Patanisho: Mwanadada agura ndoa baada ya mumewe kutafutiwa mke mwingine na dadake

Muhtasari

•Sharon alisema ndoa yao ya miaka minne alivunjika mwezi Aprili baada ya mumewe kutafutiwa mke mwingine na dadake.

•Sharon alieleza kwamba alishindwa kurudi kwa Abraham kama alivyokuwa ameahidi kwa kukosa nauli.

Ghost na Gidi
Ghost na Gidi
Image: RADIO JAMBO
Ghost na Gidi
Ghost na Gidi
Image: RADIO JAMBO

Katika kipindi cha Gidi na Ghost Asubuhi, kitengo cha Patanisho, Sharon Chepkosgei alituma ujumbe akiomba kupatanishwa na mume wake Abraham Kipkemboi.

Sharon alisema ndoa yao ya miaka minne alivunjika mwezi Aprili baada ya mumewe kutafutiwa mke mwingine na dadake.

"Nilikuwa nimeolewa kwa miaka minne. Ilifika mahali dada ya mume wangu akamletea mke mwingine. Hatukuwa tumefanikiwa kupata mtoto. Mimi nilikasirika na nikatoka nikaenda," Sharon alisema.

Mwanadada huyo alisema angependa kurudi kwa ndoa yake kwani fununu zilizomfikia ziliarifu kuwa mumewe tayari alimfukuza mke ambaye alikuwa ametafutiwa.

"Mume wangu aliniambia niende, nilimwambia nitarudi mwezi wa sita. Saa hii nampigia simu hashiki," Alisema

Sharon alieleza kwamba alishindwa kurudi kwa Abraham kama alivyokuwa ameahidi kwa kukosa nauli.

"Nilimwambia sina fare akasema nishinde hapo!"

Abraham alipopigiwa simu alisema kwamba tayari alikuwa amefanya juhudi  za kumfikia mkewe kwa simu ila hakushika.

Pia alifichua kuwa tayari alikuwa ametuma bodaboda kumchukua mkewe ila mkewe akadai kwamba ako na wageni.

Hata hivyo alikubali mkewe arudi nyumbani huku akiahidi kuwa angetuma pikipiki kumchukua baadae.

"Mi nakupenda sana. Uanze kupanga vitu vyako sasa nitatuma bodaboda"