Kazi kwa Wazee : Kutana na maajuza wanaofanya kazi ya ukahaba Nyeri

Ungelidhani umeyaona na kuyasikia yote lakini makubwa na hata mazito zaidi yapo njiani. Awali ukahaba ulizingatiwa kuwa kazi ya  mabarobaro  lakini huko nyeri nyanya  wa umri wa juu pia sasa wanaiuza miili yao  na hawajutii uamuzi wao

‘Niliona chuma yake ya doshi nikazirai. Singewezana. ’ Kahaba asimulia mambo anayopitia katika kazi yake.

Wanawake hao wanaoshi katika eneo la Chaka  wametegemea kazi hiyo kama njia ya kujipa kipato  ili kujikimu na pia kuwasaidia wajukuu wao ambao waliachiwa na wanao. Wakizungumza katika mahojiano na Runinga ya Mt Kenya TV,  wanawake hao wamesema  kwamba hali ngumu ya  maisha imewalazimu kujiingiza katika biashara hiyo .

Esther  wanjiku  (sio jina lake halisi) hufanya kazi katika mgodi wa mawe lakini giza linapofunika ardhi basi kazi yake papo hapo inageuka na kuwa ya ukahaba. Nyokabi mwenye umri wa miaka  70 (sio jina lake halisi )  anasema licha  ya kazi hiyo kudharauliwa na wengi, imempa  mkate wake wa kila siku .

 HAPO AWALI NINGEJAZA LORI KWA MAWE  KWA WIKI MOJA NA NINGETUMIA NGUVU NYINGI. KWA SASA SINA NGUVU ZAIDI. KILA SIKU LAZIMA NINYWE  POMBE YA SHILINGI 50  KABLA YA  KWENDA NYUMBANI. NINA WATOTO WATANO NA BINTI YANGU ANA WATOTO WATATU

  Alivyoulizwa jinsi wanavyowashughulikia wateja wake, Nyokabi anasema;

 Mnaafikia makubaliano yatakayokuwezesha kupata  unga na pesa. Wakati mwingine anaweza kukupa hata shilingi 200 kwa sababu wengi pia hawana pesa nyingi.

Kabla ya kwenda kuwahudumia wateja wake, Nyokabi hupitia katika eneo la burudani ili kupata kileo cha ‘kumtuliza’ .

Juliah Wambui ( sio lake halisi )  pia anaishi Nyeri na amekuwa kahaba kwa miaka 20 .

Kulingana naye, yeye na wateja wake hawana pesa za kwenda kupata vyumba au danguro na hivyo basi wanamaliza shughuli zao katika vichaka au maeneo mengine ya wazi .

‘Niliacha ukahaba baada ya babangu kuja lodging’

 ‘ Mimi huwahudumia wanaume wa umri wangu. Tunatumia uwanja huu ambao upo mbali ili kupeuka kuonekana na watu. Wakati ninaposikizana na wateja wangu , siitishi pesa kanza, mimi huitisha bia kwanza hata hivyo nahakikisha kwamba silewi. Watu wengi hupenda kufanya mapenzi chini kwenye majani na mkimaliza shughuli zenu, kila mtu anaenda zake. Ninapofika nyumbani naoga  na kisha kutoka tena kumtafuta mteja mwingine .

Kazi ni kazi! Kutana na makahaba wajasiri wanaotengeza pesa mitandaoni(Picha)

Julia  anasema yeye hutumia kinga  kwani hataki kuambukizwa maradhi .

 Mimi hurejea katika eneo tofauti la burudani kutafuta mteja mwingine. Nahakikisha kwamba natumia mpira wa kondomu. Nina mipira ya kondomu katika nyumba yangu . Singependa kujua wajukuu wangu wajue ninafanya kazi gani. Wamejaribu kuniuliza mimi huenda wapi nyakati za usiku lakini Sijawaambia .

Kazi ni kazi! Kutana na makahaba wajasiri wanaotengeza pesa mitandaoni(Picha)

Ukahaba kama kazi nyingine zote umeathiriwa na Coronavirus.

Wanaofanya kazi hiyo wamekuwa wakipata ugumu  kupata wateja na wengi  wamejipeleka karantini kama ilivyoagizwa na serikali. Wengi wapo nyumbani wakihofia kuambukizwa virusi vya COVID 19. Lakini kuna baadhi yao ambao wanatengeza kiasi kikubwa cha mpunga kwa sababu ya ujanja wa kutumia mitandao kuwapata wateja.

