Mipango ya kando na mishahara: Wanajambo wafichua wanachoficha wapenzi wao

Je ni si siri gani kubwa ambayo umeweka katika mahusiano yako? Hilo ndilo lilikuwa swali kuu au mada katika kipindi cha Bustani la Massawe hapo jana.

Hii ni baada ya Massawe Japanni kugundua kuwa wanandoa wengi humu nchini wameficha mengi katika mahusiano yao, siri ambazo wengi wameapa kupeleka kaburini.

Picha ya siku: Familia ya Lulu Hassan na Rashid yapendeza wengi

Baada ya kuuliza swali hili kupitia mtandao wa Radio Jambo wa Facebook, tulishangazwa na baadhi ya siri ambazo wanajambo wamefichia wapendwa wao.

Baadhi ya siri ambazo wengi walikiri kuficha ni; Mishahara, mipango ya kando na hata hasira kuu. Isitoshe, wengi walikataa kufichia wakidai kuwa siri zao zitasambaratisha ndoa zao.

Soma baadhi ya siri hizo;

Clen Cecilia Prynsillah:  kutotoa uchi wa matatizo zetu ya nyumba nje kwa watu

Jembez Evans: Mpango wa kando

Mukupi Philip: My side plan Yaani Mpango wakandoo🤣🤣🤣🤣🤣

Sifuna Adriano Mumanchester; Kuwa nko na hasira mbaya

Malkia Strikers yafuzu kwa michuano ya Olimpiki baada ya miaka 15

Igz Lum; My salary

Denis Lumumba; Atm

Geoffrey Junior Shikami Torrera;  Wa kangemi bottomline tuko pamoja na Madam redemta baraza

Marius Kipchirchir Kili;  Nikisema haitakua siri tena! Acha ibaki story

Mpenda Amani Alex Mwenyewe: pamoja na Millie Mokeira. Hakuna siri ninayomgifija. Anajua kila kitu kunihusu nami naju. Tunahaminiana

Harrison Juma Mchelsea: Hiyo dadangu huwa hatusemi unless ka ntaka kufariki… Ktl tuko lockd

Hillary Chirchir: Siri ni Siri massawe,ntatoboa aje Siri yangu jameni?

Tendo moja la ndoa lamsababishia virusi vya UKIMWI, Ireri afunguka A-Z

Mwanadada kwa jina la Naomi Ireri, 41, amefungukia Massawe Japanni jinsi tendo la ndoa mara moja lilimpa virusi vya ukimwi.

Akizungumza na kipindi kinachoruka kituo hiki cha Bustani la Massawe, Naomi alishiriki kimapenzi na mwanaume waliojuana kwa kipindi cha wiki mbili.

(+Picha ) Bintiye Akothee, Vesha Okello avujisha picha ya babake

Baada ya mwaka mmoja, Naomi alipata mwanamume mwingine na akazaa naye mtoto bila kujua alikuwa tayari ashapata virusi vya UKIMWI.

“Niligundua nilikuwa na virusi vya ukimwi nikiwa na miezi mitano katika vipimo vya kliniki…

“Nilidhani nilikuwa sawa ila siku moja nikapimwa katika hospitali ya kibinafsi na kuitishwa damu yangu…”

Taarifa za kuugua maradhi ya ukimwi zilimshtua zaidi Naomi,

‘Nilijua tu ni baba mtoto alisababisha, baada ya kumpigia alisema kuwa yeye hakuwa na virusi hivyo na kunituma nikapimwe tena…”
“Sikulala siku hiyo…’ Naomi.
 Asichokifahamu mwanadada huyu ni kuwa aliyemuambukiza ukimwi ni jamaa walifanya mapenzi kabla kupatana na mmewe.
Naomi alikutana na jamaa huyu na kujahamiana naye kabla wiki kumalizika.
Jombi huyu alimpa Kshs, 1000 na hakuwahi kumpigia tena simu.
Alipojaribu kumpigia simu hakushika simu zake.

“Tulifanya sex baada ya kumwambia asimwage ndani.”

Baada ya kufanya mapenzi na jamaa huyu, mawasiliano yalikata ghafla.

