Tuju aitisha mkutano wa MCA’s wa Jubilee kabla ya uchaguzi wa spika kesho

Chama cha Jubilee kimeitisha mkutano wa wawakilishi wake wa kaunti 66 kwa mkutano wa dharura leo utakaofanyika makao makuu ya chama hicho pangani.

‘Si uchawi, ni maombi.’ Sonko asema kuhusu kujiuzulu kwa Elachi

Mkutano huo unafanyika siku moja kabla ya wawakilishi wa kaunti ya jiji kufanya uchaguzi wa kumteua spika mpya baada ya Beatrice Elachi kujizulu siku ya Jumanne.

Katika barua kwa kiranja wa wengi katika bunge hilo, katibu mkuu Raphael Tuju amemtaka  Paul Kados kuhakikisha kwamba viongozi wote wa chama hicho wanahudhuria mkutano wa leo.

Spika wa bunge la kaunti ya Nairobi Beatrice Elachi ajiuzulu

Wakati huo huo  wawakilishi wanane wa Jubilee  watafika mbele ya kamati ya nidhamu inayoongozwa na  Tuju kabla ya mkutano wa leo kuanza. Siku ya Jumanne  mwenyekiti wa kitaifa wa Jubilee Nelson Dzuya na wawakilishi hao walitakiwa kufika mbele ya kamati hiyo ya nidhamu saa nne asubuhi.

Waliotakiwa kufika mbele ya kamati hiyo ni  pamoja na; John Kamangu Nyumu (Ruai), Millicent Mugambi (Ziwani) Jeremiah Karani (Kayole Central Ward) na Charles Thuo (Dandora Three MCA) wengine ni  June Ndegwa, Joyce Kamau, Susan Makungu na  Margaret Mbote.

  

Kalonzo atamatisha mkataba na Nasa, ajiunga rasmi na Jubilee

Kiongozi wa chama cha Wiper Kalonzo Musyoka  ametangaza mipango ya kujiondoa rasmi kutoka muungano wa NASA unaoongozwa na Raila Odinga ili kujiunga na  Jubilee.

Ngilu:Kalonzo hawezi kuaminika kuwatetea Wakamba

Kamati ya usimamizi wa chama cha Wiper  ilikutana kupitia njia ya mtandao na kupitisha uamuzi wa  kujiunga katika muungano na chama cha Jubilee kinachoongzowa na rais Uhuru Kenyatta.

Hatua hiyo sasa inamaanisha kwamba  Wiper sasa itaondoka kutoka muungano huo wa upinzani kwani sheria  hairuhusu chama kimoja kuwa katika zaidi ya muungano mmoja.

Je, Mudavadi anajua anataka nini? Hofu ya kujipata katika njia panda yazuka kabla ya uchaguzi wa 2022

Chama cha Kalonzo pia kitalazimika kumuandikia msajili wa vyama Anne Nderitu kumfahamisha rasmi kuhusu uamuzi wa kujiondoa kutoka NASA na kujiunga na muungano mpya.

Ili muungano wa NASA kuvunjiliwa mbali kabisa vyama tanzu  vitatu vinafaa kuondoka  lakini kwa sasa ODM, ANC na Ford Kenya bado vipo katika muungano huo.

 

Ngilu:Kalonzo hawezi kuaminika kuwatetea Wakamba

Siasa za Ukambani zinakaribia kugeuka kipute kikali cha ubabbe kati ya gavana wa Kitui Charity Ngilu na kiongozi wa Wiper Kalonzo  Musyoka uchaguzi wa 2022 unapokaribia .

Je, Mudavadi anajua anataka nini? Hofu ya kujipata katika njia panda yazuka kabla ya uchaguzi wa 2022

Kuna kambi mbili  ambazo zinataka kuwa na ushawish na kuamua mwelekeo wa jamii hiyo kisiasa na kumpiga konde  Kalonzo anayechukuliwa kama kiongozi wa jamii hiyo kisiasa .Kambi hizo ni  moja inayoongozwa na magavana   Charity Ngilu, Kivutha Kibwana wa makueni na Alfred Mutua wa  Machakos. Kambi nyingine inaongoza na aliyekeuwa  seneta wa Machakos Johnstone Muthama ambao inamwunga mkono naibu wa rais William Ruto .

