Covid-19: Watu 492 wapatikana na virusi vya corona

Kenya hii leo imerekodi visa 492 vipya vya maambukizi ya corona na kufikisha idadi ya jumla 26,928 ya watu walioambukizwa virusi hivyo hii ni kutokana na sampuli 4063 zilizopimwa chini ya saa 24.

Watu 534 wamepona kutokana na virusi hivyo na kufikisha idadi jumla ya 13,495 ya watu waliopona virusi vya corona Mutahi Kagwe alisema.

Kaunti ya Nairobi inazidi kuongoza kwa maabukizi hayo huku hii leo ikifuatwa na kaunti ya Garissa, huku haya yakijiri watu wengine watatu wameaga dunia kutokana na virusi hivyo na kufikisha idadi ya jumla 423 ya watu walioaga dunia kwa ajili ya virusi vya corona.

Huku akizungumza alisema kuwa hospitali zinapaswa kuzingatia kupeana ripoti zifaazo za maambukizi ya corona, pia alisema kuwa mgonjwa wa umri wa chini ana miezi kumi na moja na wa juu ana miaka 83.

 

Siwezi kujiuzulu! Asema Kagwe

Waziri wa Afya  Mutahi Kagwe  amesema kwamba hatojiuzulu.

Akizungumza  katika kikao  na wanahabari huko Kisumu  siku ya Jumapili  alisema kwamba ni ndoto kwa baadhi ya watu kumtaka ajiuzulu.

“Suala ambalo watu wanalitumia kunitaka nijiuzulu ni ndoto. Wanaweza kuendelea kuota,” amesema

Covid-19: Watu 599 wamepatikana na virusi vya corona huku 1,064 wakipona

Aliendelea kusema kwamba hana mtoto aliye chini ya umri wa miaka 18 katika nyumba yake  baada ya video kusambazwa mtandaoni inayodaiwa kuwa  ya mwanawe wa kiume akiwa katika karamu licha ya agizo la serikali kuzuia watu kukongamana kwa hafla kama hizo.

“Kuhusu suala la video ya  mwanangu akiwa katika karamu … sina mtoto wa kiume aliye chini ya umri wa miaka 18 katika nyumba yangu hatua inayomaanisha kwamba wote ni watu wazima. Mnaweza kuwafuata na kuwauliza,’ Kagwe alisema

Hafla za tohara lazima zifuate masharti ya afya kuhusu covid-19 – Kagwe

Kuhusu suala la covid 19 nchini  Kagwe alisema vis avipya 599 vya ugonjwa huo viliripotiwa  na kufikisha jumla ya visa hivyo kuwa  6,436.

Watu 1,062 pia amepona virusi hivyo na kufikisha idadi ya waliopona 12,961.

Hata hivyo watu 2 waliaga dunia na kufikisha jumla ya walioaga dunia kwa ajili ya virusi hivyo kuwa  420

Covid-19: Watu 781 wamepona huku 699 wakipatikana na virusi vya corona

 

Watu 781 wameruhusiwa kuenda nyumbani baada ya kupona virusi vya corona huku idadi ya waliopona ikifika 11,899watu waliopona, haya yakijiri watu,699 wamepatikana na virusi vya corona na idadi kufika 25,837 ya watu walioambukizwa virusi hivyo.

Hii ni kutokana na sampuli 7,175 zilizopimwa chini ya saa 24, wagonjwa 427 ni wanaume bali 272 ni wanawake amesema waziei wa afya Mutahi Kagwe.

Kaunti zote za rekodi visa vya maambukizi ya corona-CS Mutahi Kagwe

Hii leo watu 5 wamepoteza maisha yao kutokana na virusi vya corona na kufikisha idadi ya jumla 418 ya watu walioaga kutokana na corona.

Mutahi Kagwe
Mutahi Kagwe

Akizungumza akiwa katika kaunti a Kakamega Mutahi amesema kuwa mgonjwa wa umri wa chini ana mwaka mmoja na huku aliye na umri wa juu akiwa ana miaka 89.

Watu 14 wameaga dunia huku 727 wakipatikana na corona

Pia alimpongeza gavana Wycliffe OParanya kwa kazi yake nzuri, alioifanya kwa kuzuia kusambaa kwa maambukizi ya corona.

Kaunti zote za rekodi visa vya maambukizi ya corona-CS Mutahi Kagwe

Waziri wa afya Mutahi Kagwe ijumaa huku akitangaza maambukizi ya corona alisema kuwa kaunti zote,47 zimesajili visa vya maambukizi ya virusi vya corona.

Akiwa katika kaunti ya kisii alipokuwa amekaribisha na gavana wa kaunti hiyo James Ongwae, alitangaza habari hizo na kusema kuwa kaunti zote zinapaswa kuwa tayari kukabiliana na virusi hivyo.

