Uhuru aifurusha bodi ya Huduma za Feri

Rais Uhuru Kenyatta siku ya Alhamisi aliwapiga kalamu wanachama wote wa bodi ya huduma za feri nchini kutokana na mkasa uliosababisha vifo vya Mariam Kighenda na mwanawe Amanda katika feri ya Likoni.

 

Kwenye gazeti rasmi la serikali la tahere 16 Okotoba, Uhuru alifutulia mbali uteuzi wa Dan Mwazo kama mwenyekiti wa bodi hiyo na wanachama Daula Omar, Naima Amir, Philip Ndolo na Rosina.

Waititu Atapatapa Akitaka Uhuru Amsaidiye Katika Kesi Ya Ufisadi Dhidi Yake

Notisi hiyo kutoka ikulu ilisema:

IN EXERCISE of the powers conferred by section 7 (3) of the State Corporations Act, I, Uhuru Kenyatta, President and Commanderin-Chief of the Defence Forces of the Republic of Kenya, revokes the appointments of Dan Mwazo, Daula Omar, Naima Amir, Philip Ndolo, Rosina Nasigha Mruttu, as Non-Executive Chairperson and members of the Kenya Ferry Services Limited, with effect from the 16th October, 2019,”

Kulingana na ripoti za daktari, Mariam na Amanda walifariki kutokana na kukosa hewa ya oxijeni baada ya kuzama majini.

Miili ya wawili hao iliopolewa kwenye bahari siku 13 baaada ya ajali hiyo.

“Uso wangu ulikuwa kama nyama ilioteketezwa,” – Kelvin Kairo

 

Hela yatolewa kufadhili mazishi ya Mariam Kighenda na Amanda, KFS yatoa pole

Shirika la feri nchini limetoa taarifa kuwa imeikabidhi familia ya marehemu Mariam Kighenda na Amanda Mutheu shilingi  200,000 ili kusaidia familia yake kwa mazishi.

John Wambua pia amepokea 682,500 kutoka kwa kampuni ya bima ya gari lake

Shirika hili limetoa taarifa hizo kupitia mtandao wa Twitter.

(+Video) Harmonize alivyomfurahisha Pombe Magufuli, dili na Wizkid

Haya yanajiri baada ya mmewe John Wambua kukana taarifa za huenda mkewe alijiua kupitia mkasa huo.

Katika mahojiano na kituo cha runinga cha NTV, mmewe Mariam John Wambua alitetea mkewe kuwa hakuna uwezekano wowote wa kurudisha gari nyuma na kutumbukia baharini.

“Hii leo serikali (KFS) imeikabidhi familia ya marehemu Mariam Kighenda na mtoto wake Amanda Mutheu shilingi 200,000….” KFS ilichapisha katika Twitter.

Barua ghushi ya kuua Ruto, Dennis Itumbi akabiliwa na mashtaka mapya

Wambua alikuwa akikana taarifa kuwa huenda mkewe alikuwa na njama ya kujiua pamoja na mtoto wake.

 Bwanake alisema kuwa gari la mkewe lilikuwa katika hali ya kuegeshwa huku akiwasihi wanapolisi kuharakisha zoezi la uchunguzi.

Haya yanajiri huku feri zilizopo katika kivukio hicho zikidaiwa kuwa mzee zaidi na zina zaidi ya miaka 30.

Kwa umbali, mabati ya feri hizo yana kutu kuashiria uzee.

Milango ya feri hizo na sehemu za kukanyagia unapoingia zimezeeka zaidi.

Wengi wanahoji kuwa hali mbovu ya feri pamoja na utepetevu kazini zilichangia pakubwa na kuwa ajali hii ingeepukika.

Aidha, nyufa za mamlaka ya feri nchini kukosa kuajiri wapiga mbizi ili waweze kusaidia kunapotokea ajali zimeonekana wazi.

Miili ya Mariam Kigenda na mwanawe wa miaka minne Amanda ilipatikana ikiwa imekumbatiana katika kiti cha nyuma ndani mwa gari lao.

Kisa hicho bado kinachunguzwa kwa kina ili kubaini kilichojiri.