Patanisho:Jamaa aachwa kwa kuchunguza simu ya mkewe, kupata anachat na wanaume wengi

"Nimeanza kujuta, ata nikirudiana na yeye siwezi kurudia," Patrick alisema.

Muhtasari

•Patrick alikiri kwamba mkewe alitoroka baada ya yeye kuchokora simu yake na kupata anazungumza na wanaume wengine wengi.

•Huku akijitetea, Patrick aliweka wazi kwamba anajuta mambo ambayo alimtendea mke huyo wake wa zamani.

ndani ya studio za Radio Jambo.
Mtangazaji Jacob Ghost Mulee ndani ya studio za Radio Jambo.

Katika kitengo cha Patanisho, Patrick alituma ujumbe akiomba kupatanishwa na aliyekuwa mke wake Lilian.

Patrick alisema kuwa ndoa yao ya miaka minne ilisambaratika mwaka wa 2019 baada ya kuanza kumshtumu mkewe kwa kuwa na mipango ya kando. Kufikia wakati huo walikuwa wamebarikiwa na mtoto mmoja pamoja.

Alikiri kwamba mkewe alitoroka baada ya yeye kuchokora simu yake na kupata anazungumza na wanaume wengine wengi.

Lilian alipopigiwa simu aliweka wazi kwamba hayuko tayari kuzungumza naye na kutatua mzozo wao.

Mwanadada huyo alibainishwa kwamba hakufurahishwa na mambo mabaya ambayo Patrick alimtendea wakati wa kutengana kwao huku akitupilia mbali madai kwamba alikuwa na mipango ya kando.

"Kuna vile tulikuwa kwa mahusiano. Kweli kuna watu nilikuwa naongea na wao. Lakini ni watu wa kazi," Lilian alisimulia.

Aliongeza, "Alifikiria ni wapenzi wangu wengine. Nilimuonya na nikamwambia ni wateja. Nikifika kwa nyumba anataka kuchukua simu yangu ananichunguza. Ilifika mahali akanipiga, sikuwa namkosea."

Huku akijitetea, Patrick aliweka wazi kwamba anajuta mambo ambayo alimtendea mke huyo wake wa zamani.

"Nimeanza kujuta, ata nikirudiana na yeye siwezi kurudia," alisema

Lilian hata hivyo alimbainishia kwamba tayari amesonga mbali na maisha yake na kupata mpenzi mwingine.

"Nilishagive up na wewe, nilishapata mwingine. Nafasi yako nishapatia mwingine," alisema.

Kufuatia hayo, Patrick alidai kwamba pia yeye atatafuta mke mwingine.

Lilian aliunga mkono uamuzi wa mpenzi huyo wake wa zamani na akampa ushauri kuhusu jinsi ya kuishi vizuri na mpenziwe mpya.

"Ukipata msichana mwingine usishike simu yake. Mtu akikupenda ameshakupenda,"