“Kesi za maambukizi ya corona zikiendelea kuongezeka nchini itakuwa vigumu sana kujuwa na kufahamu kesi hizo za maambukizi ni za kaunti gani

Tunapaswa kuwa na uwezo wa kukabiliana na virusi vya corona.” Alizungumza Mutahi.

Mutahi Kagwe
Mutahi Kagwe

Pia alikumbush wanachi kuwa kuna virusi ambavyo vinachukua maisha ya wananchi kila siku mbali na corona huku akiupa ugonjwa wa saratani kipaumbele na ambao umeathiri maisha ya wananchi sana.

Mutahi aliwaambia wananchi wasichoke kuenda hospitali kwa ajili ya uoga wao wa kuambukizwa virusi vya corona, wanapaswa kuenda na kupokea matibabu.

IMG-20200807-WA0007

“Tumejua kuwa kunawagonjwa ambao hawatembelei mahospitali zetu kwa maana wanaogopa kuambukizwa virusi vya corona tumechukua hatua kuhakikisha vifaa vya corona vimetengwa na vifaa vya hospitali ya kawaida So msiogope, endeni hospitalini kama uko na ugonjwa.”

 

 

Watu 14 wameaga dunia huku 727 wakipatikana na corona

Kenya hii leo imesajili visa 727 vya maambukizi ya corona na kufikisha idadi ya jumla 25,138 ya watu walioambukizwa virusi hivyo amesema waziri wa afya Mutahi Kagwe.

Watu 538 wapatikana na covid 19 huku 8 wakiaga dunia

MUTAHI KAGWE

Huku haya yakijiri watu wengine 14 wameaga dunia kutokana na virusi hivyo na kufikisha idadi ya 413 ya watu walioaga dunia, pia watu 674 wameruhusiwa kwenda nyumbani baada ya kupona virusi hivyo na kufikisha idadi ya 11,068 waliopona kutokana na corona.

Watu 711 ni wakenya huku 16 wakiwa ni raia wa kigeni.

23 Waaga dunia huku 727 wakipata na Covid 19

Watu 23 Wameaga dunia kutokana na ugonjwa wa Covid 19  huku wengine 727 waklipatikana na virusi hivyo katika saa 24 zilizopita .Idadi ya visa vya ugonjwa huo sasa imefikia 21,363.

Waziri wa afya Mutahi Kagwe amesema idadi hiyo ya waliopatiakana na virusi vya corona ni kutoka sampuli 6371 zilizpoimwa katika kipindi hicho . Idadi ya walioaga dunia leo sasa inafikisha jumla ya vifo vilivyosababishwa na ugonjwa huo kuwa  364.

[Picha ] KQ yafanya ziara ya kwanza London baada ya zafari za kimataifa kuanza

Kati ya visa vipya vilivyosajiliwa kuwa na cvid 19  Kagwe amesema 696 ni wakenya ilhali 31 ni raia wa kigeni .

Akizugumza katika uwanja wa  ndege wa JKIA Kagwe amesema serikali imeamua  kurejelea  safari za kwneda nje ya nchi sio kwa sababu ya kupungua kwa visa vya ugonjwa huo ila kwa ajili lazima tuanze  kuendelea na shughuli za kawaida chini ya hali ya sasa kwa sababu hakuna nayejua ni lini ugonjwa huo utaweza kukabiliwa .

Covid-19:Watu 723 wapatikana na virusi vya corona huku 16 wakifariki

Watu 723 wamepatikana na virusi vya corona huku idadi ya maambukizi ya virusi hivyo ikifika 20,636, Visa hivyo vipya  vimetokana na sampuli 8,679 ambazo zilipimwa katika kipindi cha  saa 24 zilizopita .

Katka visa hivyo vipya watu 450 ni wanaume na 273 ni wanawake, kulingana na miaka aliye na umri wa chini ni mtoto wa miezi tisa na umri wa juu ni mgonjwa wa miaka 87.

Covid 19: 14 zaidi wafariki huku visa vipya 788 vya coronavirus vikiripotiwa

Haya yakijiri watu,16, wamefariki kutokana na virusi hivyo na idadi hiyo kufika 341, pia watu 44, wameruhusiwa kueenda nyumbani na kufikisha idadi ya waliopona 8165 waziri wa afya Mutahi Kagwe alisema.

Pia aliwatakia Waislamu wote sikukuu njema,huku akiwashauri wazingatie amri na maagizo ya wizara ya afya wakati huu wanasherehekea.

Mutahi alisema kati ya walioaga dunia leo, kuna mwanamke wa miaka 22, ambaye aliaga akiwa kwenye hospitali kuu ya Kenyatta huku kumi walioaga ni wa kutoka katika hospitali ya Kiambu ya level five.

