Patanisho: "Unajisikia lollipop unyonywe na nani!" Gidi amsuta jamaa baada ya kuwa mgumu

Kelvin alisema anahitaji muda wa takriban miezi minane kabla ya kufanya maamuzi.

Muhtasari

•Eunice alisema kuwa ndoa yake  ya mwaka mmoja ilisambaratika takriban wiki mbili zilizopita kufuatia mzozo wa kinyumbani.

•Kelvin alipopigiwa simu alikiri kuwa mpenziwe hakuwa amemkosea kwa njia yoyote ile. 

Katika kipindi cha Gidi na Ghost asubuhi kitengo cha Patanisho, Eunice alituma ujumbe akiomba kupatanishwa na mpenzi wake Kelvin.

Eunice alisema kuwa ndoa yake  ya mwaka mmoja ilisambaratika takriban wiki mbili zilizopita kufuatia mzozo wa kinyumbani.

"Tuliachana na yeye kwa sababu kila saa alikuwa na wanawake. Nikimwambia hakutaka kunisikia," alieleza.

Alidokeza kuwa ndoa yao haijakuwa imara kwa muda mrefu kwani wamekuwa wakizozana kuhusu tabia ya mpenziwe ya kuenda nje ya ndoa.

"Tulikuwa tumekosana alafu tukarudiana. Tuliporudiana, niliona ni kama hakuwa amebadilisha tabia zake. Ilifika mahali nikaenda nyumbani. Tulirudiana tena lakini hali haikuwa nzuri," alisimulia.

Eunice alisema wakati akiwa nyumbani kwao aliona mpenziwe akiwa amepakia picha ya mwanamke mwingine kwenye Facebook na kuchukua hatua ya kumhoji kuhusiana na hilo ila mzozo zaidi ukatimbuka na kuongeza tofauti zao.

"Nilipata amepost msichana Facebook. Kumuuliza tukakosana alafu baadae kila mtu akaenda njia zake. Nilikuwa nampenda sana," alisema.

Alisema angependa kurejesha mahusiano yake na Kelvin kwa sababu kando na kuwa bado anampenda, pia alimhakikishia kuwa amebadili tabia zake.

Kelvin alipopigiwa simu alikiri kuwa mpenziwe hakuwa amemkosea kwa njia yoyote ile. 

Hata hivyo alisema anahitaji muda wa kufikiria kabla ya kufanya maamuzi kuhusu suala la kurudiana.

"Mimi niliamua nikae kwanza nifikirie hayo maneno wakati roho yangu itatulia itakuwa sawa. Utanipea muda wa kufikiria. Niko na mawazo mengi sana," alimwambia Eunice.

Alibainisha kuwa anahitaji muda wa takriban miezi minane kabla ya kufanya maamuzi.

Huku akiingilia kati, Gidi alikosoa madai ya Kelvin na kumwagiza awe wazi. 

"Unajiskia lolipop unyonywe na nani!" alimuuliza

Kelvin alijibu "Kusema ukweli nilishamsamehe. Kama anataka kuendelea na maisha yake yeye aendelee!" 

Baada ya kuonekana wazi kuwa uwezekana wa wawili hao kupatana ni finyu mno walianza kushambulia kwa maneno huku kila nnoja akiapa kuenda njia zake na kuendelea na maisha yao bila mwingine.

"Ukiniona kwa barabara pita tu! ata usinisalimie. Hao wanawake wako chukua mmoja uoe. Na ukiniona kwa barabara usifanye chochote," Eunice alimwambia Kelvin. 

Aliendelea "Kama umemove ata mimi nimemove. Nimeanza saa hii. Niko huru!"

Kelvin hakupinga uamuzi wa Eunice kwani ata yeye alisikika tayari kusonga mbele na maisha yake.