mwezi mmoja ili kuzuia usambaaji wa virusi hivyo .

Tanzia:Mhadhiri wa UoN Ken Ouko afariki dunia kwa ajili ya Covid 19

Spika  amesema hali itatathminiwa baada  ya mwezi mmoja  na kamati ya senate kuhusu uhasibu ndio inayoweza kuandaa mikutano  kila baada ya muda Fulani  inapohitajika .

Wiki jana spika wa bunge la taifa Justin Muturi alipiga marufuku mikutano yote ya kamati na kushauri dhidi ya mikutano yote ya ana kwa ana katika majengo ya bunge . Agizo hilo lilitolewa baada ya kuibuka ripoti kwamba huenda wabunge kadhaa na wafanyikazi wa bunge wameambukizwa ugonjwa wa corona .

Jumanne iliyopita  kiongozi wa wachache bungeni John Mbadi alifichua kwamba wafanyikazi 36 wa bunge wamepatikana na Covid 19

 

 

Je BBI itaporomoka? Raila awaambia maseneta wa ODM kukataa mfumo wa ugavi wa mapato

Mwafaka wa BBI  huenda upo mashakani baada ya  washirika wa kisiasa wa kiongozi wa ODM Raila Odinga kudai kwamba kuna njama ya kumtema.

Wandani wa Raila wanadai kwamba wenzao katika upande wa Jubilee wameanza kuwatolea vitisho ili kushawishi maamuzi yao kuhusu mfumo unaotumiwa kugawa mapato kwa serikali za kaunti baada ya kuhusisha kura ya kupitisha mfumo huo na hatima ya mwafaka wa  BBI.

Je,kifaa hiki kitawazuia wanawake kuambukizwa HIV?

Wamedai kwamba washirika wa rais Kenyatta  wamekuwa wakiashiria kwamba mchakato mzima wa BBI ni mradi wa Raila. Raila na washirika wake hawajapendezwa na hatua ya kujaribu kutumiwa kwa vitisho hivyo vya BBi ili kuwashurutisha wapitishe  mfumo mpya wa ugavi wa mapato ambao utapunguza kabisa mgao katika kaunti nyingi ambazo ni ngome ya Raila.

Mfumo huo mpya kulingana na  washirika wa Raila  ni njama ya kutikisa  uungwaji mkono wa Raila katika ngome zake  ili kuwafanya wafuasi wake kumgomea wakati wa uchaguzi wa mwaka wa 2022.

“ Njama ni kumsalimisha Raila ili wampate mtu wanayemtaka. Mfumo huu wa ugavi wa mapato utazua lalama kubwa zaidi kuliko inavyodhaniwa’ amesema mwanachama sugu wa ODM.

MCA’s wa Nairobi waapa kumtimua Spika Elachi

Kwa mfano anasema maeneo ambayo yanafaa kupata mgao wa juu ndio yatakayopata ufadhili wa chini na yametengwa kwa muda mrefu.

Gazeti la The Star limesema Raila alifanya mkutano wa njia ya mtandao na   kamati ya usimamizi wa chama na kuafikia kukataa mfumo huo unaopendekezwa na serikali.

Hatua hiyo huenda sasa ikarejesha tena uhasama wa kisiasa kati ya Odinga na  Rais Uhuru Kenyatta ambao walikuwa wameafikia makubaliano ya kushirikiana.

 

Bunge kukamilisha uchaguzi wa wanakamati leo

Mbunge  wa  Moiben Silas Tiren amechaguliwa kuwa mwenyekiti mpya wa kamati ya bunge kuhusu kilimo ili kuichukua afasi ya  mbunge wa mandera kusini Adan Ali .

Mudavadi kuzuru eneo la Mlima Kenya kujipigia debe kwa uchaguzi mkuu 2022

Ali  alikuwa miongoni mwa washirika 16 wa  naibu wa rais William Ruto kupigwa shoka kutoka kamati za bunge  mwezi jana na mageuzi yaliyoendeshwa na rais Uhuru Kenyatta . Mbunge huyo wa Moiben  alichaguliwa bila kupingwa siku ya alhamisi .