“Akanyamza nikaona amenimwagia. Ningejua ni ukimwi ningeenda hospitali nipewe dawa ya kuzuia HIV…” Alisimulia Ireri.

“Nikampigia simu hashiki ,jumbe akawa hajibu na nikaamua kunyamaza nikasahau hiyo story…”

Lebo ya WCB kutumia uganga kuzuia mvua Dar Es Salaam, Babu Tale

Kinachomshangaza Ireri ni kuwa mwanamme waliyezaa naye mtoto hakupatwa na UKIMWI.

Ireri alichukulia hali yake kijasiri na akaamua kusomea elimu ya kilimo.

Kwa sasa, mwanadada huyu ni sauti ya watu wanaoishi na UKIMWI.

“Nilikaa nikaona vile niko bold nijitokeze nikaelewa na nika-jiencourage. Watu watumie condoms…”

Naomi amesema kuwa unaweza ukampigia simu kwa namba 0722384881 au utume arafa [email protected] ili aweze kukuhimiza kuhusu kuishi na virusi vya UKIMWI.

 

Ilikuaje:Teacher Wanjiku aeleza safari yake anapohitimisha miaka 10 ya uigizaji

Mwigizaji Caroline Wanjiku maarufu kama Teacher Wanjiku anasema kuwa anafurahia sana kutimiza ndoto yake anaposherehekea miaka 10 kwenye ulingo wa uigizaji na ujeshi.

Hata ingawa anasema kwamba maisha yake hayajakuwa rahisi, ila kile anachofurahia anapohitimu mwongo moja ni kuwa kielelezo kwa wengi.

Anasema kuwa anafurahia sana kuona kuwa jinsia ya kike imejitoza kwenye sanaa hii ya ucheshi kinyume na vile ilivyokuwa awali.

PICHA: Haya Ndio Maisha Magumu Yanayomngoja Jowie Huko Manyani

Kwa sasa kama kusherehekea ufanisi wake, ameandaa hafla ya kuwapongeza wote waliomshika mkono akiwemo Daniel Ndambuki maarufu kama Churchill.

Kuhusu jinsi anavyozungumza, anasema kwamba amezoea hivyo na imekuwa desturi. Licha ya kwamba ilikuwa ni mtindo wa kuigiza, kwa sasa umekuwa mfumo wake rasmi wa mazungumzo.

Teacher Wanjiku licha ya kuwa alifunga harusi mwaka mmoja uliopita anasema kuwa, ana watoto 3 kwa sasa, kulingana naye alianza Twa twa mapema.

“Niko na watoto wawili wa kike na mmoja wa kiume, nilianza twa twa mapema.” alisema.

Teacher Wanjiku anasema kuwa imekuwa vigumu sana kuwa mtangazaji wa redio na hana azma kwa kuwa kulingana naye”inalemaza ubinifu”.

Ijapokuwa hakujua kilichotokea hadi sasa, kile anachofahamu ni kuwa show yake ilifutiliwa mbali baada ya muda mfupi

“I am a successful comedian, tulianza na brand na sasa imeenea kote dunia, tumefika hadi Marekani na kutuzwa,” alisema.

Teacher Wanjiku ambaye aliolewa na Victor Ber ambaye ni maneja wake, anasema kwamba anafurahia familia yake na ushirikano ambao wamempa.

Na wito wake kwa wanaume ni kuwa wanaowajibika.

“Wanaume mchukue responsibility yenu,” alisema.

Google Yachapisha Orodha Ya Watu Maarufu Waliotafutwa Sana 2019

 

 

 

 

 

‘Jamaa wa bodaboda aliniseti kuwa nahanya,’ Rose asimulia

Je ushawahi kuwa na mpango wa kando? Na je uliwahi patikana, na kama kisanga kama hicho kimewahi kupata nini kilitokea.

Mwanadada kwa jina Rose alisimulia kuwa alikuwa na mpango wa kando kwa mda wa miaka miwili na cha kuchekesha ni kuwa aliyepasua mbarika ni jamaa wa bodaboda.

