covid-19:Watu 105 wapatikana na corona huku kukiwa hamna visa vya vifo

Kenya hii leo imesajili visa 105 vipya vya maambukizi ya corona na kufikisha idadi jumla ya 36,829  vya watu walioambukizwa corona hii ni kutokana na sampuli 2,868 zilizopimwa ndani ya saa 24.

Huyu haya yakijiri waziri wa wizara ya afya Mutahi Kagwe ametangaza kuwa kati ya maambukizi hayo mapya 83 ni wanaume huku 22 wakiwa na wanawake.

Pia mgonjwa mwenye umri wa chini ana miaka miwili huku mwenye umri wa juu akiwa na miaka 95.

Hii leo watu68 wamepona kutookana na virusi vya corona na kufikisha idadi jumla ya 23,777 waliopona kutokana na corona huku 38 wakiwa wamepona wakipokea matibabu ya nyumbani na 30 wakiruhusiwa kuenda nyumbani kutoka hospotali tofauti.

Msemaji wa serikali Cyrus Oguna aeleza jinsi alipigania maisha yake kutokana na corona

Wiki chache baada ya msemaji wa serikali Cyrus Oguna kupatikana na maambukizi ya corona na kisha kulazwa hospitali kwa matibabu hatimaye ameeleza jiinsi alipigana na virusi hivyo alipokuwa hospitali.

Kupitia kwenye mitandao yake ya kijamii, Oguna alisema kwamba wakati ambao alilazwa alikuwa na uchungu mwingi kwenye kifua chake ambao ulisababisha awe na shida ya kupumua.

Oguna alisema kuwa alipigana na shida ya kupumua usiku mzima hadi pale madaktari walikuja kesho yake kuanzisha matibabu yake.

“Kwa ugumu mkubwa singefanya chochoye yaani singepumua uchunguzi wa X-ray ulifanywa lakini mita chache kuenda kwa x-ray ilikuwa ndoto mbaya sana

ata nikiwa kwenye oksijeni ilikuwa ngumu kupumua hata kusonga ilikuwa uchungu sana si kwa kifua tu mbali kila sehemu ya mwili ilikuwa uchungu

vitu vidogo kama kugeuka kitandani halikuwa jambo rahisi hamu ya chakula niliokuwa nimebaki nayo iliisha kabisa.” Oguna Aliandika.

Baada ya siku chache Oguna hakuonyesha mabadiliko yeyote katika hali yake ya afya ambapo iliwabidi madaktari kupandisha spidi ya oksejeni yake.

“Sikufahamu kitu chochote kwenye wadi yangu hata kazi ya madaktari waliokuwa wanafanya, kila mmoja akija na kunipa dawa tofauti

nakuangalia kilichokuwa kinatendeka kwenye mashine yangu Akilini mwangu nilijua tu mambo hayako sawa lakini nilijiambia kuwa napaswa kuwa na nguvu.”

Wakati huo msemaji huyo alisema kuwa alikuwa anasikia sauti kwenye akili yake zilizomshangaza kama alikuwa hai ama amefariki.

Kulingana naye hakuwa anazungumza sana hata kumaliza sentensi moja.

Covid-19: Visa 148 vipya vya corona vyarekodiwa huku watu 4 wakiaga dunia

Watu 148 wamepatikana na virusi vya corona na kufikisha jumla idadi ya 36,724, hii ni kutokana na sampuli 2,438 zilizopimwa ndani ya saa 24 zilizopita.

Waziri wa wizara ya afya Mutahi Kagwe pia amesema kati ya maambukizi hayo mapya 105 ni wanaume na 43 ni wanawake,mgonjwa mwenye umri wa chini ana miaka miwiii ilhali mwenye umri wa juu ana miaka 75.

Huku hayo yakijiri, watu 98 wamepona kutokana na virusi hivyo, na kufikisha idadi jumla ya 23,709 watu waliopona.

pia hii leo watu,4,wamepoteza maisha yao kutokana na virusi hivyo na kufikisha jumla idadi ya 646

Covid-19:Watu 183 wapatikana na corona huku idadi ikifika 36,576

Kenya hii leo imesajili visa 183 mpya vya maambukizi ya corona na kufikisha idadi ya 36,576 watu walioambukizwa corona hii ni kutokana na sampuli 4,188 zilizopimwa ndani ya saa 24 zilizopita.