Charity Ngilu
Charity Ngilu

Uhasama huo wa kisiasa kati ya Ngilu na Klalonzo umejitokeza katika kanda ya sauti iliyotolewa kati ya Ngilu na mbunge wa zamani wa Kibwezi  Kalembe  Ndile . katika sauti hiyo  Ngilu anamshtumu Kalonzo kwa kuwa mbinafasi kwani kila kizuri anakivutia kwake bila kujali maslahi ya jamii yao, na hivyo basi hawezi kutegemewa kujadili hatma ya kisiasa ya Ukamban na kutetea maslahi ya watu wa eneo hilo .

“Kalonzo  hawezi kufanya mazungumzo ya kisiasa kwa niaba ya jamii .endapo atapewa fursa hiyo ,tutakwisha’  amesema Ngilu katika kanda hiyo iliyovuja .

Kalonzo  alimteua mwanawe kujiunga na bunge la EALA na kumuacha  Temi Mutia ambaye alikuwa amekisaidia sana chama cha wiper .Baadaye ilimlazimu Ngilu Kumpa kazi  Mutia kama mshauri katika serikali yake .

Mshauri huyo alikuwa miongoni mwa waliozingatia kwa nafasi hiyo ya Eala  lakini Musyoka alimuacha na kumpa mwanawe Kennedy Kalonzo nafasi hiyo .

Hii Itaweza? Ruto aunda mkakati wa 2022 ili kuzichukua ngome za Uhuru, Raila

Wakati palipotokea mazungumzo kuhusu uwezekano wa rais Uhuru Kenyatta kuwajumuisha  watu kutoka upinznai katika baraza la mawaziri na kila chama kutakiwa kumpendekezamtu wa kujiunga na serikali ,Kalonzo alidaiwa kupendekeza jina lake .

Katika kanda hiyo  Ngilu alipuuzilia mbali azma ya Kalonzo kugombea urais akisema kwamba amekuwa akibadili msimamo wake wa kisiasa kila mara . Amesema kwamba makubaliano kati ya Wiper na Jubilee yaayoonyesha jinsi Kalonzo hawezi kutegemewa .

“ Tunafaa kujitaarisha kuunda muungano thabiti ili kutetea  maslai ya jamii  kwa sababu hatuwezi kumuamini Kalonzo … kundi hilo linafaa kuwajumuisha magavana watatu na viongozi wote ambao hawamo katika  mrengo wa Ruto  ili tuwe katika upande ulio salama’

Kalembe  katika mazungumzo hayo anamshauri Ngilu kuitisha mkutano Stone Athi  ambao pia unafaa kumjumuisha gavana wa Nairobi Mike Sonko

Ngilu pia ameashiria kwamba huenda  asitetee kiti chake cha ugavana na analenga kujinyakulia kiti kikubwa katika mchakato wa BBI ambacho kitatengewa wanawake .

Ngilu ni miongoni mwa magavana wanaounga mkono vikali mchakato wa BBI  na alikuwa miongoni mwa magavana waliokuwa wenyeji wa kampeini za BBI abla ya janga la corona .

Lakini kalonzo kupitia msemaji wake Dennis Kavisu amesema njama za Ngilu sio mpya  kwani amekuwa akifanya shughuli hizo za hujuma kwa muda mrefu .

Ndoto za Abunuasi! Gavana Mutua asema atawania kiti cha Urais mwaka 2022

Kavisu  ametaja miradi kadhaa anayodai ilianzishwa na kufanikishwa na Kalonzo ikiwemo barabara ya   Kibwezi–Kitui-Mwingi  ambayo anasema Klaonzo alijadili ufadhili wake kabla ya kuondoka afini kama makamu wa rais mwaka wa 2012.

Amevitaja vyuo vikuu vya Machakos na  South Eastern Kenya University (SEKU) s kama miradi iliyofanikishwa wakaliz Kalonzo alipokuwa waziri wa Elimu .

stephen kalonzo na rais Uhuru
stephen kalonzo na rais Uhuru

Muthama,  kwa upande wake ameliambia gazeti la The Star kwamba  Kalonzo na Ngilu wamekuwa na tofauti za tangu jadi .Seneta huyo wa zamani wa Machakos amechekelea kwa bezo mwafaka wa ushirikiano kati ya  Kalonzo na Uhuru akisema hautabadilisha chochote .