Kulingana na bi Rose, aliamua kutafuta mpango wa kando pindi tu alipogundua mumewe ana hanya hanya. Lengo lake lilikuwa apate jamaa halafu wakimalizana arudi kwa ndoa yake.

Hata hivyo, uhusiano wao uliendelea na kabla ajue miaka miwili ilikuwa imeisha. Alisimulia kuwa jamaa wa bodaboda ambaye anajua wana ndoa hao wawili ndiye aliyetobolea mumewe siri.

Bustani la Massawe: I have been smashing my boss’ wife for the last 6 years

Soma usimulizi wake,

Nilipatikana live live! Ni mtu wa boda aliniseti na si eti ni ile huwa anaskia, alikuja na akanipata live.

Hata sikutumia bodaboda ni vile ananijua na anajua bwanangu, sasa tulikuja tukaelewana na mambo yako salama sasa kwani pia yeye aliogopa.

Jamaa alianza kuhanya na nikampata si eti niliambiwa akikuja kwa nyumba anapiga mgongo kwa ukuta akilia amechoka. Massawe akaanza kuja na 600 kwa nyumba na ni mtu alikuwa anakuja na 3,000 kwa siku.

Hapo nikaanza kumshuku nikapeleleza polepole nikampata na nikashikana na mjamaa fulani. Huyo jamaa alikuwa serious alikuwa anataka kunioa na mimi ilikuwa tu revenge na nirudi kwa nyumba yangu.

Tulienda enda na yeye karibu miaka miwili na nikapatwa, bwanangu alimuongelesha na akamwambia kuwa mimi ni mke wake na amelipa mahari. Tangia hapo hajawahi taja chochote kuhusiana na hilo baada ya kunisamehe na yeye pia aliwacha kuhanya.

Jambo Massawe: Bwanangu alikuwa ananyemelea auntie yake

 

Kanoga asimulia alivyobakwa na genge la wanaume jijini Nairobi

Willson Kanoga amefunguka mwanzo mwisho jinsi alivyolawitiwa na genge la watoto wanaorandaranda mitaani akiwa na umri wa miaka 7.

Kanoga alikuwa mgeni katika vichochoro vya jiji la Nairobi.

Katika kipindi cha Bustani la Massawe, Wilson amesema alihisi uchungu mwingi sana.

Masaibu ya Babu Owino, ataja sababu za mahasidi kutaka kumtoa uhai

“Unajua ukiwa mgeni katika streets lazima ukaribishwe. Wale wakubwa uwa wanataka kulala na wewe….” Alisimulia Massawe.

Wilson alikuwa anatafuta maisha mtaani baada ya babake kuaga na mama kumtoroka.

Baadaye Jamaa huyu alizamia maisha ya mtaani na kuanza kulewa dawa za kulevya pamoja na kuuza.

“Kuna stages na ambazo unatakiwa kupitia ili ukaribishwe mtaani…”

Njama ya Ruto na TangaTanga ‘kuiteka nyara’ Jubilee kutoka kwa Uhuru Kenyatta

Kanoga amesema kuwa alikuwa analala kwa gunia.

Kanoga amesema kuwa alibakwa mara nne.

Mara ya pili, ya tatu na nne alibakwa akiwa Shimo la Tewa.

Baadaye Kanoga alibadilika na akaacha tabia za kihuni.

 

Nina uhusiano na ma pastor wawili na sponsor – Emily

Kama ilivyo desturi, kipindi ukipendacho cha Massawe Japannni, Bustani la Massawe hukuwacha ukiwa mchangamfu, ukiwa umeelimika na isitoshe ukiwa umetosheleza kiu yako ya mziki na burudani.

Mhubiri James Ng’ang’a aomba Linus Kaika msamaha hadharani

Siku kadhaa zilizopita ilikuwa zamu yake mwanamke mmoja kwa jina Emily, kuwaacha waskizaji vinywa wazi. Hii ni baada yake kusimulia kuwa licha ya kuwa ameolewa, tatizo lake la kutopata mtoto lilimskuma kutafuta uhusiano nje ya ndoa.

Jitihada zake zilimfikisha kwa pastor mmoja ambaye baada ya uhusiano alimpachika mimba.