Katibu msimamizi wa wizara ya afya Mercy Mwangangi amesema ya kwamba Watu 5 wameaga dunia kufuatia kutokana na virusi vya corona na idadi ya jumla ya waliofariki kufikia watu 642. 82 wamepona na wote waliopona ugonjwa huo wamefika watu 23,611.

Pia amesema kuwa wahidumu wa afya 945 wameeta maambukizi ya corona huku 16 wakipoteza maisha yao tangu maambukizi ya corona yaanze kurekodiwa nchini.

Covid-19: Visa vya maambukizi ya corona vyafika 36,393 baada ya watu 92 kupatikana na corona

Kenya hii leo imesajili visa 92 vya maambukizi ya corona na kufikisha idadi ya 36,393 kutokana na sampuli 2,985 zilizopimwa kati ya saa 24 zilizopita, amesema katibu msimamizi wa wizara ya afya  Mercy Mwangangi.

Mgonjwa wa umri wa chini ana miaka 2 huku mwenye umri wa juu akiwa na miaka 75, kutokana na maambukizi hayo mapya, 64 ni wanaume na 28 wakiwa wanawake.

Covid-19: Watu 10 waaga dunia huku 96 wakipatikana na corona

Pia kati ya maambukizi hayo wote ni wakenya ilhali wanne ni raia wa kigeni.

Huku hayo yakijiri, watu 165 wamepona kutokana na maambukizi hayo, huku 105 wakipona baada ya kupokea matibabu hospitalini na 60 katika mpango wa utunzi na matibabu ya nyumbani.

covid-19: Watu 176 wamepona corona huku 48 wakipatikana na virusi hivyo

Hii leo watu 3 wamepoteza maisha yao na kufikisha idadi jumla ya 637 ya watu walioaga dunia kutokana na virusi hivyo

Covid-19: Watu 10 waaga dunia huku 96 wakipatikana na corona

Hii leo watu,10 wameaga dunia na kufikisha jumla iai ya 634 ya watu walioaga kutokana na virusi hivyo, wakati huohuo watu 96 wamepatikana na virusi vya corona na kufikisha jumla idadi ya 36,301 kati ya sampuli 3270 zilizopimwa kwa saa 24 zilizopita.

Mgonjwa wa umri wa chini ana mwaka mmoja huku mwenye umri wa juu ana miaka 81, 70 ni wanaume huku 26 wakiwa wanawake.

Vile vile watu 121 wamepona na kufikisha jumla idadi ya 23,364 ya watu waliopona kutokana na virusi hivyo.

covid-19: Watu 176 wamepona corona huku 48 wakipatikana na virusi hivyo

Watu 48 wamepatikana na virusi vya corona na kufukisha jumla idadi ya 36,205 hii ni kutokana na sampuli 1,081 qmbqzo zimepimwa kati ya saa 24 zilizopita amesema katibu msimamizi wa wizara ya afya Mercy Mwangangi.

Vilevile watu 176 wamepona kutokana na virusi hivyo na kufikisha jumla idadi ya 23,243 kufikia sasa, pia watu 2, wamefariki kutokana na virusi vya cororna na kufikisha jumla idadi ya 624.

Corona: Kenya yaandikisha visa 188 vipya huku idadi ikifikia 36,157

Kati ya maambukizi hayo mapya  31 ni wanaume na 17 ni wanawake huku mgonjwa wa umri wa chini ana miaka kumi na mbili na mwenye umri wa juu ana miaka 76.

Huku akitangaza maambukizi ya virusi hivyo Mwangangi alisema kuwa wananchi wanahitaji kufuata kanuni za kuthibithi kusambaa kwa maambukizi ya corona.

Jinsi ya kukabiliana na mtoto wako endapo watarudi shuleni

Siku chache baada ya virusi vya corona kutibitishwa kukita humu nchini shule, makanisa na hata watu walianza kufanya kazi wakiwa nyumba huku rais akiagiza kufungwa kwa maeneo hayo.