“ Anafikiria  [Kalonzo] Uhuru  atamuachia kiti hicho. Hakuna uongozi wa kurithi Kenya  ,wakenya wataamua mkondo wanaotaka wenyewe’ Muthama amesema

Ameongeza  kwama Ngilu hunda anatuia njama yake dhidi ya kalonzo ili kusalia uongozinikwa kumkaribia Kiongozi wa ODM Raila Odinga  kwa sababu anafahamu kwamba hali imekuwa moto Kitui .

muthama

“Ngilu anatafuta njia za kumkaribia Raila ili aweze kupata nafasi ya uongozi’

Muthama  amesema atamuunga mkono DP Ruto na watamfuata endapo atasalia Jubilee au ataondoka ili kuanzisha chama kingine .

Mwanasiasa huyo amesema hakuna anayeweza kutetea maslahi ya Ukambani kati ya Kalonzo na Ngilu

“Ngilu  hawezi kuongoza muungano thabiti .Mtu anayeweza kufanya hivyo kuiongoza Ukambani ni Kivutha’ amesema

Kivutha ametangaza kwamba atawania urais mwaka wa 2022  hatua inayomuweka katika nafasi nzuri ya kuanza kujadiliana na wengine kuhusu uwezekano wa kuunda muungano wa kisiasa .

 

 

Chama cha Jubilee hakina pesa ripoti ya mkaguzi yafichua

Ripoti ya mkaguzi mkuu imefichua hali ya kifedha ya chama cha jubilee, huku ikionyesha kuwa chama hicho hakina fedha zozote huku wakisalia kuwa na deni kubwa.

Awali chama hicho kiliripotiwa kutegemea wasamaria wema na waliokopa pesa waweze kurudisha huku deni lao likizidi millioni 66.

Ripoti hiyo ilifichua katika ukaguzi wa kifedha wa mwaka wa 2017-2018, ripoti hiyo ilisoma kama vile ifuatavyo;

“The statement of financial position as at June 30, 2018, reflects current liabilities balance of Sh133,558,229 which exceeds current assets of Sh67,278,244 by Sh66,279,985 implying that the party was operating with a negative working capital, thus technically bankrupt

In the circumstances, the continued existence of the party is dependent on continued financial support from creditors, bankers and well-wishers.” Ripoti ilisoma.

Ripoti hiyo ya kifedha imekuwa kikwazo kati ya katibu mkuu wa chama cha Jubilee Raphael Tuju na naibu wake Caleb Kositany.

Awali Tuju alimpa jibu Caleb kwa kutaka hati ya kifedha za chama hicho.

Mgogoro: Mabilioni ya Chama cha Jubilee yazua mgawanyiko zaidi katika ‘talaka’ ya Uhuruto

Makabiliano kati ya kambi za  rais Uhuru Kenyatta na naibu wake William Ruto sasa yameelekea katika mfuko wa fedha za chama hicho huku upande wa Ruto ukiushtumu mrengo wa rais Kenyatta  kwa utumizi  mbaya wa fedha na hata ufisadi.

UHURU

Katika kinachonekana kama kudorora zaidi kwa uhusiano kati ya viongozi hao wawili , washirika wa Ruto wanaoshikilia nafasi za uongozi chamani, wanasema chama hicho kilitoa zaidi ya shilingi milioni 183  mwaka wa 2018 ambazo matumizi yake hayajaelezwa ifaavyo.

Naibu katibu mkuu wa chama Caleb  Kisitany ambaye ni mshirika wa Ruto ametaka kupewa stakabadhi za keleza jinsi mamilioni hayo yalivyotumiwa  lakini katibu mkuu Raphael Tuju amempepezea chini akisema  matakwa yake hayo ni sarakasi tu za kisiasa kwa sababu hana uwezo au mamlaka ya kutaka kuchunguza  madai hayo.

Kimya kimya: Raila arejea nchini kutoka Dubai baada ya matibabu

Kositany anataka kupewa stakabadhi mbalimbali zikiwemo taarifa za benki za  akaunti za pesa za Chama cha Jubilee kwa muda wa miaka  4 iliyopita. Yadaiwa Kositany ni miongoni mwa washirika wa Ruto watakaopigwa shoka kutoka nafasi za uongozi katika chama cha Jubilee.