Mwakilishi wa akina mama wa  Laikipia  Catherine Waruguru alichaguliwa kuwa  naibu mwenyekiti wa kamati hiyo .anaichukua nafasi ya  mbunge wa Navakholo Emmanuel Wangwe,  aliyeteuliwa kuwa kiranja .Tiren  anaichukua nafasi hiyo alioyolazimika kuiacha baada ya Chama cha Jubilee kumpendelea Ali mwaka wa 2018.

Mbunge wa Shinyalu  Justus Kizito  na mwakilishi wa akina mama wa Nyamira  Jerusha Momanyi  walichaguliwa kuwa mwenyekiti na naibu mwenyekiti wa kamati ya matangazo na  makataba .walichaguliwa bila kupingwa .mbunge wa Limuru Peter Mwathi na mwenzake wa chepalungu  Gideon Koske  watahudumu katika kamati ya bunge kuhusu leba na huduma za kijamii kama mwenyekiti na naibu wake mtawalia .

Kinoti apata pigo baada ya mahakama kusema ni Haji pekee mwenye uwezo wa kufungulia mashtaka

Upande wa walio wengi na wachache tayari zimekubaliana kuhusu uongozi wa kamati mbali mbali  na uchaguzi utakuwa tu kama njia rasmi ya kuidhinisha mwafaka huo . Kwa mfano mwakilishi wa akina mama wa Homabay Gladys Wanga  amependekezwa kuwa mwenyekiti wa kamati ya fedha na mipango  na naibu wake atakuwa mbunge wa Roysambu  Waihenya Ndirangu

 

Serikali yaondoa sheria kali za kupambana na ufisadi

Serikali imeondoa bungeni sheria ambazo zingekabiliana  kikamilifu na ufisadi na  kufichua vita vya ndani kwa ndani miongoni mwa mashirika ya serikali  ambayo yana jukumu la kupambana na ulaji rushwa.

Kinoti apata pigo baada ya mahakama kusema ni Haji pekee mwenye uwezo wa kufungulia mashtaka

Miswada hiyo ilikuwa imetegemewa pakubwa sana kuweza kupiga jeki vita dhidi ya ufisadi  na ilikuwa imependekeza maafisa wote wa umma wanaoshtakiwa akiwemo naibu wa rais kuondoka afisini.

Hata hivyo imeibuka kwamba malumbano baina ya mashirika mbalimbali yamefanya miswada hiyo kuondolewa hasa baada ya shirika kutwaa mali  iliyopatikana kwa njia za kifisadi ARA kulalamika vikali.

ARA ilikuwa imesema kwamba sheria hizo zingeyafanya mashirika mengine ya serikali kuchukua sehemu ya majukumu yake.

Siku ya Jumatano, spika wa bunge Justin Muturi   alitangaza kwamba amekubali ombi la kiongozi wa wengi bungeni kuondoa marekebisho hayo katika sheria za kupambana na ufisadi.

Maseneta 20 wanataka kuwa magavana 2022

Muturi,  amesema katika ujumbe wake wa wabunge kwamba ni muhimu kutoa fursa kwa majadiliano zaidi kati ya mashirika mbalimbali ya serikali kabla ya marekebisho hayo kuwasilishwa tena bungeni .

Kasuku nje ndani kimya: Sudi, Wako hakusema neno hata moja bungeni mwaka wa 2019 – Mzalendo

Mbunge wa Kapseret Oscar Sudi  hakusema lolote   bungeni mwaka wa 2019,  imeonyesha  ripoti iliyotolewa na shirika la mzalendo.

