PATANISHO: Isaac aomba apatanishwe na bibi yake au ameze sumu (Audio)

Bwana Isaac asubuhi ya leo alilia machozi akiomba bibi yake Helen arudi nyumbani, baada ya kutoroka.

Bwana Isaac alishtua Gidi sana akisema ikipita leo na mama hajarudi nyumbani, atameza sumu. Isaac aliarifu wanajambo kwamba

mwezi wa tisa alitoka kazi na kufika nyumbani alipata bibi yake asha toroka nyumbani mwao.

 “Hiyo siku, hatukuwa tumekosana na tumekaa kwa ndoa miaka tatu na amezaa mtoto mmoja. Bibi yangu alitoroka na mtoto wetu juzi mwezi wa tisa. Mapka wa leo sijui ako wapi, na sikumkosea.

Alijaribu kumpigia simu lakini ni kama aliblock nambari yake ya simu.

“Familia yangu imejaribu pia kumpigia simu na wanania rifu, eti ameenda ziara tuu kidogo.”

Gidi aliweza kupigia Bi Helen simu.

Helen alimwelezea Gidi kilicho fanya atoroke nyumbani mwao akisema ni mambo mengi inayo wakumba. “ Nilikasirika kwasababu mtoto aligonjeka lakini Isaac hakujishugulika, nikaamua kwenda zangu.”

Kwa upande wake, Isaac alimwomba Helen msamaha na kumbebeleza.

Bwana Isaac alitofautiana na bibi yake, lakini alikubali makosa yake kabisa akisema haja kata kauli tangu aende mwezi wa tisa.

Helen ali ibua kwamba Isaac alikosa kumfuata, na kusuluhisha mambo ilikuwa ngumu. Helen bado haja amua kitu na anan pumzika tuu, na Isaac asiende kwao nyumbani.

Skiza kanda ifuatayo Isaac akimbembeleza na kumsihi Helen warudiane na matamshi matamu. Isaac alisema atatulia, na kumpatia nafasi Helen aweze kufikiria maisha yake.