Siwezi amini haya,’Muigizaji Luwi amuomboleza Pretty Mtave

Kumpoteza umpendaye au rafiki yako ni jambo ngumu sana na la huzuni huku familia ya kipindi  cha Maza, Moyo na Aziza wakimuomboleza mmoja wao Pretty Mutave ambaye aliaga dunia mnamo Septemba 15.

Waigizaji wenzake,marafiki na wakenya walituma risala za rambi rambi zao kwa familia huku wengi wakimsifu.

Muigizaji mwenzake wa kipindi cha Maza Luwi Capello, kutokana na ujumbe wake wawili hao walikuwa wanataniana na hata kuwa marafiki wa karibu sana.

0D375641-C756-483E-B37F-E5281EB3E41D

Kupitia kwenye ujumbe huo Luwi alisema kuwa hajaamini ya kuwa Pretty hayupo tena.

“Nilikuwa nakuita Pretty Pretty, bado sijaweza kuamini haya, wacha Mungu ailaze roho yako mahali pema peponi kwa kweli maisha ni mafupi.” Luwi aliandika.

Mungu azidi kuilaza Roho yake mahali pema peponi.