‘Niliacha ukahaba baada ya babangu kuja lodging’

Kati ya maelfu wanaofanya kazi ya ukahaba ni wachache waliopata ujasiri wa kujitokeza wazi kusema kwamba hiyo ndio kazi wanayofanya ili kujikimu kimaisha. Wanapenda wanachofanya na hawafichi. Eddy aka mama G na Shiko Baibe  ndio walioweza kujitokeza wazi. Shiko,  alikulia katika mtaa wa ghetto huko Nyeri  na  alitaka kuwa daktari lakini mambo hayakumwendea vizuri na akajipata katika ukahaba.

kahaba 2

Amesema ;

AFTER COMPLETING FORM FOUR I HAD KIDS AND LIFE BECAME UNBEARABLE. MY FRIENDS INTRODUCED ME TO PROSTITUTION. I’M PROUD OF WHAT I DO.’ SHE SAID IN AN INTERVIEW WITH MASSAWE JAPANNI

‘Its over!’ Kipusa mkenya aachana mpenzi wake mzungu kwa hofu ya coronavirus

Mama G  anayetoka Kisumu  alitaka kuwa mwalimu lakini kwa sababu ya ukosefu wa kazi  aliamua kuuza mwili wake . Alipogundua kwamba yeye ni mpenzi wa jinsia moja alisema.

I USED TO BE ATTRACTED TO FELLOW MEN, THOUGH I HID IT BECAUSE OF MY BACKGROUND AS AN AFRICAN, MORE SO A KENYAN.

I DID THAT BUT IT REACHED A TIME THAT I COULD NO LONGER HIDE. I AM A SEX WORKER AND HAPPILY MARRIED WITH MY MAN IN THE HOUSE

kahaba 3

Kama tu  mtu yeyote mama G amesema alitafuta kazi na hakupata na hivyo basi hajutii kujiingiza katika kazi hiyo

LIKE ANY OTHER JOB, SEX WORK IS ALSO WORK. AS MAMA G, WHO EARNS A LIVING FROM SEX WORK, I TAKE IT SERIOUSLY, AND DESPITE PEOPLE GIVING ME OTHER OPTIONS, WHICH I DON’T TAKE BECAUSE I APPRECIATE MY WORK SO MUCH AND THEREFORE I SEARCHED FOR IT, KAZI HUTAFUTWA HAIKUTAFUTI. FOR THE PAST 10 YEARS, I HAVE BEEN A SEX WORKER AND GETTING MY EARNING FROM THAT. A GOOD EARNING, INDEED,’ HE SAID IN A PREVIOUS MEDA INTERVIEW.

‘Nililala na mamangu wa kambo kumuadhibu babangu’ Dunia ina mambo

Kwa sasa ukahaba sasa umekuwa digital na wengi wanapata wateja wao mitandaoni na kupitia applications za simu ambapo watu hukutana.

WE HAVE GAY SITES WHERE WE MEET OUR GAY CLIENTS AND WE ALSO HAVE GAY CLUBS,’ MAMA G REVEALED.

Baadhi ya makahaba wanaishi maisha ya kifahari  na iwapo hujui kazi wanazofanya unaweza  kufikiri  wanapokea mishahara mizito katika afisi za  makampuni mazito ya Kenya hii. Picha zifuatazo ni za Mama G ambaye anaweza kuwafedhehesha baadhi ya maslayqueens.

kahaba 4

 

kahaba 5

Mhariri: Davis Ojiambo

‘Niliacha ukahaba baada ya babangu kuja lodging’

Joy Ndirangu* alijipata katika hali  ambayo kamwe hakuna anayewahi kutamani kujipata . Mwanadada huyu mwenye umri wa miaka 32 amekuwa akifanya kazi ya ukahaba kwa miaka  9 , tangu alipomaliza shule ya upili . Anasema haikuwa kupenda kwake kujiiingiza katika kazi ya kuuza mwili wake lakini hali ya umaskini ,mateso ya kukosekana kwa kazi ndio baadhi ya sababi zilizomsukuma hadi akajipata katika biashara ya ukahaba hapa Nairobi .