Isitoshe Emily hakuwachia hapo kwani alishikana na pastor mwingine kama mpango wa kando, kabla ya kuangukia jibaba kama sponsor.

Anasema pastor yule aliyempachika mimba sasa hivi hayuko kwa ndoa yake na alichobakia ni kumuahidi Emily kuwa atamuoa, na sasa anangojea aone jinsi mambo yatakavyokuwa.

PATANISHO: Mume wangu kila mara hutishia kunikata kata

Soma usimulizi wake,

Niliolewa na mume wangu sasa nilikuwa nimetoa mimba na nikakaa bila kupata mimba na akaanza kunisumbua kuwa siwezi pata. Nikaangukia pastor nikalala na pastor akanipa uja uzito.

Sasa hivi nina sponsor na pastor mwingine. Pastor huyu aliwachana na nyumba yake na aliniahidi atanioa lakini tutaona tu.

Say what? Kichwa cha jamaa cha kwama siku tano ngazini

Majonzi yangu yalianza kwa runinga nilipoona bwanagu ameoa mtangazaji Esther Arunga

Alijua kwa vyombo vya habari kwamba bwanake ameoa.

Rose Mueni, alikuwa ameolewa na Quincy Timberlake.

Quincy Timberlake aliweza kuwa kwa vyombo vya habari na tuliweza kumjua baada yake yeye ku kupatana na Esthe rArunga ambaye alikuwa ni mwanahabari na kulikuwa na vituko vingi sana. Ilikuwaje?

Rose Mueni, bibi yake alisimulia

‘Quincy tulipatana mimi nikiwa shule, na yeye alikuwa pale Alliance Francaise, Alikuwa nasomea French, so tulikutana na yangu nasema ilikuwa love at first sight then fromt here tukakuwa na uhusiano. Kisha nikawa mke 1999, though sikufanya harusi ya kanisani, hiyo ilikuwa ikuje later. Then from hapo tukakuwa familia nikapata watoto watatu Quincy, Trevor na Cassidy. Tukaisihi na yeye kwa ndoa miaka kumi.

rosemueni
Rose Mueni and Japanni Massawe

Je majonzi yake yalianza lini?

siku moja nili kuwa kwa nyumba kama kawaida alafu jirani yangu akaja akaniuliza kama kuna news yoyote nimeona, nikamwambia sijaona, nikakuwa curious, nikamuuliza mbona unaniuliza? Akaniambia kuna jambo nimeona lakini sitaki niwe wa kwanza kukuambia, naeza taka uone breaking news at 4. 

So wakati niliona breaking news ilikuwa ni Quicny ameoa Esther.

Doh, aliwezaje kuoa bila Rose Mueni kujua?

‘Alikuwa ametoka ameenda safari kama mda wa wiki moja nikamtayarish akam vila mke hutayarisha bwana, akaenda safari. Ilikuwa safari ya kwenda kazini, ilikuwa aende kukaa kwa wiki moja so baada ya ile wiki moja hakuja ile siku alikuwa namtarajia alikuaj I think foru days later. So after hizo siku nilikuwa namtarajia baadaye mimi niliona kwa runinga akiwa ameoa Esther. Sasa yangu ilikuwa mshangao kwanza sikuamini 

Baada ya kushikwa na butwaa, alifanyaje?

Nilipiga simu but nikapata simu yake ikiwa mteja siku hiyo sp personally huwa nareact pole pole, so baadaye nikafikiria labda nimchezo wa kuigiza na labda alikuwa anataka iwe surprise. Nikangoja akuje labda hii ni soap opera.

Ikawa ni safari ndefu kutoka wakati huo hadi leo ambacho niliogopea 

bwanake alikuja vipi nyumbani, waliongea aje?

Baada ya hiyo harusi alikuja nadhani after wiki moja Alikuja nyumbani kama vile yeye huja tu siku zingine za kawaida akabisha akaketi chini niakmgoja anielezee. Hakunielezea anything yeye alikuja tuu kama the man of the house tukaongea mambo ya nyumbani. So mimi hujiuliza mbona sikureact I never asked that man anything, so 

Ilikuwa inasemekana kwamba aliweza kuwa katika cult na Joseph Helon wakisema kwamba moja wao alikuwa rais. 

