Sababu kuu ya kubadilisha jina la Yummy Mummy-Murigi Munyi aeleza

Muhtasari
  • Munyi anasema wakati huo alikuja na jina alikuwa akipitia matatizo ya uzazi
  • Murugi Munyi alishiriki kwamba ufichuzi uliofanywa na Edar Obare umeathiri ndoa yake wakati fulani
Murugi Munyi
Image: Mercy Mumo

Katika kirengo cha ilikuaje tulikuwa naye Mtayarishaji wa maudhui nchini Kenya Murugi Munyi almaarufu Yummy Mummyambaye ameeleza ni kwa nini alibadilisha majina yake ya mitandao ya kijamii.

Hapo awali, mama wa watoto watatu alitambuliwa kama Yummy Mummy.

"Kuwa na jina la Yummy Mummy kulikuwa kukizuia chapa ambazo zilitaka kufanya kazi nami."

Munyi anasema wakati huo alikuja na jina alikuwa akipitia matatizo ya uzazi.

"Nilikuwa nikipambana na umama. Mwanangu alikuwa na umri wa miaka 6 nilipopata mtoto wangu wa pili. Akina mama wanaweza kuwa wapweke kwa hivyo nilitaka kuona kama akina mama wengine walikuwa wakipitia hali hiyo hiyo.

Niliangalia kote lakini hapakuwa na waundaji wengi wa maudhui wanaounda vile. Nimebadilika, sasa mimi ni mwanamke ambaye nataka kuzungumza kuhusu ngono, vipindi nk," Alizungumza Munyi.

Murugi Munyi alishiriki kwamba ufichuzi uliofanywa na Edar Obare umeathiri ndoa yake wakati fulani.

"Kila mtu anajaribu kutafuta riziki. Sijawahi kukutana naye (Edgar) uso kwa uso. Baadhi ya watu wanakaa tu na kuamua kumchukia mtu

Mtazamo wangu binafsi ni kwamba kuna watu ambao anahisi kutoheshimiwa nao kwa sababu hawachukui simulizi yake. Hajawahi kuathiri biashara yangu wala maisha yangu."

Akiongeza;

"Wakati fulani hadithi huweka shinikizo kwenye ndoa yangu,Lakini kuishi maisha ya kijamii kunaweka familia yangu yote chini ya shinikizo. Katika mstari wowote wa kazi unapaswa kujitolea baadhi ya mambo.

Ili niweze kuishi maisha ninayoishi sina budi kujinyima uhuru wangu. Nilichojifunza kwenye mitandao ya kijamii ni kwamba watu watazungumza na kulala. Kitu kipya huja kila wakati."