Obama Girls! Malia na Sasha Obama sasa ni watu wazima-Tazama picha

Alipomaliza shule ya upili , Joy alikuja Nairobi kutafuta kazi kwa sababu wazazi wake huko Subukia ,Nakuru hawakuwa na pesa wala mipango ya kumpeleka katika chuo  chochote kwa mafunzo zaidi .Akija  Nairobi ,alikuwa  mwingi wa matumaini kwamba  angepata kazi ili arudi shule mwenyewe .Alianza kuishi na  jamaa yake mmoja maybe pia alikuwa mtu kutoka kwao Subukia .Bila kujua kazi ya huyo ‘shangazi’ yake ,Joy alijipata katika shimo ambalo hangeweza kujitoa .Jamaa yake huyo ambaye alimwita shangazi ingawaje uhusiano wao wa kifamilia ulikuwa wa mbali alikuwa  ‘madam’ –jina linaloitwa wanawake ambao huwaingiza wasichana katika ukahaba na kasha kuchukua kiasi cha fedha wanazolipwa wasichana hao katika kazi ya kujiuza.

‘Msijali kuhusu Bill’ ,Babu Owino aiambia familia ya DJ Evolve  

Alishangaa ni vipi shangazi yake alimudu kuishi katika nyumba nzuri  nay a gharam ya juu mtaani Highrise ingawa hakuwa na kazi maalum iliyojulikana .Kumbe alikuwa anampa tu Joy muda wa kuzoa jiji kabla ya kumwingiza kaika ukahaba Baada ya miezi miwili ,shangazi yake alimkalisha chini na kumuambia yote! Joy alishangaa  atafanya nini lakini hakuwa na chaguo jingine ila kukubali kufanya ukahaba  -na hapo safari yake katika biashara hiyo ya aibu ikaanza . Alijidanganya kila mara kwamba ataifanya muda tu kasha aiache na ajishughulishe na kitu kingine lakini anasema ukahaba ni kama uraibu .Wakati fulani hutaki kuacha kabisa kwa sababu ya mazoea na pia unapata uzoefu na wateka ambao pesa zao unazipata kama ada .

Sauti za  Ninga: Malkia wa Redio nchini Kenya .

Lakini kwa Joy mgutuko ulimjia siku moja akiwa katika  danguro alikokuwa akipiga shughuli yake akamwona mwanamme aliyevalia koti na mwenye umri wa juu kidogo akiingia katika sehemu ile .Kwa sababu ya giza na alivyokuwa mbali  hakuweza hasa kumjua kwa urahisi na kama kawaida yao,wanawake wote ambao walikuwa  nje ya lango walimkimbilia mzee Yule ili awachague wampe raha ya mwili usiku huo . Mzee alikuwa amevalia kofia iliyofunika sehemu kubwa ya uso wake na hivyo haikuwa rahisi kumtambua .Walipomfikia ,Joy alikuwa wa kwanza na mzee akamchagua yeye kama ambaye wataingia naye danguroni kwa  shughuli ya kufurahisha nyama za ‘kimwili’.

Uchawi?‘Niliambiwa nitayarishe uji wageni wanakuja,Kumbe ni Nyoka aliyefaa kunywa uji!’

Ole wake ! walipofika katika  cha ghorofa ya juu ,mzee aliitoa kofia yake na miwani .Joy alikuwa mbele yake na hivyo alianza kwa kutoa nguo yake ya juu kabla ya kuwasha taa.kulikuwa na mwanga kutoka dirishani lakini Mzee alipowasha taa ya chumba hicho ndipo  ulimwengu wake ukatikisika .

Heart-broken:Nilimpata girlfriend yangu na mwanamme mwingine siku ya Valentine!

Joy alionana macho kwa macho na babake mzazi .Muda wote wakiingia katika chumba kile mzee hakusema neon na abaada ya kumchagua Joy walianza kupandaa juu . Maskini  mzee alipoangaliwa kwa makini akagundua kwamba Yule kahaba aliyetaka kula uroda naye usiku ule alikuwa binti yake! Joy hakungoja kuitwa na babake ,alianza kutoka nje ya chumba kile akilia.Mzee hakusema lolote naye akaketi kitandani akizungumza lugha ya nyumbani pekee pale . Alivyoondoka pale ,Joy alikata kauli ya kutorejea kufanya tena kazi ya ukahaba . Baba na bintiye hawakuzungumziana kwa miaka takriban mitano iliyofuata na hakuna aliyesema jambo lolote kuhusu tukio hilo .

 

 

 

Ukahaba sio dhambi! Mahakama ya Nigeria yasema

Jaji wa mahakama kuu katika mji mkuu wa Nigeria, Abuja, amewapa wanawake elfu 16,000 za Nigeria (naira) au ($ 275) kila mmoja baada ya uamuzi kwamba kukamatwa kwao mwaka wa 2017 kulikuwa ni ukiukwaji wa haki yao ya faragha.

