‘Sitasikia vizuri kama mimi nilifinywa na wao hawafinywi,’ Babu Owino amwambia rais

Mbunge wa Embakasi mashariki Babu Owino mnamo Ijumaa Septemba 11, alidai kwamba yuko ndani ya ikulu ambayo itaunda serikali ijayo.

Huku akizungumza alisema kuwa kabla ya hendisheki aliumia sana lakini sasa anakula matunda ya hendisheki kwa amani.

“Hakuna mtu ambaye ameumia sana kama Babu Owino akipigana na Uhuru Kenyatta, nilipelekwa industrial area walifinya kila sehemu ya mwili wangu

Hata hivyo yalikuwa na hendisheki na tulizungumza kulikuwa na hendisheki mbili moja kati ya Uhuru Kenyatta na Raila Odinga na nyingine kati ya Uhuru na Babu

Tangu hendisheki ifanyike tumekuwa tukifanya kazi pamoja, kwa hakika naweza sema kuwa mimi niko ndani ikuluni mimi niko pale ndani kabisa

Tuwe na umoja na tuunge mkono BBI.” Alisema Babu.

Huku akizungumzia wanaomtusi rais Babu alisema kuwa wanaomdharau rais wanapaswa kufinywa vile alifanyiwa wakati huo. Alizungumza haya alipokuwa katika mtaa wa South B wakiwa na mbunge wa eneo hilo Charles Jaguar.

“kwa wale wanamtusi rais, nataka kumwambia ameketi kwenye kiti cha juu Sitaskia vizuri Rais kama mimi nlifinywa na hao hawafinywi.” Alizungumza Babu.

‘Kama kila mtu ataenda kumtusi mama yake nyumbani tutajenga nchi gani?’ Murkomen amjibu Uhuru

Seneta wa Elgeyo Marakwet Kipchumba Murkomen Alhamisi usiku alimjibu rais Uhuru Kenyatta na kuzungumzia jinsi aliweza kumtetea Mama Ngina, Kenyatta alikuwa anajibu maneno yaliyosemwa na mbunge Oscar Sudi na mbunge Johanna Ng’eno, huku Ng’eno akisalia ndani na kisha kutoka kwa dhamana ya milioni moja.

Rais aliwashauri ambao wanatukana mama yake waende wakatukana mama zao, huku usemi wake ukijibiwa na seneta huyo.

‘Murkomen anza kujipanga kuondoka,’Waziri Tobiko aapa kumfurusha Murkomen

” Naelekea kukagua barabara moja hapa chini ambayo tunajenga na itaunganisha  Naiorbi  kupitia  Kiambu  hadi Murang’a kisha ifike Nyeri… niliwaambia mimi haja yangu ni kazi

 Hata kama umri wangu ni mdogo  sina tatizo na kwenda nyumbani ili mradi watu waone kazi ambayo nimefanya . Hawa wajinga  wanaozunguka wakitoa matusi, waambie watusi mama zao na waachane na wangu..” Uhuru Aliwajibu wanasiasa.

Baada ya matamshi yake Uhuru seneta Kipchumba hakupokea vyema usemi huo huku akisema kuwa,

Waziri Tobiko asema Ruto ni karani wa Uhuru na kumtaka Murkomen kuheshimu rais

“Ninatoa wito kwa unyov na uvumilivu nchini, kama kila mtu ataenda nyumbani na kumtukana mama yake tutakuwa tunakuza nchi gani?

Nini kitafanyikia maadili na kanuni zetu kama nchi tuwaonyesha mama zetu upendo na si kuwatukana vita vya jicho kwa jicho zinafanya nchi kuwa kipovu.” Alisema Murkomen.

Nendeni mkawatukane mama zenu, muachane na wangu-Uhuru

Nendeni  mkawatukane mama zenu  na muachane na wangu ,rais Uhuru Kenyatta  amewajibu wanasiasa waliotoa matamshi ya kumshambulia aliyekuwa mama wa taifa  Mama  Ngina Kenyatta .

” Naelekea kukagua barabara moja hapa chini ambayo tunajenga na itaunganisha  Naiorbi  kupitia  Kiambu  hadi Murang’a kisha ifike Nyeri… niliwaambia mimi haja yangu ni kazi ..’ amesema rais

Mbunge Johana Ng’eno aachiliwa kwa dhamana ya shilingi milioni 1

” Hata kama umri wangu ni mdogo  sina tatizo na kwenda nyumbani ili mradi watu waone kazi ambayo nimefanya . hawa wajinga  wanaozunguka wakitoa matusi  ,waambie watusi mama zao na waachane na wangu..’

