Pigo kubwa kwa Mungatana baada ya uamuzi mpya wa korti

Aliyekuwa Mbunge wa Garsen Danson Mungatana na mwanabiashara mwenzake Collins Waweru wameshtakiwa kwa udanganyifu, wakili wa wawili hao alisihi mahakama kuacha mashtaka hayo na kisha kuzungumza na mlalamishi nje ya mahakama.

Hata hivyo mashtaka yalikataa huku yakisema kuwa makosa ya wawili hao yalikuwa ya jinai.

“Wizara ya ulinzi inahusika kama mlalamikaji, kwa vile wanataka kupatanisha na mlalamikaji mashtaka mengi ni ya serikali.”

Jumatano Mungatana alishtakiwa kwa udanganyifu katika mahakama ya Kibra baada ya ombi lake kutupiliwa mbali la kuskizana na mlalamikashi nje ya korti.

Kulingana na jaji Abdul Lorot ombi lake lilikosa ustahimilifu hivyo basi alibidi kutupilia mbali.

“Walikuwa na makubaliano yao lakini wameshtakiwa kwa maana mashtaka yameafikiana na kizingiti cha maslahi ya umma.” Alisema.

Mungatana na mwenzake waliachiliwa kwa dhamana ya shillingi 200,000 baada ya kukana mashataka hayo, huku wakishtakiwa kwa udanganyifu wa hati na hata kupokea pesa kwa kujifanya.


PATANISHO: Mjomba wangu alinipiga kwa chuma kichwani

Collins, 23, kutoka Narok ndiye aliyeomba kupatanishwa na mjombake, bwana Peter, 47, akidai kuwa wawili hao walikosana na hadi akapigwa chuma cha kichwa na kumlaani. Aliongeza kuwa mjombake ndiye mzazi wake na sahii anasononeka na anafikiri kujitoa uhai.

“Nilikuwa na mwanadada mpenzi wangu nikiwa naishi kwa yule mjomba, niliondoka na kwenda Nairobi kutafuta kazi ila sikupata na nikateseka. Nilikuwa nimefungua kinyozi na mjomba wangu wakapangana na mwanadada wakauza zile mashini na akaenda kwao.” Alielezea.

PATANISHO: Mume wangu aliniambia nitaendea kifo krisimasi

Collins anadai mjomba hakuuza mashini zote ila alipoenda kuidai wakaanza vita na kwa mwaka mzima hajasafiri hadi nyumbani. Juzi alitishiwa kuwa asiwahi fika kwa shamba la ukoo wao.

Ni mchungaji pia na ndiye amekuwa akinilea kwa mambo ya kiroho.” Aliongeza.

Alipopigiwa simu bwana Peter alisema kuwa alimlea Collins maisha yake na kijana amekuwa akimkosea na kumtumia arafa za matusi.

“Najua ni mtoto mdogo na sote tunahitaji msaada kutoka kila mmoja, juzi alikuja nyumbani akitaka kunichapa na hata kama nilikosea angekuja tuzungumze vyema, hadi nikaapa kuwa hatakanyanga hapa.” Alieleza bwana Peter.

PATANISHO: Nashuku boss wangu mwanajeshi ana uhusiano na mke wangu

Akijitetea, Collins alisema kuwa chanzo chake cha kumtumia ujumbe ni kuwa mjombake alikuwa amesema kuwa asiwahi patikana kwa shamba la nyanya. Hapo akaamua kumpigia simu na kumueleza kuwa angemwambia yeye mwenyewe.

Nilipofika kule kwa mjomba alikuwa amebeba panga na kama sio ndugu angeniua na isitoshe alitoa chuma kotini mwake na ikaniumiza hadi nikkashonwa hospitalini.”

Mjombake alimaliza akisema kuwa arafa hizo zote ziko kwa polisi kwani alihatarisha maisha yake kwa njia kubwa. Alisema amemsamehe lakini aite jamii ili aombe msamaha na aape kuwa hatorudia tena.

 

Sema Na Raey: Wanaume Wawili Wapigania Mwanadada Hewani

 

Hivi majuzi kulikuwa na kizazaa katika kipindi cha ‘Sema Na Raey’.

sema na raey: Men reveal they beat up their wives to ‘get them in line’

Jamaa mmoja kwa jina Ken alidai kuwa anamshuku mkewe wa miaka mitano kuwa ana uhusiano na jamaa kwa jina Collins, akidai kuwa anashuku uhusiano huo umekuwa ukiendelea kwa miaka miwili sasa.

Wawili hao walianza kujibizana huku Collins akikubali makosa yake lakini bwana Ken bado akishuku kuwa bado uhusiano huo unaendelea.

Pata uhondo kamili.

Sema Na Raey: Nilifukuzwa na bibi yangu wa miaka ishirini

PATANISHO: Nalaumu Bangi Kwa Kunikosanisha Na Mke Wangu

Wanaume kwa wake, wengi hulimbikizia lawama chochote kilichokaribu nao ili kujikwamua kutoka kwa hukumu yoyote ile, iwe ni kazini au pia kwenye ndoa.

Mojawapo ya mengi yanayolengwa nyakati nyingi ni dawa ya kulevya aina ya bangi ambayo imekuwa chanzo cha madhara mengi katika jamii. Basi tukio hili lilitokea hapo jana katika kitengo cha Patanisho wakti bwana Collins alipolaumu bangi kwa kumkosanisha kati yake na mkewe.

Bwana Collins mwenye umri wa miaka 25, aliomba apatanishwe na mkewe Lydiah 23, baada ya wapendwa hao wawili kukosana mwaka uliopita, kisa na maana Collins alikuwa na tabia ya kumpiga mkewe kila alipovuta bangi.

“Nilikuwa natumia bangi, katika harakati ya kuivuta jioni na marafiki, kufika kwa nyumba yangu ile bangi ilikuwa inanionesha sitaki kuona mwanamke yeyote karibu nami, hadi nikimuona mke wangu namtafutia makosa ili nimpige na hapo ndipo mke wangu hutoweka kwa masaa matatu. Bangi ikishuka kiasi nashtuka baada ya kugundia nilichokifanya na hapo ndipo namtafuta na baada ya tukio kadhaa mke wangu akadai amechoshwa na tabia zangu akidai napenda raha. Kurudi nyumbani baada ya siku kadhaa nikapata mke ameenda na akabeba vitu kadhaa na kumtafuta akawa mkali zaidi. Tumeishi kwa miaka miwili na aliingia kwa ndoa na mtoto mmoja.”

Alisema bwana Collins huku akifichua amevuta bangi kwa miaka kumi kwani alianza tabia ile akiwa shuleni huku akikiri kuwa amewacha bangi na sasa ana miezi mitatu tangia aitumie.

Pata uhondo kamili.