SUNSET:Mwisho wa safari ya Rais mstaafu Daniel Moi -1924 hadi 2020.

Daniel Toroitich arap Moi,  alizaliwa tarehe 2 septemba mwaka wa 1924  katika kijiji cha  Kabarak , taarafa ya  Sacho  kaunti ya  Baringo  na alilelewa na mjombake Kimoi Chebii  kufuatia kifo cha babake aliyekuwa mzee . Alitoka  ukoo wa tugen  ambao ni sehemu ya jamii ya kalenjin .baada ya kumaliza masomo yake ya shule ya Upili  katika shule ya sekondari ya Kapsabet  alihudhuria masomo  ya ualimu katika chuo cha Tambach  katika wilaya ya Keiyo. Alifanya kazi kama mwalimu  kutoka mwaka wa 1946 hadi mwaka wa 1955 .

TANZIA: Rais mstaafu Moi aaga dunia

Mnamo mwaka wa 1955  Moi alijitosa katika siasa  alipochagliwa katika  bunge ili kuliwakilisha eneoe la Rift valley katika LEGCO.Aliteuliwa kuichukua nafasi ya  Dr.John Ole Tameno  mwakilishi wa zamani aliyeng’atuka maamlakani kwa sababu ya unywaji pombe kupindukia na kushukiwa kuhusika na vugu vugu la kupigania uhuru . Mwaka wa 1957  Moi alichaguliwa tena kujiunga na legco  na akawa waziri  wa elimu katika serikali  ya kabla ya Kenya kupata uhuru  kati ya mwaka wa  1960–1961. Mwaka wa 1960  alikuwa miongoni kwa walionzisha chama cha KADU  pamoja na Ronald Ngala  ili kupigania uongozi dhidi ya  chama cha KANU kikiongozwa na Mzee Jomo Kenyatta .KADU  ilipigania kuwepo kwa utawala wa majimbo ilhali  Kanu Ilitaka pawepo serikali ya muungano na utawala wa kikapitolisti . Kanu hata hivyo ilikuwa na uthabiti wa idadi ya waakilishi pamoja na kuungwa mkono na Uingereza amayo ilichukua hatua za kuondoa vipendee vyote vya majimbo katika katiba

MKASA:Wanafunzi 14 wafariki katika mkanyagano Kakamega .

Mnamo mwaka wa  1978 Moi alichukua usukani wa kuiongoza nchi wakati mzee Jomo Kenyatta alipoaga dunia .Aliongoza hadi mwaka wa 2002 alipostaafu . Kupitia shinikizo la mageuzi  ,Moi aliruhusu kuwepo mfumo wa siasa za vyama vingi mwaka wa 1991  na kukiongoza chama cha KANU kupata ushindi katika chaguzi za  1992   na 1997 . kabla ya kuwa rais  Moi alihudumu kama makamu wa  rais  kutoka mwaka wa 1967 hadi 1978 .Moi alimua kuendeleza mfumo wa ‘nyayo’ ili kudumisha sera na mtindo wa utawala wa mtangulizi wake Mzee Jomo Kenyatta . Pia alipata jina la sifa kama ‘profesa wa siasa ‘  kwa sababu ya uongozi wake uliodumu miaka 24 na jinsi alivyokabiliana na wapinzani wake .Akiwa na umri wa miaka 95  Moi alikuwa rais mstaafu mwenye umri wa juu zaidi aliyekuwa hai. Februari tarehe 4 2020 ,Daniel Arapa Moi aliaga dunia katika hospitali ya Nairobi . Mwezi uliopita madaktari katika hospitali ya Nairobi walilazimika kumrejesha Moi katika mashine za kumpa usaidizi wa kupumua .Hali yake ya afya imekuwa maaya tangu oktoba mwaka jana  alipolazwa hospitalini .

FREE:Mahakama yawapata bila hatia washukiwa 9 wa mkasa wa Bwawa la Solai .