Si mmoja au wawili wanafunzi wengi walikatizwa tamaa na virusi hivyo kwa kusalia nyumbani huku wengi wakisahau umuhimu wa elimu na masomo yao katika maisha yao.

Haya basi huku wengi wakitaka shule kufunguliwa na wanafnzi kurudi shuleni,si wote wamo tayari kurudi kwa maana akili zao zishaasahau masomo.

Kama mzazi hizi hapa mbinu za kukabiliana na mtoto wako endapo watarudi shuleni hivi karibuni au mwaka ujao huku tukingoja waziri wa elimu George Magoha kutoa uamuzi wake hii leo.

1.Msikize mwanao

Wakati huu wazazi wengine wanapaswa kuwasikiza watoto wao ambacho wanahitaji na shida ambazo wamepitia kama wanafunzi na haswa kama yuko tayari kurudi shuleni.

Wazazi wanapaswa kutafuta wakati na kuketi na watoto wao na kisha kuwatayarisha kimawazo kuwa wanarudi shuleni na vile wanapaswa kufanya wakiwa na walimu wao.

2.Tambua vichocheo

Kama mzaziunapaswa kufahamu nini kinamfanya mwanao hasirudi shuleni na kutaka kukaa nyumbani haswa nini hicho kinachochea hali hiyo ya kutisha.

3.Msaidie mtoto wako kupumzika

Kwa maana wamekaa nyumbani sana bila ya wengi kushika vitabu wala kupitia vitabu vyao msaidia mwanao kupumzika na kutulia endapo atasikia shule zitafunguliwa.

Wengi hushikwa na kiwewe na hata kusikia kuna msukumo usio wa kawaida katika maishani mwao.

4.Zungumza na mtoto wako na kumueleza hali jinsi ilivyo

Kama mzazi unapaswa kumueleza mtoto wako hali jinsi ilivyo na kumueleza umuhimu wa masomo katika karne hii ya sasa.

Mpe mawaidha mema na kutuliza akili yake, na kisha aweze kutilia maanani elimu na masomo yake.

Asilimia kubwa ya wanafunzi hasa wa darasa la nane na kidato cha nne waliathrika pakubwa kwa maana walikuwa tayari kukabiliana na mtihani wao wa mwisho wa mwaka.

Covid-19:Watu 179 wamepatikana na virusi vya corona

Kenya imesajili visa 179 vipya vya maambukizi ya virusi vya corona na kufikisha idadi  jumla ya 34,884 hii ni kutokana na sampuli 4178 zilizopimwa saa 24 zilizopita.

Katibu mratibu wa wizara ya afya Rashid Aman amesema kuwa  wananchi wasilege kamba ya kuzuia maambukizi ya corona alizungumza haya akiwa katika kaunti ya Bomet.

Covid-19: Visa 212 vipya vya maambukizi ya corona vyarekodiwa nchini

Vile vile watu 4 wamepoteza maisha yao na kufikisha idadi ya 589 ya watu wakioaga kutokana na virusi hivyo amesema Rashid Aman.

Pia watu 415 wamepona na kufikisha idadi jumla ya 21,059 waliopona kutokana na virusi vya corona.

Covid-19: Visa 212 vipya vya maambukizi ya corona vyarekodiwa nchini

Watu 212 wamepatikana na virusi vya corona na kufikisha idadi ya jumla ya 34,705, hii ni kutokana na sampuli 3,937 zilizopimwa kwa saa 24 zilizopita.

Katibu msimamizi wa wizara ya afya daktari Rashid Aman amesema kuwa wagonjwa 132 walikuwa wanaume huku 80 wakiwa wanawake, mgonjwa wa umri wa chini ana mwezi mmoja na mwenye umri wa juu ana miaka 76.

Huku haya yakijiri watu 195 wameruhusiwa kwenda nyumbani baada ya kupona virusi hivyo na kufikisha idadi ya jumla ya 20,644.

Kaunti ya Nairobi inazidi kuongoza katika maambukizi ya virusi hivyo, pia hii leo watu 4 wamefariki kutokana na virusi hivyo na kufikisha idadi ya 585 ya watu walioaga kutokana na virusi hivyo.