Uhuru  ambaye alikuwa kizungumza kwa lugha ya kikuyu  amesema viongozi wanafaa kushirikiana kuleta umoja na Amani .

“..  Sitajiruhusu kuzungumza kwa hamaki kwa sababu nawataka wakenya kuishi pamoja kwa Amani’

” taifa litasalia kuwepo lakini sisi kama watu hatutaishi milele’

Matamshi hayo ya rais yanajiri baada ya mbunge wa Emurua Dikiir Johanna Ng’eno na wa kapsrete Oscar Sudi  kurekodiwa wakizingumza matamshi ambayo  yalionekana kumlenga rais Kenyatta na familia yake . Ng;eno baadaye alikamatwa na ameachiliwa leo na mahakama kwa dhamana ya shilingi milioni 1

NCIC Kuchunguza matamshi ya Oscar Sudi kumhusu rais Kenyatta

Baadhi ya viongozi wamejitokeza kutoa onyo dhidi ya mtindo wa kutumia lugha mbaya nay a uchochezi inayotishia Amani ya nchi kabla ya uchaguzi mkuu wa 2022

 

 

Mkuu wa NMS Badi Kuhudhuria mikutano ya baraza la mawaziri baada ya kula kiapo cha kuweka siri

Mkurugenzi mkuu wa  usimamizi wa Mamlaka ya Nairobi  Mohammed Badi  atakuwa akihudhuria mikutano ya baraza la mawaziri baada ya kula kiapo cha kuweka siri .

badi

EACC yawaonya magavana kuhusu azimio la kuvinyima vyombo vya habari pesa za matangazo

Kupitia taarifa iliyotumwa siku ya alhamisi ,Ikulu imesema kwamba rais alishuhudia hafla ya kuapishwa kwa Badi  kama inavyohitajika na wote wanaohudhuria mikutano ya baraza la mawaziri  au wanaoshughulika na tarataibu za   uendeshaji wa serikali .

Msemaji  wa Ikulu Kanze Dena amesema  kuanzia sasa Mkuu huyo wa NMS  atakuwa akihudhuria mikutano ya baraza la mawaziri na kamati zake  kwa mujibu wa agizo la rais la tatu la mwaka wa 2020 .

Hafla hiyo iliandaliwa alhamisi kabla ya mkutano wa baraza la mawaziri kufanyika

 

 

 

 

 

 

 

Uhuru anapaswa kuita kamati ya bunge,’ Hisia za Wakenya baada ya usemi wa Oscar Sudi

Baada ya mbunge wa Kapsaret Oscar Sudi kutoa matamshi yake ya kumsuta rais na familia wakenya wengi walitoa hisia tofauti kuhusu matamshi ya mbunge huyo.

Sudi alikuwa akizungumzia kukamatwa kwa mbunge wa Emurua Dikirr Johanna Ng’eno aliyekamatwa siku ya Jumatatu alasiri kuhusiana na madai ya kutoa matamshi ya chuki na kudhihaki rais Kenyatta.

Kupitia kwenye ukurasa wake wa facebook, Sudi alisema ya kwamba akina mama wote wanapaswa kupewa heshima.

Ruto ajitenga na matamshi ya Sudi na Johana Ng’eno waliomdhalilisha rais na familia yake

Hii ni baada ya naibu rais Ruto kujitenga na matamshi ya Sudi na Johana Ng’eno.

“Kwa kutoa ufafanuzi hapa, si kumtusi mama ya mtu nilirudia kwamba mama yangu, mama Ngina na akina mama wote wanstahili kupewa heshima

Hata hivyo mwenzangu Johana Ng’eno alikamatwa kwa kutaja jina lake mama Ngina, hamna mama wa mtu ambaye ni muhimu kuliko wa mwingine 

Hayo ndio maoni yangu.” Aliandika Sudi.