Uhuru azindua baluni za internet za loon ili kutumia vyema mtandao wa 4G

Kulingana na tathmini ya  ripoti  za hapo awali, Sudi amedumisha sifa yake hiyo ya kutosema lolote bungeni tangu mwaka wa 2017. Mbunge huyo ni mtetezi mkubwa wa naibu wa rais William Ruto  na amekuwa  akitoa maoni kuhusu masuala ya kisiasa

bunge 2

Ripoti hiyo imeonyesha kwamba  seneta wa  Busia Amos Wako  hakuzungumza  katika seneti  mwaka jana  pamoja na viongozi  wengine walioteuliwa

Shhh! Mwanamke ashtakiwa kwa kuwaita polisi ‘wafisadi’ Riruta

Viongozi hao ni  miongoni mwa wajumbe 25  katika seneti na bunge la  taifa  ambao wametajwa kwa  utendakazi mbovu  katika kipindi hicho. Seneta wa Kajiado Philip Mpaayei,  wenzake  wateule  Christine Zawadi  na  Mercy Chebeni  walitajwa kwa utendakazi adimu.

Seneta  Ledama Ole Kina (Narok)  alitajwa kama mchapakazi zaidi katika seneti.

bunge 3

Alifuatwa na Moses Wetangula (Bungoma), Aaron Cheruiyot (Kericho), Ochilo Ayako (Migori)  na  Getrude Musuruve (Mteule).

Katika bunge la taifa mbunge wa Mumias Mumias West John Naicca; Samuel Arama (Nakuru West); James Gakuya (Embakasi North); George Aladwa (Makadara); Abdi Shurie (Balambala)  ni miongoni mwa waliotajwa kwa utendakazi mbovu  katika bunge na mijadala

Miongoni mwa waliotambuliwa kwa uchapakazi mzuri katika bunge ni  Millie Odhiambo (Suba North), David Ole Sankok

( Mteule ), Wilberforce Oundo (Funyula)  na Robert Pukose (Endebess).

Nipe Nikupe:Maseneta walimana makonde baada ya ushindi wa Ole Kina

Maseneta wawili wateule – Beatrice Kwamboka  na  Mary Seneta  walipigana makonde  bungeni  wakati wa uchaguzi wa naibu mwenyekiti  wa kamati ya bunge kuhusu afya .

Patashika ilizuka muda mfupi baada ya seneta wa Narok  Ledama Ole Kina  kutangazwa mshindi wa kinyang’anyiro hicho  dhidi ya  Seneta.

Seneta  alikuwa akiungwa mkono nan a baadhi ya  wanakamati hiyo wakiongozwa na  naibu kiranja  wa walio wengi  Farhiya Ali.

Kulingana na maseneta waliokuwa katika mkutano huo kundi la  Farhiya lilitumia sahihi bandia ya seneta Millicent Omanga ili kumpa ushindi   Seneta .

 

 

Who’s Next? Jeshi la Ruto Bungeni lapatwa na hofu baada ya washirika wake senate kufurushwa

Baada ya kuondolewa kwa washirika wa naibu wa rais William Ruto katika nafasi za uongozi wa senate ,washirika wake katika bunge la kitaifa sasa wapo  katika hali ya wasi wasi kwani  huenda ndio watakaolengwa .

uhuruto

Aluta Continua: Uhuru sasa kuwafurusha washirika wa Ruto Katika kamati za senate

Den Duale ,Ben Washiali na Kimani  Kimani Ichung’wa  wapo katika hatari ya kufurushwa katika nyadhifa za uongozi bungeni   baada ya kushtumiwa kwa kutokuwa waamonifu kwa kiongozi wa chama chao cha Jubilee Rai Uhuru Kenyatta. Baada ya kufaulu kutekeleza mageuzi  katika senate  washirika wa rais Uhuru Kenyatta sasa wamepata ujasiri wa kuzidisha adhabu yao hadi bungeni  na imeibuka kwamba mkutano wa wabunge wa Jubilee huenda ukafanyika tarehe 2 au 6 Juni .

We Have Options:Mashambulizi dhidi ya DP Ruto yawahamakisha viongozi wa Kalenjin

Rais Uhuru Kenyatta analenga kunadhifisha usimamizi wa mabunge ypote ili kurahisisha utekelezaji wa jenda yake anapokaribia kumaliza muhuma wake mwaka wa 2022 . Ruto na viongozi katika mrengo wake wameshtumiwa kwa kuendeleza siasa za kumrithi rais Uhuru Kenyatta na kuhujumu jitihada za rais kutekeleza ahadi nyingi za maendeleo alizotoa kwa wakenya mwaka wa 2013 na mwaka wa 2017 . Washiali ambayeni  kiranja wa walio wengi bungeni ,naibu wake Cecily Mbarire na mwenyekiti wa kamati ya bajeti Kimani  Ichungwa,  ni miongoni mwa wanaolengwa endapo  Jubilee italenga kuendeleza msururu wa kuwaondoa washirika wa Ruto katika uongozi wa bunge.