Kositany ameshangaa mbona chama hicho kinalipa kodi ya jengo zima la makao makuu ya Jubilee ilhali hakitumii jengo zima na pia kuhoji kutolewa kwa mamilioni  ya pesa kulipa kodi za matawi ya chama ilhali hayajakuwa yakiendelea na oparesheni  zozote.

Wawakilishi wa kaunti wa  Chama cha Jubile  wamekuwa wakitoa shilingi 5000 kila mwezi, wabunge elfu 20  na magavana shilingi elfu 50 kila mwezi kwa chama hicho kwa miaka saba iliyopita.

Maambukizi ya corona yafika 10,105 huku wakenya wengi wakianza kupuuza maagizo ya kuzuia ugonjwa huo

Chama hicho kina  wabunge 171  katika mabunge yote mawili hatua inayomaanisha kwamba wamekuwa wakikusanya  shilingi milioni 3.4 kila mwezi. Magavana wote  25  wa Jubilee  hutoa pato la shilingi millioni1.2 kila mwezi  kando na mamia ya wawakilishi wa kaunti  ambao pia hutoa michango yao chamani.

Wabunge wake watano wa EALA hutoa shilingi 20,000 kila mwezi.  Hatua ya kutaka stakabadhi za kifedha za chama imejiri baada ya washirika wa Ruto chamani humo kupa kusalia ndani ili kuendeleza mapambano yao wakiwa ndani ya Jubilee.

 

Aluta Continua: Ruto aendelea na mipango ya kuchukua usukani,aamua kukabiliana na Uhuru

Naibu wa rais William Ruto anatafuta chombo mbadala cha kutumia kuwania urais mwaka wa 2022 huku ishara zikionyesha uwezekano wa kuzuka  makabiliano makali  kati yake na rais Uhuru Kenyatta.

Ruto 1

Kwa mara ya kwanza baada ya meizi kadhaa ya kuonekana kutengwa na washirika wake kulengwa,  Ruto siku ya Jumamosi alifunguka na kusimulia masaibu ambayo washirika wake wanayapitia serikalini na bungeni   katika kijembe aliochoonekana kumuelekezea mkuu wake, Uhuru .Uhuru  ametekeleza mageuzi makubwa katika uongozi wa mabunge yote mawili katika kilichoonekana wazi kama njama ya kukabiliana na ushawishi  wa Ruto kisiasa tunapoelekea uchaguzi mkuu wa 20222. Rais Kenyatta amewashtumu  Ruto na washirika wake kwa kuhujumu ajenda yake ya maendeleo na badala yake kuendeleza siasa za urithi.

Baada ya kumtimua Duale ,Uhuru sasa anajitayarisha kulirekebisha baraza la mawaziri na ripoti ya BBI

Hatima ya Ruto katika chama cha Jubilee inaendelea kuwa katika hali ya mizani  na huenda anapanga kikakatai ya kujiondoa wakati ufaao ili kukitumia chama kingine kugombea kiti cha urais . Duru zaarifu kwamba  washrika wa Ruto wanazinghatia kukitwa chama  The Party of Development and Reforms (PDR).

PDR  kina ushawishi mkubwa miongoni mwa jamii za wafugaji wa kuhama hama  na  miongoni mwa vyama tanzu vya Jubilee . Kabla ya uchaguzi wa mwaka wa 2017  PDR   kilikuwa kikiendeshwa katika afisi ya Naibu wa rais  katika jengo la  Transnational Bank House  kwenye barabara ya  City Hall Way. Afisi hizo katika ghorofa ya tisa   zilikuwa zikitumiwa kama afisi ya kibinafsi ya naibu wa rais  tangu mwaka wa 2007 alipokuwa mbunge wa eldoret kaskazini . Duru zaarifu huenda chama hicho kikabilishwa jina  na kisha kuboreshwa ili kutumiwa na Ruto .

Baadye DP atafanya mikataba ya ushirikiano na vyama vingine  ili kujenga muungano thabiti wa kisiasa kukabiliana na mrengo ambao utaungwa mkono na rais Kenyatta pamoja na mshirika wake mpya kisiasa bwana Raila Odinga .

