FAMILIA IPATE HAKI

DJ Fatxo aeleza sababu ya kutozungumza na mamake Jeff Mwathi baada ya kifo chake

"Sina pesa za kutoa hongo kwa serikali mimi!" alisema.

Muhtasari

•Mwanamuziki huyo alikanusha madai  kwamba alihusika na mauaji ya kijana huyo wa miaka 23.

•.″Tayari mitandao ya kijamii na  vyombo vya habari vimekwisha dhibitisha kuwa nilihusika katika tendo hilo,mamake na familia ni vigumu kuniamini kwamba sikuhusika.″ Fatxo alieleza.

DJ Fatxo ndani ya studio za Radio Jambo
Image: RADIO JAMBO

Lawrence Njuguna Wagura almaarufu DJ Fatxo ameeleza sababu zilichochangia asisemezane na mamake Jeff Mwathi baada ya kifo chake.

Katika kikao na Massawe Japanni kwenye Radio Jambo, msanii huyo alikanusha madai  kwamba alihusika na mauaji ya kijana huyo wa miaka 23.

Alipoulizwa kwa nini hakuzungumza na mama ya marehemu baada ya tukio hilo, alijibu kuwa tayari familia hiyo ilmhukumu na kuhitimisha alihusika na hivyo hakuna anachoweza kufanya kubadili mawazo yao

.″Tayari mitandao ya kijamii na  vyombo vya habari vimekwisha dhibitisha kuwa nilihusika katika tendo hilo,mamake na familia ni vigumu kuniamini kwamba sikuhusika.″ Fatxo alieleza.

Aliendelea na kukiri kwamba,hamjui yeyote katika serikali ndipo ibainike kuwa alitoa hongo ili kesi yake itupiliwe mbali.

″ Mimi sina pesa sinazoweza kutoa hongo,nakaa katika nyumba ya kukodisha na gari langu bado sijamaliza kulipia.Iwapo serikali inamkamata Ezekiel mimi ni nani nisikamatwe?″

Mamake Jeff kwa upande wake alidai kuwa, haki haikufanyika huku akiweka wazi hakuwa na maneno ya kumwambia DJ Faxto. ″Aliiba mtoto wangu kwa nyumba akamwita akaenda naye.Nina kila kitu cha kuthibitsha hilo. Ninachoomba serikali ni kutekeleza haki na wala si kufunika maovu.″ Ann Wacuka,mamake Jeff kwa njia ya simu.

″Walishinda naye mchana mzima.Kama ni kujitoa uhai angejitolea kwao.Iweje alipoondoka naye ndio hiyo siku ya kifo chake?″Mnyonge hana haki hii dunia lakini damu ya mwanangu itakuja kuwahukumu maana kwa Mungu hakuna hongo.″ Ann aliendelea kusimulia kwa ghadhabu na huzuni.