‘But hiyo ya cult naweza mtetea, ata kama tumekuwa na differences zetu kwasababu angekuwa kwa cult mambo ya cult ilijitokeza wakati walipoteza mtot wao wakiwa Australia na watu wakaongea sana  ni kwasababu ya cult anaweza kuwa amesacrifice mtoto wake but hapo ninakataa kwasababu ingekuwa yuko kwa cult hawa watoto wangu ndio wangekuwa wa kwana kuptatiwanwa. And then alikuw mtu mcha mungu sana. kwa hiyo siwezi mambo yake ya kuwa kwa cult kwasababu sitaki kumwekelea jambo ambalo sijaliona.

Quincy aliweza kunedelza jukumu lake kama baba?

Alikuwa akija kuona watoto, alikuja kuendeleza jukumu lake kama baba hakutuwacha tuu immediately aliendelea, akaendelea wakati alikata communication alivyo enda Australia tulipoteza mawasiliano kabisa 

Kabla ya kutoka Kenya, Quicny aliniletea katiba nisoma ili niweze kujua kwamba katiba inasema a man is allowed to have more than one wife. Nikama alikuwa ananiambia hajaniwacha hata kama ameoa mke mwingine. So hapo nikasink into depression nikawa sielewi najiuliza maswali so nikawa na mda mgumu sana hapo ndio nilianza my walk with God.

Rose Mueni alisema baada ya kugundua mume wake ameoa na bwanake hakumwambia kwa kumkalisha chini alikuja tuu kwa kubeba katiba akamwambia some hiki kipengee

Also read more here

Askofu Deya stadi wa “kiingeresha” amfunza Massawe!

Mtangazaji Massawe anayefanya kipindi cha Bustani la Massawe katika kitengo cha Ilikuaje huwahoji wageni tofauti tofauti katika studio. Wiki hii akaja Askofu mwenye utata Gilbert Deya ambaye kwa kuwa ameishi Uingereza kwa miaka 15 akawa anajinadi na kujipiga kifua kuhusu uweledi wake wa lugha ya kiingereza.

DEYAPIX

Pata hadithi hapa:

Namzidi mpenzi wangu kwa miaka 50- Askofu Gilbert Deya

Deya ni mhubiri tata aliyewahi kugonga vichwa vya habari kwa umaarufu wa kuwaombea wanawake na baadaye kupokea baraka za watoto almaarufu kama “Miracle babies”. Katika kipindi hiki, Gilbert alitangaza kuwa haoni tatizo Askofu Ng’ang’a kuwatusi na kuwakaripia watumishi wake pale kanisani.

Katika mahojiano yaliyochukua saa moja, Massawe alimuuliza kuhusu tetesi kukua aliwahi kuhamishwa kwa nguvu kutoka nchi ya Uingereza hadi nchini kwa tuhuma za kuiba mtoto. Ikumbukwe kuwa, raia wa nchi tofauti anapohitilafiana na sheria katika nchi nyingine anaweza kufurushwa nchini humo. Tendo kama hilo kwa kiingereza huwa ni “Deportation.” 

gilbert

Soma pia:

Ata kama umeokoka, macho huwa hayaokoki-Askofu Deya

Neno hili kulingana na Deya halikufaa kitendo hicho kilichotekelezwa na serikali ya Uingereza. Kulingana naye, Massawe angefaa kusema “Extradited”. Neno hili la kiingereza likiwa na maana kuwa mshukiwa alitumwa nchi aliyofanya uhalifu akashtakiwe huko ambayo ni Kenya.

“Rumour has it that you were deported, is it true?” aliuliza Massawe.

“No, it’s not Deportation, you don’t know English, jaribu kishwahili… i was extradited…its different from deportation.” alijitetea Deya.

“Now  that you know English than myself, whats the difference?” Aliuliza Massawe.

“Sasa wewe ni Swahili yako unanipinga nayo…Mimi nilikuwa extradited nikuje nianze kesi hapa Kenya. Nikimaliza keshi Nitarudi Uingeresha… Unajua kiswahili ni hatari kwangu kama vile wewe kizungu inakusumbua.”