Wakati huo alipolazwa hospitalini ,msemaji wake Lee Njiru  alisema Moi alikuwa amekwenda hospitali kwa ukaguzi wa kawaida  lakini tangia hapo alilazwa hospitalini mara nne.  Kundi lake la madaktari likiongozwa na  Daktari  David Silverstein  limekuwa likimpa mkatibabu kwa matatizo yanayojirejeeza na kumfanya kusalia kitandani kwa miezi mitatu . Hali ya afya ya Mzee Moi ilizidishwa kuwa mbaya na  jeraha la goti alilopata wakati wa ajali iliyohusisha gari lake mwaka wa 2006 huko Limuru . Mzee Moi angetimu umri wa miaka 96 Septemba mwaka huu

 

Atwoli amshauri Ruto kumwomba msamaha Mzee Moi ili kumrithi Uhuru

Katibu mkuu wa Cotu Francis Atwoli amesema kwamba itakuwa vigumu sana kwa Naibu wa Rais William Ruto kumrithi Rais Uhuru Kenyatta hadi atakapozingatia maadili ya unyenyekevu.

Atwoli ambaye alizuru ngome ya Ruto mjini Eldoret alisema kwamba Ruto anakumbwa na vizingiti vingi na alimshauri kumwomba msamaha Rais mstaafu Daniel Moi.

Alimshauri Ruto kupitia Seneta wa Baringo Gideon Moi akutane na Mzee Moi ili apewe baraka za mzee anapotazamia madaraka ya juu.

“Iwapo hatafanya hivyo basi itakuwa vigumu kwake kuchukua uongozi 2022,” Atwoli alisema.

Alizungumza hayo katika halfa ya kuchangisha pesa katika kanisa la Evangelical Bible mjini Eldoret ambapo aliambatana na wabunge Joshua Kutuny wa Cherangany, Sila Tiren wa Moiben na Wilson Sossion ambaye ni mbunge mteule.

“Ninamshauri Ruto hasipuuze wito huu iwapo anataka kiti cha urais,” alisema.

Masaibu ya Babu Owino, ataja sababu za mahasidi kutaka kumtoa uhai

Miezi mitatu iliyopita, katibu  huyo wa Cotu alizua tafaruku aliposisitiza kwamba jina la Ruto halitakuwa miongoni mwa watakaogombea kiti cha urais 2022.

Akita Eldoret, Atwoli alisema kwamba iwapo Ruto hatapatana na Moi, hasahau azma ya kurithi rais Uhuru.

Hata hivyo juhudi za naibu wa rais William Ruto za kufika Kabarak nyumbani kwake Moi kumeambulia patupu.

Baada ya kusemekana kuwa Seneta wa Baringo Gideon Moi kumzuia Ruto kukutana na mzee.

Maajabu! Jamaa ajitia kitanzi baada ya kujimbia kaburi, Homa Bay

 

Rais Moi yu nafuu na mwenye fahamu, yasema familia

Familia ya rais mstaafu Daniel Moi imesema kuwa amelazwa hospitalini lakini ana ufahamu na anajua aliko.

Msemaji wa familia, Lee Njiru alituma ujumbe Jumanne akisema familia ya Moi haijafurahishwa na jumbe ambazp zinazoenezwa kuhusu afya ya mzee Moi.

Rais Mustaafu Moi alazwa ICU

Njiru alisema kuwa mzee Moi anashughulikiwa na timu ya madaktari wakiongozwa na daktari wake wa kibinafsi, daktari David Silverstein.

“Anajua aliko na mazingira yake. Familia ilisema huku wakirai vyombo vya habari kuchapisha taarifa za matibabu ziliyotolewa kupitia njia rasmi,” Njiru alisema.

“Familia hiyo inafuraha na inashukuru sana Wakenya wote na waatu wa heri njema kutoka ng’ambo kwa sala zao na ujumbe wa ‘kupona haraka’

Njiru alisema familia ya Moi imegundua kwa kuthamini riba kubwa ambayo imeletwa kutokana na kulazwa kwake hospitalini.

“Hii inaarifiwa na hadhi yake kubwa, nchini Kenya na kimataifa,” alisema.