Polisi wapewa siku 30 kung’amua kilichomuua mwanamke mmoja Kilimani

Washukiwa watatu waliohusishwa na  mauaji ya mwanamke ambaye mwili wake ulipatikana nje ya nyumba moja mtaani Kilimani  watakuwa wakiripoti katika kituo cha polisi eneo hilo kwa siku 30 huku uchunguzi ukiendelea.

Kaimu mkuu wa milimani Martha Mutuku amewapa polisi siku 30 kutengeza ripoti  kuhusiana na mauaji hayo  ya Sheila  Muruge.

Muruge  alipatikana ameaga dunia  karibu na  shamba la maua  Julai tarehe 17  baada ya usiku wa karamu na kulewa.

14 wafariki huku visa vipya 606 vya coronavirus vikisajiliwa

Washukiwa, Shem Ng’eno, Christine Awour  na  Claire Chepkoech  wote waliachiliwa kwa bondi ya shilingi laki moja  au dhamana ya shilingi 50,000 pesa taslimu kila mmoja.

Afisa anayechunguza mauaji hayo JOSEPH Nderitu ameiambia mahakama kwamba polisi wamechukua sampuli za DNA  kutoka kwa washukiwa na zinachunguzwa na mwanakemia wa serikali.

Kachero huyo ameongeza kwamba kundi lake linangoja matokeo hayo ili  kuamua hatua itakayochukuliwa  na tayari faili imeshatumwa kwa mkurugenzi wa mashtaka ya umma.

Polisi walitaka vipimo vya DNA  baada ya kutokea ripoti kwamba alidhulumiwa kimapenzi  kwa ajili kulikuwa na ushahidi wa kuwepo mabaki ya manii katika uke wake.

Mahakama imeagiza kwamba washukiwa watakuwa wakiripoti katika kituo cha polisi cha kilimani  kila Jumatatu hadi tarehe 28 Agosti wakati kesi hiyo itakapotajwa kwa maelekezo zaidi.

Hapana Tambua Urembo? Tazama jinsi Polisi walivyomcharaza mwakilishi wa Mlango kubwa Patricia Mutheu

Makachero wanatarajiwa kuiarifu mahakama kuhusu matokeo ya uchunguzi wao  ambapo picha za video kutoka kamera ya CCTV zitachunguzwa.

Siku ya Alhamisi wiki jana, wakili  wa washukiwa aliiambia mahakama kwamba  wateja wake walikuwa na  matatizo ya kiafya na kuwaweka katika seli ni jambo ambalo lingewatia katika hatari ya kuambukizwa Covid 19 kwani polisi hawakua na barakoa za washukiwa.

Watatu hao walikamatwa Julai tarehe 17 katika jumba la makaazi la  Santonio Courts.

Mwanaume apatikana ameuawa na mwili wake kutupwa Naivasha

Idadi ya watu wanaopatikana wakiwa wameuawa na mili yao kutupwa huko Naivasha imeongezeka hadi nne hii leo, baada ya mwanamme mmoja kupatikana ameuawa na mwili wake kutupwa katika barabara ya Moi North Lake.

Visa viwili vya kwanza viliripotiwa siku ya Jumatatu na siku moja baadaye kisa cha tatu kika ripotiwa ambapo mwili ulipatakina kichakani huku uso ukiwa na majeraha.

Mwili wa mwanamme huyo ulipatikana mikono ikiwa imefungwa nyuma na kulingana wakaazi huenda alinyongwa na waya kabla ya mwili wake kutupwa katika bara bara hiyo.

Kulingana na kiongozi wa eneo hilo Boniface Waiganjo, mwanamme huyo hakuwa stabadhi yoyote ya kumtambua. Aliongeza kuwa watu wote wanne si wakaazi wa eneo hilo na huenda waliuawa mahala kwingine kisha kutupwa eneo hilo.

Mwanamke raia wa Kenya apatikana amefariki Australia

Wakaazi sasa wanantaka uchunguzi wa kina kufanywa kuhusu mauaji hayo na wahalifu wanaotekeleza unyama huo kukamatwa.

“Hii ni mara ya kwanza tumeshuhudia visa kama hivi eneo hili na tunaomba polisi kuanzisha uchunguzi mara moja,” Waiganjo alisema.

OCPD wa Naivasha Samuel Waweru alithibitisha kisa hicho na kusema kuwa mwili umepelekwa katika chumba cha kuhifadhi maiti.

Huku hayo yakiarifiwa shughuli ya kumtafuta mwanamke mmoja huko Mia Mhiu iliishia majonzi baada ya mwili wake ulokuwa ukioza kupatikana umefungiwa nyumbani kwake.

Inakisiwa kuwa mwanamke huyo aliaga dunia siku ya Jumatatu kabla ya mwili wake kupatikana leo.

Chifu wa eneo hilo alidhibitisha kisa hicho.