Soma pia:

‘Wanawake Kenya ni kama njugu’ shouts Pastor Deya on fighting temptations

Baadhi ya maneno Massawe huyatumia hewani na maana yake

Utangazaji wa redio ni mojawapo ya sanaa duniani zinazohitaji ubunifu mkubwa na ukakamavu wa kuwashika na kuwagandisha wasikilizaji katika spika za redio zao.

Sanaa yoyote lazima msanii achombeze maneno matamu yanayofanya kazi yake ionekane bora na ya kuvutia zaidi.

Soma hapa:

Massawe afunguka kuhusu ajali – Jumatano

Mwimbaji wa nyimbo za mapenzi atapenda sana kuchonga mistari inayokwenda freshi na maudhui na lengo anayokusudia kwa mashabiki wa jinsia tofauti. Hali kadhalika anapofanya maonyesho jukwaani atakuwa na baadhi ya maneno kinywani ambayo wafuasi wake humtambua nayo.

Mtangazaji Massawe hajaachwa nyuma katika mtindo huu na kuna baadhi ya maneno anayoyatumia katika kipindi chake cha Bustani la massawe ili kuvutia mashabiki.

Pata uhondo hapa:

Sababu Massawe Japanni hatokuwa hewani kwa mda

Tumekusogezea hapa baadhi ya tungo virai (phrases) anazopenda kutumia:

  1. “Nafurahi kuwa tupo pamoja nawe”

Baada ya nyimbo inayocheza hewani kumalizika, mtangazaji huyu anapenda sana kuanza na maneno haya kama kitambulisho cha kufungua shoo.

     2. “Ngwenee”

Hili ni tamko ambalo lina asili ya lugha ya Kikamba na huwa na maana ya ‘Nakuona’. Kwa haraka haraka unaweza toa ubashiri wako na kusema kuwa Massawe husema hivi labda kwa sababu anatoka maeneo ya ukambani au labda ni mbinu ya kugeuza ndimi na kuwavuta wasikilizaji kutoka jamii hiyo.

    3 .” Uko hii town? Au niko hii town au labda hii ni town”

Massawe hutumia maneno haya mara kwa mara. Staa huyu huwa anataka kujua mashabiki wake wanategea kipindi wakiwa maeneo gani.

 

Soma pia:

‘Safiri salama dadangu’ Massawe Japanni mourns her best friend

Massawe afunguka kuhusu ajali – Jumatano

Mtangazaji wa kipindi cha majira ya mchana – Bustani la Massawe  na kinachopeperushwa kuanzia saa nne hadi saa nane alasiri katika mawimbikasi ya Redio Jambo amechapisha ujumbe  kwa mashabiki wake katika mtandao  maridhawa wa Instagram.

Staa huyu amezamia insta story yake na kutoa ushauri wake kwa mashabiki wake kuwa wakae ange muda wowote wanaposafiri.

“Siku iliyoje! Ndo nafika chumbani baada ya kuhusika katika ajali ndogo ! Mafunzo nimeyasoma muda wowote chochote kinaweza kufanyika. Funga mkanda wa usalama kila wakati.”

 

 

massawe

Tumekusogezea hapa:

Massawe Japanni anusurika baada ya kuhusika katika ajali mbaya (PICHA)

Mtangazaji Massawe alipigwa na butwaa na kuingiwa na kibuhuti baada ya tukio la jana. Wasikilizaji walimkosa Jumatano ila leo (Alhamisi) yupo yupo kuwakonga nafsi wasikilizaji wake.

Zamia uhondo hapa:

Sababu Massawe Japanni hatokuwa hewani kwa mda

Kipindi chake huangazia sana matatizo yanakumba familia katika jamii hususan wanaume wanaopachika mabinti mimba na kuwazimia data ghafla. Massawe huwapigia simu na kuwasaidia kwa kuwaelekeza katika kituo cha kusaidia kina mama.

Jilie utamu hapa:

Video of the day: Massawe Japanni’s dancing skills are top notch!