 

Hii ni sawa na jumla ya Sh444,000 kwa wanawake wote 16. Inaaminika kuwa wanawake hao walifungwa kwa sababu walishtumiwa kuwa makahaba.

Mahakamani, Babatunde Jacob ambaye ndiye alikuwa wakili wa wanawake hao, alisema kwamba kazi ya kufanya ukahabba haijawahi tambulika kama uhalifu, Nigeria.

Jacob also argued thatwas a violation of their “dignity… and right to private life”, a summary of the judgement says.

Jacob pia alisema kwamba “”the act of pulling down the doors of the applicants [and] indecently searching them was a violation of their dignity… and right to private life” , muhtasari wa uamuzi unasema.

Jaji Binta Nyako alisema haki za wanawake chini ya katiba zilikuwa zimekiukwa.

Katika utetezi wao, viongozi walidai kuwa wanawake hao walikuwa wamefungwa kizuizini baada ya kukiuka sehemu ya sheria ya mazingira ya Abuja, uamuzi unasema.

But Justice Nyako said constitutional rights overrode the local regulations.

She did not, however, specifically state that sex work was not a crime.

Lakini Jaji Nyako alisema haki za kikatiba zinapita zaidi ya kanuni za mitaa.
Hakusema, hata hivyo, kuwa  kazi ya ukahaba ni hatia.

 

 

Ethiopia wapanga mikakati ya kupiga marufuku ukahaba

Maafisa katika mji mkuu wa Ethiopia Adis Ababa wanaandaa mkakati kupiga marufuku ukahaba na kuombaomba wa mitaani , ikiwa ni hatua ya hivi karibuni katika msururu wa hatua za kusafisha sura ya taifa , imesema ofisi ya meya wa mji huo.

Muswada unaoonyesha sheria za marufuku hizo bado unakamilishwa.

Hata hivyo afisa wa habari wa Meya wa Mji wa Adis Ababa Feven Teshome, ameliambia shirika la habari la AFP amesema marufuku hizo ni muhimu ili kupambana na “matatizo ya kijamii ” katika mji huo wenye zaidi ya watu milioni moja.

” Tunakadiria kuwa kuna ombaomba 50,000 na zaidi ya makahaba 10,000 mjini Addis Ababa. Muswada wa sheria unalenga kumaliza matatizo haya ya kijamii ambayo pia yanaleta picha mbaya kwa Ethiopia,” anasema Feven.Mhandisi Takele Uma, Naibu Meya wajiji la Addis Ababa

Kazi ya ukahaba kwa sasa si uhalifu nchini Ethiopia, na Feven anasema pendekezo la kuipiga marufuku mjini Addis Ababa itawahusu tu ombaomba wanaozurura mitaani.

Hii ikimaanisha kuwa haiwezi kutekelezwa katika sehemu kama vile baa , maineo ya kusinga, nyumba za malazi na maeneo mengine ambapo shughuli za ukahaba huwa ni nyingi.

Wafanyabiashara ya ukahaba na wateja wao kwa pamoja watakabiliwa na adhabu ambayo inaweza kuwa ni kulipa faini au kufungwa jela kwa muda fulani anasema Feven.

Mnamo Mei, maafisa wa Ethiopia walitangaza sheria kuhusu matangazo ya biashara ya pombe kote nchini ambapo walipiga marufuku matangazo ya biashara ya pombe na sigara katika maeneo ya umma.

Sheria hiyo pia ilipiga marufuku mauazo ya pombe kwa mtu yeyote mwenye umri wa chini ya miaka 21.

-BBC

Hali ya umaskini yasababishia Ashley na Joyce kujitosa katika ukahaba

Katika kipindi cha Bustani La Massawe kitengo cha Ilikuaje, wageni katika studio walikuwa wawili Ashley na Joyce ambao wamekuwa katika uraibu wa ukahaba kwa muda mrefu. Wawili hawa wana sababu zao zilizowafanya wajitose katika kazi hii.

Soma mengine hapa:

PATANISHO: Atafute bibi mwingine kwani siwezi rudiana naye!

Ashley, 22, baada ya kumpoteza mama akiwa kidato cha pili alipata pigo la kimaisha na kujipata katika tandabelua huku akilelewa na baba wa kambo.

Baba huyu ndiye alimuingiza katika ukahaba. Kazi hii alikuwa anaifanya ili kumsitiri kakake mdogo pamoja na mahitaji yake ya kila siku.