 

Wafanyakazi wa afya walioambukizwa virusi vya corona ni 634-CS Mutahi Kagwe

Waziri wa afya Mutahi Kagwe Jumatano alithibitisha kuwa jumla ya wafanyakazi wa  afya walioambukizwa na virusi vya corona sasa imefikia 634.

Akiongea haya Mutahi alikuwa anatangaza maambukizi ya kila siku ya virusi vya corona huku akisema kuwa idadi hiyo ya wafanyakazi wa afya imebeba asilimia 3% ya maambukizi ya corona humu nchini.

Hata hivyo, Mutahi aliwaonya wafanyakazi wa afya wanaoasi kutengwa kwa watu walioambukizwa.

“Tunawaomba wafanyakazi wa afya wafuate kanuni za wizara ya afya wao wenyewe, tunajua kuna baadhi yao ambao tabia zao hazipendezi

Kuna kesi ambayo tulikuwa nayo mmoja wa madaktari kutoka hospitali kuu ya Kenyatta ambaye alikuwa amesafiri na badala ya kwenda karantini alikuwa anataka kwenda thieta kufanya upasuaji lakini kwa bahati mbaya hakuweza

Tunamshukuru muuguzi aliyeripoti kesi hiyo, na hatua kali ilichukuliwa, hii wiki kuna daktari ambaye alipatikana na virusi vya corona na alikuwa anataka kukaa kikawaida kwa uaminifu hii ni tabia ya magaidi.” Alizungumza Mutahi.

Hii leo watu 544 wamepatikana na virusi vya cororna huku 12 wakiaga dunia kutokana na virusi hivyo.

Covid-19: Watu12 wafariki huku 544 wakipatikana na virusi vya corona

Watu 544 hii leo wamepatikana na virusi vya corona katika saa 24 zilizopita huku idadi ya walioambukizwa nchini ikiongezeka na kufikisha jumla ya 19,125 walioambukizwa virusii hivyo.

Huku hayo yakijiri watu 12 wamepoteza maish yao kutokana na virusi hivyo huku idadi ya jumla ya 311 ya watu walioga dunia, katika visa hvyo vipya 340 ni wanaume huku 204 wakiwa wanawake.

14 wafariki huku visa vipya 606 vya coronavirus vikisajiliwa

Watu 113 wameruhusiwa kwenda nyumbani waziri wa afya Mutahi Kagwe alisema.

Waziri wa afya Mutahi Kagwa alisema huenda kuongezeka kwa wanaopatwa na maambukizi ni kutokana na msimu huu wa baridi. Aidha Mutahi alionya kuwa idadi ya maambukizi kwa wanawake imeanza kupanda ikilinganishwa na hapo awali.

Ndio hawa:Orodha ya wanahabari waliopatikana na virusi vya corona

“Tunaona idadi ya kina dada ambao wanaambukizwa imeanza kuongezeka. Hatujui ni tabia zimeanza kubadilika ua ni nini,” alisema Kagwa 

14 wafariki huku visa vipya 606 vya coronavirus vikisajiliwa

Kenya leo imesajili visa vipya 606 vya coronavirus na kufikisha jumla ya visa hivyo nchini kuwa   18,585

Visa hivyo ni kutoka sampuli 4,888  zilizopimw akatika saa 24 zilizopita.

Waziri wa afya Mutahi Kagwe  amesema watu 409 ni wanaume ilhali 197 ni wanawake. Mgonjwa aliye na umri wa chini sana ana miezi minne  ilhai mwenye umri wa juu ana miaka 85.

NHIF kulipa gharama za wagonjwa wa Covid-19 KNH, Mbagathi

Watu 75 wamepona ugonjwa huo na kufikisha  7,908 watu waliopona corona hadi kufikia sasa.

Kagwe amesema wanaofanyia kazi nyumbani wanafaa kuhakikisha kwamba wanafanyia katika nyumba zao.

“Nimekuwa risasi nawe pia umekuwa risasi, tumekuwa hatari na  tunaweza kusababisha maafa’ amesema Kagwe

Amewahimiza wazazi kuhakikisha kwamba wanao wananawa mikono kila wakati

Kagwe  amekariri msimamo  wa rais Kenyatta kwamba hakuna atakayesazwa  katika kuhakikisha kwamba kila mmoja anafuata kanuni zilizowekwa kuzuia usambaaji wa virusi vya corona.

Shule zimegeuka kuwa mahame-Walimu wakuu wasema

Amewashauri watu kutosafiri kwenda  mashambani  ama kuwaalika wageni makwao isipokuwa katika hali za dharura .