Patanisho: Jamaa ampa mkewe miaka 3 ya kubadilika baada ya kukiri kutoka nje ya ndoa

Achieng alisema aligura ndoa yao ya miaka saba baada ya kutofautiana na mama mkwe wake.

Muhtasari

•Betty Achieng alisema aligura ndoa yao ya miaka saba baada ya kutofautiana na mama mkwe wake.

•Achieng alijitetea kwa kusema kuwa yuko tayari kurekebisha tabia zake pamoja na marafiki ambao walikuwa wakimpotosha.

Ghost na Gidi
Ghost na Gidi
Image: RADIO JAMBO

Betty Achieng alituma ujumbe akiomba kupatanishwa na mume wake Josphat Muima ambaye aliachana naye mapema mwaka huu.

Achieng alisema aligura ndoa yao ya miaka saba baada ya kutofautiana na mama mkwe wake.

"Mimi nilikuwa naishi nyumbani na mama mkwe naye mume wangu alikuwa akiishi mjini. Kuna kijana ambaye mama mkwe alikuwa anasema ni rafiki yangu. Niliposikia hivo ndio nikaanza kugombana naye," Alisema.

"Bwanangu alisema ati babangu alimtusi. Aliniambia nishughulike na maisha yangu,"

Achieng alidai kuwa tayari  amefanya amani na mama mkwe wake na amemhakikishia kuwa yupo tayari kumsamehe. 

Alisema angependa kurudi kwa ndoa yake kwa kuwa anatazamia kuendelea kuishi karibu na watoto wao wawili kama alivyokuwa amezoea.

Josphat alipopigiwa simu alisita kukubali msamaha wa mkewe na kusisitiza kuwa alikuwa akienda nje ya ndoa.

"Ni ngumu sana kumsamehe. Vitu alinifanyia ni mingi!" Josphat alisema.

Aliongeza "Mimi nilikuwa mbali na yeye. Wakati nilikuwa mbali ndio vituko hivyo vilikuwa vinafanyika nyumbani. Ripoti iko hata kwa chief. Niliona nimsamehe tukakuja naye huku. Baadae nilimpata na mtu ambaye nilijua. Nilipata thibitisho kwa simu,"

Achieng alijitetea kwa kusema kuwa yuko tayari kurekebisha tabia zake pamoja na marafiki ambao walikuwa wakimpotosha.

"Nilikwambia nitabadilika. Nitabadilisha marafiki ambao nilikuwa nao. Nisamehe mimi sitawahi kurudia tena. Nilikuwa mzuri alafu kuna rafiki yangu alifanya nianze hayo mambo. Alikuwa ni mama mkubwa," Achieng alijitetea

Josphat alisema, "Nilimpatia nafasi ya mwisho na nikamtazama kwa umakini. Hakubadilika. Yeye aendelee na maisha yake. Hiyo maisha ni ngumu juu mimi nishamove on."

Josphat alisema kuwa yuko tayari kumpatia mkewe miaka mitatu ya kurekebisha tabia zake.

 "Aendelee na maisha yake, ajaribu bahati yake tu" Alisema.

Juhudi za kuwapatanisha wawili hao hazikufua dafu.