“Nilipoteza mama nikiwa kidato cha pili miaka minne iliypita. Hapo nikaanza kujipata katika matatizo kidogo. Babangu wa kambo alinipeleka katika danguro ili niingize pato la kila siku.”

Binti hawa wanasimulia jinsi wanavyojipata katika matatizo kazini yao huku wakitaja wanapolisi kama changamoto kubwa. Hali kadhalika wameweza kufunguka jinsi wapo katika mahusiano na wanapotumia ujanja kuwafanya wanaume wao wasijue kazi wanayoifanya.

Pata uhondo hapa:

Former KU VC Olive Mugenda shows off daughter after graduating with PHD

Huwa wanapata kipigo kikali kutoka kwa wateja wao na wengine kukosa kuwalipa katika vyumba vya kukodi.

Joyce alianza ukahaba baada ya ufukara katika nyumba yao kukita mizizi.

Anasimulia kisa na ambapo alibakwa na marafiki wake wanne wakitoka shuleni na hapo akapata ujauzito.

“Nimelelewa na single mum na nyumbani tuko watoto watano. Mamangu anafanya kibarua na kuzungusha nguo. Ikafika kipindi tunatoka shuleni saa kumi na mbili mimi na marafiki zangu tukapatana na wanaume watano na wakatubaka na hapo nikapata mimba.”

Hatimaye wawili hawa wamejutia kuwa maisha yao yalizama katika usiku wa giza totoro na kutoa nasaha kwa wanadada wasiufuate mtindo huu.

Soma hadithi nyingine hapa:

This is why you should update your WhatsApp now!

Ilikuwaje: Mpenzi wangu alinivunja moyo na nikaamua kuwa kahaba – Jane Watiri

Leo studioni tulikuwa na Jane Watiri ambaye alikuwa kahaba kwa miaka saba lakini sasa amegeuza mienendo yake na kuwa mhubiri.

Watiri alifichua kuwa aliingizwa katika biashara ya ukahaba akiwa na umri mchanga na rafikiye wakati alipokosa namna ya maisha.

Hayo yalifanyika baada ya kupachikwa mimba akiwa na umri wa miaka kumi na saba, mimba ambayo baba mtoto aliikata na pia kumtenga.

Ilikuwaje: Caleb Onyango asimulia jinsi mkewe alipata ajali akiwa mja mzito

Rafiki aliyemwezesha kuingilia ukahaba alikuwa amemshinda ki umri kwani alikuwa na miaka 32, takriban mara dufu ya miaka yake Watiri.

 

Kulingana na Watiri, alifanya ukahaba kwa miaka saba huku akijaribu kuuponya moyo wake baada ya kuvunjwa na mpenzi wake.

jane watiri

Alieleza: Wakati nilijifungua mtoto nikiwa mchanga, baba mtoto alinikataa na nilikimbia Koinange kutafuta riziki na pia kuuponya moyo wangu.

Rafiki yangu mwenye umri mkuu kuniliko alinifunza kazi ya ukahaba nikiwa umri wa miaka 17.

Huyo rafiki yangu aliniambia kuwa atanipeleka kazi na wakati huo mtoto wangu alikuwa na mwaka mmoja unusu. Nilikuwa nampa dawa ya kulala na naenda ukahaba usiku mzima.

Mtoto wangu ilifikia mahali na mwili ukaanza kuzoea zile dawa na hapo mamangu alimkujia na kwenda naye nyumbani.

Hata hivyo, sahizi amebadilika na yeye ni mhubiri. Hata hivyo, Watiri amewashauri watu kuto wahakimu kahaba kwani kuna aina tatu ya ukahaba.

Moja ni ukahaba wa kujitakia, pili ni kahaba ambaye hataki kufanya kazi na anataka fedha na tatu ni kahaba ambaye amevunjwa moyo na mpenzi wake.

Ilikuwaje?: Tracy Wanjiru aelezea alivyonusurika kifo katika shambulizi la Westgate na DusitD2

 

Sahizi mimi ni mhubiri baada ya maisha ya ukahaba kwa miaka saba na nilikuwa natumia bangi. Kwa sasa siwezi ambia wasichana watumie bangi kwani haikubaliki hata kwa jamii.

Kuna kahaba mara tatu; Kuna ule wa kujitakia labda hataki kufanya kazi, kuna mwenye anaifanya kwa hiari yake na pia kuna mwenye amevunjwa moyo. Kwa hivyo ukiona kahaba usiwahi wahukumu.

jane watiri

Kazi ya ukahaba ina hatari mbali mbali kwani Watiri aliwahi lala korokoroni kwa mwezi mmoja baada ya kumuongelesha jaji vibaya.