Ni ujumbe ambao uliibua hisia mseto na hata mjadala kwenye mitandao hiyo na hizi hapa baadhi ya hisia za wakenya;

Ushindi Wa Bwana: So now why was your good friend mentioning the president’s mother. Where did she come in. She’s not a politician.
Kimonyi Harun :Uhuru should simply call a parliamentary group meeting and cool down the ongoing temperatures,he is the party leader.
Hon Micah Rutto:Absolutely true, Uhuru is a Product of the same process as Sudi and everybody,mamake isn’t special than all other mothers, Kenya Sio Mali yake!!
Naeema Kuttuny:Sudi Respect all mothers you say?Sudi keep off my mother too she deserves the respect that you expect to be accorded your mother, remember the several times you mentioned her in your political quest!

 

‘Wengi wanasema kuna siri kati yangu na Uhuru ya kumtapeli Raila,’Ruto ajibu

Je kuna siri kati ya rais Uhuru Kenyatta na naibu wake William Ruto ya kumtapeli kinara wa NASA Raila Odinga? haya hapa majibu ya swali lenu ambalo naibu wake Uhuru aliweza kujibu akiwa kwnye mahojiano.

Huku akiwa kwenye mahojiano Ruto alikana kuwepo na siri kati yake na Rais Uhuru Kenyatta ya kumtapeli Raila Odinga kupitia hendisheki.

Ruto 1

Acheni kujipiga kifua! Ruto ajibu makombora ya mawaziri wanaomdunisha

“Kuna watu ambao huwa wanasema kuwa kuna siri kati yangu na rais kwanini tufanye hayo kama viongozi? Mungu ametupa uongozi na hatuwezi kuwa watapeli

Hiyo haitakuwa heshima kwa Mungu na wananchi wa kenya, sijawahi jihusisha kwa mambo kama hayo.” Ruto Alisema.

Ruto alidai kuwa maneno hayo yalisemwa na watu wa karibu sana na rais na wala si kutoka kwa mdomo wa rais Uhuru Kenyatta.

‘Ruto hayuko serikalini hahusishwi katika mikutano muhimu ,’Dennis Itumbi adai

rUTO t 1

“Watu hawa hawazungumzi wala kutoa matamshi hayo kwa niaba ya rais kwa maana na mjua vyema, si mtapeli wa siasa wala msaliti 

Hivi karibuni watu hawa wataachwa waende.”

‘Endeleeni kumuunga baba na Uhuru Kenyatta mkono,’ Sonko awaambia wananchi wa Kisumu

Hku akihudhuria mazishi ya mwendazake mwanakandanda Kevin Oliech ambaye alikuwa nduguye kiranja ya timu ya Harambee Stars Dennis Oliech ambaye aliaga dunia akiwa ujerumani akipokea matibabu ya saratani, hii leo Sonko aliwashukuru wakazi wa Kisumu kwa kumkaribisha na heshima kubwa.

Sonko kugharamia mazishi ya Kevin Oliech

Huku walinzi wake wakijaribu kutafuta njia katika ukumbi wa vijana wa eneo hilo, nguvu zao zilifua dafu baada ya vijana hao kusema gavana Mike Sonko awahotubia mwanzo ili aweze kuhudhuria mkutano wa mazishi ya mchezaji huo.

Sonko 1

Hakuwa na jambo la kufanya alifungua gari lake na kuwahotubia vijana hao, alipokuwa anazungumza aliwashauri wenyeji waweze kumuunga mkono rais Uhuru Kenyatta na Raila kwa umoja wa taifa.

“Watu wa Kisumu nina furaha kwa maana mmenikaribisha vyema humu, nataka kuwashauri na kuwaambia mwendelee kumuunga baba na rais Uhuru Kenyatta mkono

Kwa ajili ya umoja wa taifa letu.” Alisema Sonko.

Usikubali hawa ministers wakuharibie jina-Gavana Sonko amwambia Uhuru

Pia alizungumzia kutokuwa na kazi kwa vijana huku akisema handisheki ijayo itashughulikia shida hiyo.

“Najua vijana wengi huku kisumu hawana kazi, nawahakikishia kuwa serikali na hendisheki ijayo itashughulikia jambo hilo.”

Muda wa kafyu waongezwa kwa siku 30 huku kufungwa kwa mikahawa kukiongezwa muda wa saa moja

Rais Uhuru Kenyatta mnamo Jumatano, Agosti 26 alitangaza kuendelea kwa kafyu kwa siku zingine 30 katika harakati ya kudhibiti kusambaa kwa virusi vya corona.

