'Ninamshukuru Mungu kwa kunipa mama kama Zainab,'Mwanaisha Chidzuga afunguka kuhusu kifo cha mama yake

Muhtasari
  • Mwanaisha Chidzuga afunguka kuhusu kifo cha mama yake

Katika kitengo cha ilikuaje tulikuwa naye Mwanaisha Chidzuga ambaye kwa mara ya kwanza alifunguka kuhusu kifo cha mama yake kwa mara ya kwanza, mwezi mmoja baada ya kumpoteza.

  Mwanaisha alifichua kwamba kifo cha mama yake kilikuwa mshtuko kwa familia.

Wakati mama yake, Zainab Chidzuga alikufa, Mwanaisha alikuwa pamoja naye katika hospitali huko Nairobi.

"Nilikuwa pamoja naye katika hospitali wakati kila kitu kilifanyika. Tulikuwa tumezungumza siku moja kabla, kwa sababu ya hali yake hakuweza kusema mengi. Lakini popote alipo, yuko na amani hiyo ni muhimu zaidi," Mwanaisha alishiriki.

Mwandishi wa zamani pia alifichua kwamba mama yake alikuwa nguzo kali katika familia yake na mshauri wake binafsi.

"Kabla ya kufa, aliwaita watoto wake wote na wajukuu ndani ya nyumba. Alitupikia Pilau na Kaimati, tulikula chakula cha mchana pamoja," alikumbuka.

Mwanaisha ambaye alitangaza kujiunga na siasa alikuwa na haya ya kusema kuhusu sera zake.

Tazama video hii,akieleza kuhusu sera zake;