Isitoshe, ashawahi patana na wateja ambao walitaka kumtumia kama dhabihu huku mwingine akitaka kumpiga risasi bila sababu. Lakini kwa bahati nzuri aliponea yote.

Niliwahi shikwa juu ya ukahaba na nikapelekwa kortini na kufungwa mwezi mmoja baada ya kumuongelesha jaji vibaya. Aliniuliza kama nilikuwa nafanya ukahaba nikamjibu ‘Kwani unaonaje?’.

Hapo akaniambia niende korokoroni ili nipate adabu kwani asiyefunzwa na mamaye hufunzwa na ulimwengu.

Akizungumzia kuhusu siku aliyoponea kutolewa kama dhabihu alisema.

Nishawahi patana na client akaniambia nimngoje afike up stairs, alirudi akasema miungu yake imekataa nitolewe kama dhabihu. Hapo nikajua kuwa kuna watu hukujia wanadada barabarani na kuwatoa kama dhabahu.

Pia nishawahi shikiwa bunduki Uhuru Highway na mteja wangu saa nane usiku. Jamaa alisema kuwa anajihisi kuniua na kilichoniokoa ni polisi fulani walikuja na hapo nikatoweka.

 

PATANISHO: Nilimuambia Mke Wangu Akafanye Ukahaba Na Babake

Bwana Mwaniki alituma ujumbe akiomba apatanishwe na mkewe baada ya kumkosea sana.

Akijitetea Mwaniki alidai, “Kuna wakati nilikuwa nimeenda kazi kisumu na usiku mmoja nikampigia simu na mwanamke mwingine ndiye alijibu, kumuuliza mke wangu yuko wapi yule mwanadada akadai amepigiwa simu na mwanaume mwingine na akaondoka. Kumpigia simu ile ingine hakushika na nikapandwa na hasira na kumuandikia ujumbe mbaya nikimuambia kama ameenda umalaya basi aende alale na babake.

Sasa siku tuliyozungumza akadai kuwa hiyo siku hakuwa amefunga kazi na alikuwa ametuma jamaa fulani ndio maana hakujibu simu zangu. Alisema.

Alipopigiwa simu mkewe alidai kuwa wawili hao wameishi wakigombana tangia mwaka wa 2013.

“Alinidanganya kuwa hakuwa ameoa lakini niligundua kuwa ameoa na ana watoto wanne na huyo mke anatambulika kwo nyumbani. Licha ya hayo yote bado alikana. Ya pili nikimpa fedha hudai zimepotea kwa benki eti hajui kwenye zilienda. kwenda kwa bank alikuwa na zaidi ya elfu sitini na hakulipia mtoto karo.

Dadangu alikuwa mgonjwa alikuwa amelazwa hospitalini na wakati mamangu alikuja kunitembelea huyu jamaa akanitusi mbele yao akidai aliniokota kama chokora. Hapo niliondoka kwani hana heshima hata kidogo.

Isitoshe alitumia dadangu ujumbe akidai mimi natembea na bwanake na kuwa nina virusi vya ukimwi.

Hiyo ni ngumu kumsamehe sijawahi mweleza babangu lakini nitamweleza na chenye babangu ataamua ni chake. ” Alijieleza mama Peter.

Pata uhondo kamili.

Makahaba Wanataka Kutambuliwa Na Serikali

picha: AFP | 

Makahaba wanataka kutambuliwa na serikali ili waruhisiwe kuendesha shughuli zao pasi kusumbuliwa kila mara.

Doty Agala kutoka muungano wa makahaba nchini anasema kwamba kazi yao ni kama tu kazi yoyote ile nchini Kenya na inafaa kuheshimiwa.

Ukahaba ni marufuku nchini na hii si mara ya kwanza kukuwa na muito wa kazi hiyo kuhalalishwa.

Katika mwaka wa 2012, aliyekuwa meya wa jiji la Nairobi wakati huo, George Aladwa, alipendekeza kupitishwa kwa sheria ambayo itahalalisha ukahaba katika jiji la Nairobi lakini hata hivyo juhudi hiyo ulipingwa vikali.

Sheria za ukahaba zinatofautiana kutoka kwa nchi moja hadi nyingine na baadhi ya nchi ambazo zimehalalisha ukahaba dunia ni Uholanzi, Ujerumani, Ugiriki, Benin, Armenia, Uingereza na Zambia.