Ni kubaya! Ruto anyolewa baada ya mgao wa bajeti yake kupunguzwa kwa asilimia 40

Wandani wanasema chama cha waziri wa zamani wa Kilimo Mwangi Kiunjuri  Service Party  na the  Transformational National Alliance  kinachohusishwa na mbunge wa  gatundu kusini  Moses Kuria vitakuwa katika muungano wa Ruto kwa matayuarisho ya uchaguzi mkuu wa 2022 .

The United Green Party (UGP)  na  Grand Dream Development Party (GDDP) pia ni baadhi ya vyama ambavyo Ruto analenga kushirikiana navyo katika mpango  huo wake. Kuna mikakati pia ya kuwashawishi Musalia Mudavadi wa ANC na Moses Wetangula wa Ford Kenya kujiunga na mrengo wa naibu wa rais .Chama cha PDR kinatarajiwa kuzinduliwa hivi karibuni kwa lengo la kukipa umaarufu .tayari chama hicho kipo katika mkataba wa ushirikiano na chama cha  Jubilee .

 

 

 

Baada ya kumtimua Duale ,Uhuru sasa anajitayarisha kulirekebisha baraza la mawaziri na ripoti ya BBI

Rais   Uhuru Kenyatta sasa anaweza kutangaza mabadiliko katika baraza la mawaziri na kuipokea ripoti ya BBI katika kipindi cha wiki mbili zijazo baada ya kufaulu kuwafurisha washirika wote wa naibu wake William Ruto kutoka nyadhifa za uongozi bungeni.

Touble ni Amani: Mudavadi sio kinara wa chama cha ANC Osotsi

Katika mkutano uliodumu kwa dakika 22  wa  wabunge wa Jubilee, rais aliongoza kutimuliwa kwa Aden Duale kama kiongozi wa wengi bungeni na nafasi yake kuchukuliwa na mbunge wa Kipipiri Amos Kimunya . Hatua  hiyo sasa inatoa fursa kwa rais Kenyatta kuweza kutangaza mageuzi katika baraza la mawaziri na pia kuhakikisha kwamba mapendekezo ya  jopo la BBI yanapitishwa bungeni bila vikwazo.

Ruto  amekuwa akipinga baadhi ya mapendekezo ya BBI huku washirika wake wakidai   kwamba mchakato huo mzima ulikuwa njama ya kumzuia kumrithi Kenyatta mwaka wa 2022. Duru zaarifu kwamba viongozi kadhaa wa upinzani na washirika wao watajumuishwa katika baraza jipya la mawaziri kando na kutengewa nafasi mbalimbali katika nyadhifa zingine kuu serikalini. Siku ya Jumatatu, Ruto alishuhudia  bila kuwa na uwezo wa kumsaidia  Mshirika wake Duale aliposalimishwa mbele ya wabunge na kupigwa shoka la kutimuliwa kutoka uongozi wa shughuli za serikali bungeni.

New Home? Ruto na Washirika wake waanza kutoa ishara za kufanya rasmi mrengo wao kabla ya uchaguzi

Ruto  alidinda mara mbili mualiko wa kuzungumza katika mkutano huo uliofanyika kwenye ukumbi wa KICC lakini baadaye akatumia twitter kumtumia Duale ujumbe wa kumsifu na kumtaja kama kiongozi aliyejitolea kulihudumia taifa kwa  ukakamavu na kwa njia ya kipekee. Aliandika ;

“ Kaka yangu Aden Duale, wewe ni kiongozi shupavu. Kwa miaka minane umetekeleza majukumu yako vyema kama kiongozi wa wengi bungeni. Rafiki yangu, historia ya bunge ikiandikwa lazima  sura nzima itakuwa kukuhusu. Mbele iko sawa na Mungu’

Ruto hata hivyo hakumhongera mrithi wa  Duale Amos Kimunya ambaye aliteuliwa na rais Kenyatta kuichukua nafasi hiyo. Pia hakumtaja mbunge wa Eldas Adan Keynan ambaye ndiye katibu wa pamoja wa  Muungano wa Jubilee

 

Wandani wa Ruto watofautiana baada ya William Ruto kutoa kadi yake ya kisiasa

Sasa ni wazi kuwa huenda Naibu Rais William Ruto akajiondoa kutoka chama cha Jubilee na kuingia chama chake. Hilo lilidhihirika Alhamisi, Juni 18, wakati DP Ruto alikutana na wabunge 16 katika afisi za Jubilee Asili Centre.

