“Simama wakuone kijana mfupi round” – Mbusii amuita Uche

Katika shoo ya Papa Na Mastaa, Mbusi alifunguka kuhusu anavyofanya kazi na deejay wake Uche Adi Rasta. Uche ni kati ya madeejay wanaofanya na mtangazaji huyu katika shoo ya Mbusi Na Lion TekeTeke katika kituo cha Redio Jambo kuanzia saa tisa hadi saa moja jioni.

Katika mahojiano hayo ambayo hufanyika kwa mastaa wanaofanya sanaa nchini, Mbusi alimwambia Uche asimame aonekane na watazamaji.

“Simama wakuone kijana mfupi round. Uche namchukulia kama small brother.” alisema Mbusii

radiojambodj

Soma hapa:

“Nikiingia Mombasani nione Fatuma sitambania” – Mbusii

Uche pia alielezea anavyomfahamu bosi wake na kusema kuwa ni mtangazaji ambaye inakuwa rahisi kufanya kazi naye huku akisimulia kuwa hawajahi kuwa katika matatizo katika kazi zao.

“Mbusi ni mtu ambaye mwenye heshima. Anakubali chochote unamwambia.” alisema Uche.

Mbusi alieleza jinsi yupo katika mstari wa kwanza kuunga mkono muziki wa hapa nchini ili kuwainua wasanii.

mbusihnaliondehplayful

“Mbusi Na Lion TekeTeke supporting local content.”

Mbusi alionekana pia kuwakanya mabinti wanamitindo na kusema kuwa waende polepole katika kazi zao huku akisisitiza kuwa hawezi kuwabania katika mahusiano.

“Na hao unawaita watoto waambie waende polepole tafadhali.”

 

Soma hapa:

King Kaka afunguka kuhusu kufanya collabo na mzazi mwenzake Sage

Je, ushawahi jiuliza ni nani huyu “kijana fupi round”?

Ucheshi wa “kijana fupi round” umeteka anga za ucheshi kwa takriban mwezi mmoja sasa.

Tamko hili ambalo limewafanya wakenya kulifurahia katika mitandao ya kijamii lilifanyika wakati na ambapo gavana wa kaunti wa Pokot Magharibi mheshimiwa  John Lonyangapuo alikuwa akihutubia wananchi na kuonekana kupandwa na mori sana.

Gavana huyu alionekana kugadhabishwa na mwanasiasa aliyegombea kiti cha mwakilishi wodi na kupoteza kwa mpinzani wake wa karibu. Katika hotuba hiyo gavana huyu anadai kuwa mwanasiasa huyu alipata kura tatu na kuaibisha chama chake cha KANU.

President Uhuru bursts out laughing with Governor Lonyangapuo about ‘kijana fupi amenona’ joke

Gavana huyu alikuwa anamtupia vijembe mwanasiasa katika kaunti yake anayefahamika kama Dennis Ruto. Mwanasiasa huyu ni katika ya watu wanaopinga uchaguzi wake gavana John.

Ruto alitaka kujua na kuelezwa sababu zinazomfanya naibu wa gavana kaunti hiyo kuwahudumia wananchi akiwa nchi za ng’ambo Marekani badala ya kuwahudumia watu akiwa nchini.

Rais Kenyatta amtembelea na kumfariji Rais Mstaafu Moi kufuatia kifo cha Jonathan Moi

Tamko la gavana huyu linaonekana kutamba kwa kasi sana na kukamata hisia za wengi huku Rais Uhuru Kenyatta akiwa miongoni mwa wakenya wanaofurahishwa sana na jinsi ucheshi huu unavyotokea. Wawili hawa walikutana hapo jana kipindi na ambapo Rais alikuwa ameenda kumfariji aliyekuwa rais wa Kenya mzee Moi kwa kumpoteza mwanawe Jonathan.

Denis Ruto ambaye ameanzisha vuguvugu la kumpinga Lonyangapuo linalokwenda kwa jina Mulmwas katika mahojiano na vyombo vya habari  anadokeza kuwa alihisi vibaya sana aliposikia kwa mara ya kwanza.

Ruto aligombea kiti cha mwakilishi wa wodi ya Lelan katika mkoa wa Pokot Kusini na tikiti ya chama cha KANU  na kupoteza kwa mpinzani  wake Johnson Lokato .