Kwenye hotuba yake ya 11 kuhusiana na hali ya COVID-19 inchini akiwa Ikulu, rais alitangaza kuwa kafyu itaendela kaawaida ilivyotangazwa awali kuanzia saa tatu usiku hadi saa kumi asubuhi.

Uhuru

Uhuru pia alisema maeneo ya burudani ikiwemo baa yataendelea kufungwa kwa siku zingine 30 na watakaopatikana wakikiuka amri hiyo watakabiliwa kisheria.

Aidha alitangaza kuongeza muda wa kuhudumu kwa maeneo ya maankuli kwa saa moja na kuwaruhusu kusalia wazi hadi saa mbili usiku.

“Kufutiliwa mbali kwa kuuzwa kwa vileo katika mikahawa pia itaendelea kupigwa marufuku,mikahawa imeongezwa saa moja ya kufanya kazi kwa hivyo mikahawa itafungwa saa mbili.” Aliongea Uhuru.

Uhuru Kenyatta

Hii ni mara ya pili kwa kiongozi wa taifa kutangaza kufungwa kwa maeneo ya burudani ambapo alikuwa ametoa amri hiyo awali.

Tangazazo lake limewavunja mioyo baadhi ya wamiliki wa baa walikuwa na matumaini ya kufunguliwa kwa vilabu ikizingatiwa kwa visa vya COVID-19 vimepungua kwa siku za hivi punde.

Wakati wa kurekebisha katiba iwe bora ni sasa-Uhuru

Rais Uhuru Kenyatta amesema wakati umewadia wa kuorekjebisha katiba .Rais amesema licha ya katiba ya sasa kuwa bora mkuna umuhimu wa kuirekebisha katiba ili iweze kustahimili muda na changamoto zote zijazo .

Uhuru: Watu 5 wafariki huku 213 wakipatikana na covid 19

Rais Kenyatta amezitaja katiba za hapo awali kama zilzioundwa kuzuia ama kumaliza uhasama lakini haziwezi kutegemewa kuliboresha taifa asiku zijazo .

Katika kinachoonekana kama hatua ya kuwatayarisha wakenya kwa kura  ya maoni  kuhusu katiba mrais amesema katiba inafaa kuchukuliwa kama chombo cha kuboreshwa kwa lengo la kuimarisha  utawala na utoaji wa huduma kwa wakenya. Kuna mjadala kwa sasa kuhusu iwapo kura ya maonia kuirekebisha katiba inafaa kuandaliwa kwanza kabla ya uchaguzi .

viongozi wanaounga mkono mchakato wa BBi wamekuwa wakiitisha kuandaliwa kwa kura ya maoni kuirekebisha katiba huku wanaopinga mchakato huo wakikosoa pendekezo la kuirekebisha katiba . Katiba ya sasa imekuwa ikitumiwa kwa miaka kumi sasa tangu ilipoanza kutekelezwa mwaka wa 2010.

60% ya wakenya wanataka katiba kutekelezwa jinsi ilivyo- Infotrak

Wanaopinga kurekebishwa kwa katiba wanadai ni njama  ya kuanzisha mfumo wa utawala utakaoongeza nafasi za uongozi wa kurejesha tena nafasi ya waziri mkuu na manaibu wake .

 

 

Uhuru: Watu 5 wafariki huku 213 wakipatikana na covid 19

Rais Uhurukenyatta ametangaza kwamba visa vya covid 19 vimepungua nchini huku akisema watu 213 ndio waliopatikana na ugonjwa huo katika saa 24 zilizopita .idadi hiyo sasa inafikisha jumla ya visa hivyo nchini kuwa 33,016.

Rais Kenyatta amesema watu 5 wameaga dunia na kufikisha idadi ya walioaga dunia hadi sasa kuwa 564. Hata hivyo kuna habari njema baada ya watu 241 kupona na kufikisha jumla ya idadi ya waliopona kuwa 19 296.

Uhuru  amesema mengi zaidi yanafaa kufanywa ili kuthibiti maambukizi ya virusi hivyo ambayo sasa yamekita kambi katika kaunti na maeneo ya mashambani . Akilihutubia taifa rais alitangaza kuundwa kwa jopo maalum la Covid kujadili hatua za kuainisha mfumo wa huduma za afya katika kaunti na serikali kuu ili kuboresha sekta ya afya .