Hisia za mwanawe seneta Gloria baada ya kufukuzwa bungeni

Gloria alifichua kwamba mwanawe hakumkejeli baada ya kufukuzwa na hakulichukulia kama jambo kubwa.

Muhtasari
  • HUku akizungumzia safari yake ya siasa alisema kwamba kila mtu anapojiunga na siasa anapaswa kuwa tayari kupoteza kila kitu
SENETA MTEULE GLORIA ORWOBA
Image: RADIOJAMBO

Seneta mteule Gloria Orwoba akiwa kwenye mahojiano na Radiojambo alifichua kwamba mwanawe alitazama alipofukuzwa kutoka bunge.

Gloria, aliingia seneti tarehe 14 mwezi huu akiwa amevalia nguo zilizo na "damu" hedhi kuteta usambazaji wa sodo za bila malipo kwa mtoto wa kike.

Ingawa haikuwa hedhi halisi, wengi walimuunga mkono huku wengine wakimshambulia vikali kuhusu kitendo hicho.

Seneta huyo ambaye alizungumzia familia yake alisema kwamba yeye ni mama wa mtoto mmoja ambaye ana umri wa miaka 15.

Gloria alifichua kwamba mwanawe hakumkejeli baada ya kufukuzwa  na hakulichukulia kama jambo kubwa.

"Mimi ni mwanamke, mama, mtetezi wa vijana, wanawake na mtu mwenye shauku sana katika maendeleo. Nina mtoto mvulana, ana miaka kumi na mitano. Huwa ananisaidia wakati mwingine na mitandao yangu ya kijamii. Hakuna mazungumzo ambayo sijafanya naye..

Niliporudi nyumbani baada ya kufukzwa bunge,nadhani alitazama kwenye televisheni aliniuliza kama sitawahi rudi bunge tena, na nikamjibu kwamba nitarejea bali nimefukuzwa hiyo siku kwa ajili ya hedhi

Aliniambia niende nibadilishe na nrudi, yaani hakuchukulia kama jambo zito kwake,"Alisema.

HUku akizungumzia safari yake ya siasa alisema kwamba kila mtu anapojiunga na siasa anapaswa kuwa tayari kupoteza kila kitu.

"Jitayarishe kupoteza kila kitu unapoingia kwenye siasa... Mimi nilinyanganywa cheo kama naibu mwenyekiti mahali kwa sababu nilipinga jambo fulani ambalo halikuwa zuri. Sina rafiki wa karibu seneti. Kuna watu tunaongea ndio. Pengine mimi ndiye mbaya

Ningependa kuwaambia watu tuache kujifanya eti hatujui kuwa akina mama hapata hedhi... Kabla seneti, nilikuwa ninafanyia facebook kazi kama mchambuzi wa deta, nilirudi Kenya 2009. Mshahara wangu wa kwanza kama seneta ulienda kwa madeni."