Inaaminika DP William Ruto ameunda chama hicho atakachowania urais nacho ifikapo 2022 baada ya masaibu kumzidi ndani ya Jubilee.

DP ndiye naibu wa chama cha Jubilee huku Rais Uhuru Kenyatta akiwa kiongozi wa chama. Hata hivyo, DP amekuwa akipokea kichapo kikali kisiasa kutoka kwa maafisa wengine kama vile katibu Raphael Tuju na naibu mwenyekiti David Murathe.

“Nimekuwa na chakula cha mchana na wabunge wa Jubilee ambao hivi karibuni walitolewa kwenye nyadhifa zao na kupewa wajibu mwingine. Niliwashukuru kwa kazi yao kwa chama na taifa,” alisema DP kuhusu mkutano wake na wabunge hao katika makao ya Jubilee Asili.

Huku kauli mbiu ya chama cha Jubilee ikiwa ni ‘Tuko Pamoja’, DP alimalizia ujumbe wake ‘Sote Pamoja’ katika kile kiliashiria usemi wa chama hicho kipya.

Hatua ya DP ilijiri siku moja tu baada ya Murathe na Tuju kuongoza Jubilee kutia sahihi mkataba wa ushirikiano na chama cha Wiper na CCM.

104383045_3572439039451274_5104904251102928504_o104444835_3572439186117926_4142137434990055815_o

Hatua ya DP inatarajiwa kuzua hisia kali za kisiasa ndani ya Jubilee wakati ambapo Rais Kenyatta anaonekana kutangaza vita dhidi ya wandani wa Ruto.

Tayari Jubilee Asili ina ukurasa wa Facebook ambapo picha ya DP imewekwa na kutangazwa kama chama cha kisiasa.

Seneta wa Elgeyo Marakwet Kipchumba Murkomen, hata hivyo, alisema Jubilee Asili si chama kingine mbali ni nyumba ya wanaoamini kuhusu ajenda ya awali ya Jubilee.

104549666_3572439682784543_1468469773586660188_o

“Tulikuwa na mkutano na DP katika jumba la Jubilee Asili Centre. Ni makao ya wanachama wote si chama mbadala kwa Jubilee

Ni makao ya wanachama wanaoamini kuhusu ajenda ya awali ya Jubilee.” Murkomen alisema.

Hata hivyo, Mbunge wa Soy Caleb Kositany ambaye pia ni naibu katibu wa Jubilee alisema kuna mipango ya kusajili Jubilee Asili kama chama cha kisiasa.

“Sisi kwa Jubilee hakuna demokrasia, hakuna tena kujadiliana, imekuwa ni kama klabu ya watu wachache ambapo wanachama wanaamriwa kile watafanya. Kama hawatapinga kusajiliwa, basi tutakuwa na chama cha Jubilee Asili.” Alisema Kositany.

Vyama vya Kalonzo, Rutto vyasiani mkataba wa Kujiunga na Jubilee

Vyama vya Wiper  na  CCM  vimesaini mkataba wa  ushirikiano na chama cha Jubilee cha rais Uhuru Kenyatta .

COVID 19: Akina mama walio na corona wanaweza kuwanyonyesha wanao ili mradi wavalie maski-Wizara ya afya

Kiongozi wa Wiper  Kalonzo Musyoka na gavana wa zamani wa Bomet  Isaac Rutto  walikuwa katika hafla  hiyo katika makao makuu ya chama cha Jubilee . Katibu mkuu wa chama cha   Judith Sijeny  amesema lengo lao kujiunga na Jubilee kupitia makubaliano hayo ya ushirikiano   ni kuwaleta watu pamoja . Mwezi uliopita  baraza kuu la usimamizi wa chama cha Wiper Lilimpa kalonzo Idhini ya kusainia makubaliano ya kushirikiana  na Jubilee . Mwafaka uliafikiwa baada ya mkutano uliofanywa kupitia njia ya video na zaidi ya watu 50

Rutto

Wanachama hao  waliunga mkono kwa kauli moja kutekelezwa  kwa mkataba huo wa ushirikiano huo. Wakati wa mkutano huo  Kalonzo amesema makubaliano hayo  haumaanishi kwamba wamejiondoa kutoka  muungano wa NASA .

