"Hajui mtoto ako na miaka ngapi, anakula nini, anavaa nini!" Jamaa aanikwa na mzazi mwenzake

Franklin alisema mkewe aligura na kubeba vitu vya nyumba baada ya yeye kuenda kazi Machakos.

Muhtasari

•"Tulikuwa kwa ndoa miaka miwili. Nilikuwa naenda kazi Machakos, tukaanza mvurago kwa nyumba. Singekosa kuenda hiyo kazi," alisema.

•Phynis alipopigiwa simu alifichua kwamba mume huyo wa zamani hajakuwa akiwajibikia malezi ya mtoto wao.

Ghost na Gidi
Ghost na Gidi
Image: RADIO JAMBO

Katika kipindi cha Gidi na Ghost Asubuhi, kitengo cha Patanisho, Franklin Fedha Musoma alituma ujumbe akiomba kupatanishwa na aliyekuwa mke wake, Phynis ambaye alitengana naye takriban miaka mitatu iliyopita.

Franklin alisema mkewe aligura ndoa na kubeba vitu vya nyumba baada ya yeye kuenda kazi Machakos, hatua ambayo hakuifuhiya.

"Tulikuwa kwa ndoa miaka miwili. Nilikuwa naenda kazi Machakos, tukaanza mvurago kwa nyumba. Singekosa kuenda hiyo kazi," alisema.

Aliongeza, "Wakati nilipata pesa nilimtumia pesa za mahitaji na kodi. Baada ya kumtumia pesa, alizitumia kama nauli ya kuhama."

Franklin pia alifichua kuwa hapo awali alikuwa amezozana na mkewe baada ya kukosa kumpatia pesa za kutengeneza nywele.

"Tulikuwa tumevurugana kwa nyumba. Alikuwa anahitaji pesa za kuenda salon na sikuwa na pesa.Baada ya kuhama tulikuwa tunazungumza bila mimi kujua amehama. Wakati nilirudi Nairobi nikapata amehama," alisema.

Aidha, alidai kwamba amekuwa akizungumza na mzazi huyo mwenzake na hata alipanga kukutana na wazazi wake ila mpango huo ukakosa kufanikiwa. Alifichua kwamba mara ya mwisho kumuona Phynis ilikuwa 2020.

"Baada ya yeye kuhama, nilikuwa namtumia kile nilikuwa napata," alisema.

Phynis alipopigiwa simu alifichua kwamba mume huyo wa zamani hajakuwa akiwajibikia malezi ya mtoto wao.

"Huyo mtoto unajua anakula nini? ata unajua ako na miaka ngapi. Wewe ata hujui majukumu ya mtoto?" Phynis alimuuliza Franklin.

Franklin alijitetea kwamba amekuwa akifanya juhudi za kuwasiliana na Phynis ila hajafanikiwa kwa kuwa amemblock.

"Mimi nilikuwa nataka turudi pamoja tulee mtoto," alisema.

Phynis alisema, "Mimi sina shida. Bora atashughulikia mtoto. Ata hajui mtoto ako na miaka ngapi. Hajawahi kuona mtoto. Watu wake pia walikataa mtoto. Hata hawajui anakula nini na anavaa nini,"

Franklin ambaye alisikika kuridhika na matamshi ya mzazi huyo mwenzake alimhakikishia kuhusu upendo wake kwake na kuahidi kuwajibikia malezi ya mtoto wao.

"Nakupenda na ningependa turudi pamoja tulee mtoto. Nafurahi umenisikia na tumepatana," alisema.

Phynis alisema atafanya maamuzi yake baada ya Franklin kuwajibikia mtoto.