Ingawaje jina lake limetajwa kwa wanaoweza kufurushwa kama kiongozi wa wengi bungeni ,Aden Duale amekuwa akituma jumbe za kukinzana wakati mmoja akieleza kwamba yupo nyuma ya rais Kenyatta na haijabainika endapo chuma chake kipo motoni .

 

What? Kikao cha bunge chakatizwa baada ya picha za ngono kuibuka

 

Bunge la kitaifa la Afrika Kusini lilifunga bunge kufuatia mlipuko wa virusi vya corona. Wabunge kwa muda sasa wamekuwa wakifanya vikao vyao kupitia kwa njia ya mtandao wa kijamii.

Kikao ambacho kimekuwa kikifanyika kupitia mtandao wa kijamii wa zoom, kilikatizwa baada ya picha ya ngono kujitokeza kwenye skrini.

Spika Thandi Modise alighadhabishwa na picha hizo huku akisema hiyo ni sababu kuu ambayo humfanya apinge mikutano ya mitandaoni.

Imeripotiwa kuwa, wahandisi wa bunge hilo walilazimika kutumia kiunganishi kingine ambapo wabunge waliungana tena na kuendelea na kikao chao.

Kwa mujibu wa tovuti ya EyeWitness, Wabunge walitaja tukio hilo kuwa la aibu na la kukera sana.

Kwa sasa, bunge la Afrika Kusini limefungwa na vikao vyote vinafanyika kwa njia ya mitandao huku nchi ikiendelea kukabiliana na jinamizi la ugonjwa wa corona.

Zero! Hakuna mbunge aliyepatikana na coronavirus— Muturi

Hakuna mbunge  au mfanyikazi wa bunge aliyepatikana na virusi vya Corona katika vipimo vya hiari vilivyofanywa mapema mwezi huu.

Spika wa bunge Justin Muturi  katika arifa kwa wabunge amesema  matokeo ya waliopimwa kutoka bunge  na seneti pamoja na wafanyikazi  wa mabunge yote yameonyesha kwamba hakuna aliyepatikana na virusi hivyo.

Danganya toto:‘Sikusoma mkataba wa kuhamisha majukumu ya Jiji kwa serikali kuu’-Sonko asema

“  Ningependa kusisitiza kwamba matokeo haya hayafai kutufanya tulegeze kamba kuhusu jitihada za kudumisha usafi  na kuwa na tahadhari  pamoja na kuvalia barakoa  na kuepuka maeneo yaliyo na misongamano.’  Muturi alishauri.

Vipimo vya hiari vya wabunge na wafanyikazi wa bunge vilifanywa kati ya Aprili tarehe 2 na tarehe 4 katika majengo ya bunge.

Bunge liliwataka wajumbe na wafanyikazi kufanyiwa vipimo kwa hiari  kama jitihada za mapema za kukabiliana na ugonjwa huo  baada ya ripoti za magazeti kudai kwamba wabunge 17 wamepatikana na virusi hivyo.

Tuwashtaki wote wanaotoroka maeneo ya karantini-Mutahi Kagwe awaambia wakenya

Muturi amesema  tume ya wafanyikazi wa bunge inandaa  vipimo vinginge kwa wabunge na wafanyikazi wa bunge na wanafaa kuendelea kufuata ushauri na mwongozo unaotolewa na shirika la afya duniani WHO na wizara ya Afya nchini

Mass testing kuanza rasmi wikendi hii-Rais Kenyatta asema

“ Shughuli hiyo itakuwa ya hiari na inawalenga wabunge wote  na wafanyikazi. Wengine watakaopimwa ni wafanyikazi waliopewa kandarasi ya kufanya kazi ya usafi bungeni. ‘ Muturi aliongeza