Maafisa wawili wa IT waliowapiga picha ais Uhuru na Raila CBD washtakiwa

Mkataba huo  unajiri  baada ya chama cha Kanu pia  kusaini mkataba   wa ushirikiano nan a Jubilee. Mkataba huo wa Kanu na Jubilee ulifanikisha kuteuliwa  kwa seneta wa West Pokot Samuel Poghisio wa  Kanu  kutajwa kuwa kiongozi wa walio wengi katika senate .

tuju

Mwezi ulipita Rutto  alifichua kwamba  alikuwa akijadili mkataba wa ushirikiano  wa kisiasa na rais Uhuru Kenyatta .Rutto ni mshirika wa karibu wa seneta wa Baringo   Gideon Moi  ambaye pia chama chake cha KANU kipo katika makubaliano ya kisiasa na Jubilee .

 

 

Tanga Hama : Washirika zaidi wa DP Ruto wamkimbilia Raila

Naibu wa rais William Ruto amepata pigo jingine baada ya washirika wake  watatu muhimu kuiacha kambi yake na kujiunga na mrengo wa rais Uhuru Kenyatta na kiongozi wa ODM Raila Odinga.

Watatu hao ni katibu msimamizi wa wizara ya ardhi Gideon Mung’aro,  mbunge wa Laikipia kaskazini  Sarah Korere  na mfanyibiashara wa pwani  Suleiman Shahbal.  Wote walikuwa katika afisi za Raila za Capital Hill ili kutangaza misimamo yao kujiunga na mrengo wa rais na bwana Odiga huku wakijitenga na kundi la tanga tanga. Wa kwanza kuvuka  laini na kujiunga na upande wa pili ni mwakilishi wa akina mama wa Laikipia  Catherine Waruguru. Korere  wakati mmoja alikuwa mtetezi sugu wa DP Ruto  na kauli zake za pingamizi dhidi ya sera za rais Kenyatta na azama ya kisiasa ya Bwana Odinga zinafahamika na wengi. Pia amekuwa mksoaji mkubwa wa mwafaka wa handshake kati ya rais Kenyatta na Odinga.

Who’s Next? Jeshi la Ruto Bungeni lapatwa na hofu baada ya washirika wake senate kufurushwa

Alikuwa miongoni mwa wajumbe wa Jubilee waliolengwa na shoka la kutimuliwa kutoka kamati za bunge lakini sasa amejitokeza na kutangaza kwamba anaunga mkono mwafaka wa handshake  na  BBI. Alikuwa ameandamana na seneta wa  Narok Ledama  ole Kina  alipotangaza kujiunga na mrengo wa Uhur-Raila Kutoka kundi la tanga tanga.

“ Nimempokea mbunge wa Laikipia North  Sarah Korere ambaye ameunga mkono  jitihada za kuliunganisha taifa’ Raila aliandika katika twitter muda mfupi baada ya  kukutana na mbunge huyo.

Aluta Continua: Uhuru sasa kuwafurusha washirika wa Ruto Katika kamati za senate

Tangu chama cha Jubilee kiwafurushe viongozi wa  seneti na bunge waliokuwa katika mrengo wa Ruto kutoka nafasi za uongozi, baadhi ya wabunge kutoka mrengo wake wamekuwa wakizingatia kubadilisha misimamo kisiasa ili waweze kuepushwa na shoka la kuonyeshwa mlango. Gazeti  la The Star limeripoti kugundua kwamba  wabunge wengi wanaomuunga mkono Ruto ambao wanalengwa kuondolewa katika kamati za bunge wanapanga kukutana na Raila  wiki zijazo .

Ruto Ruto amesalia kimya tangu shoka kuwakuta washirika wake  Kithure Kindiki  wa Tharaka Nithi, Kipchumba Murkomen wa Elgeyo Marakwet, Susan Kihika wa  Nakuru, Benjamin Washiali wa Mumias mashariki na  Cecily Mbarire(Mteule). Raila  pia amekutana na  mwanasiasa wa pwani CAS Mung’aro  na Shahbal  ili kujadili masuala mbalimbali yanayohusu ‘maendeleo ya eneo la pwani’.