Patanisho: Mwanadada mjamzito ampa mumewe na mama mkwe kipigo cha mbwa baada ya ugomvi

Sylvia alikuwa na ujauzito wa miezi saba alipomfungia mama mkwe wake kwa nyumba na kumpiga.

Muhtasari

•Mwanadada huyo alisema uhusiano wake na mama mkwe ulisambaratika mwezi Julai mwaka jana baada ya kumpiga.

•"Mtoto anashinda akilia kila mara. Nikienda hospitali wanasema hana ugonjwa. Halali anashinda tu akilia," Syvia alimwambia mama mkwe.

Gidi na Ghost
Gidi na Ghost
Image: RADIO JAMBO

Sylvia ,23, alituma ujumbe akiomba kupatanishwa na mama mkwe wake Bi Ruth ,58, ambaye alikosana naye mwaka jana.

Mwanadada huyo alisema uhusiano wake na mama mkwe ulisambaratika mwezi Julai mwaka jana baada ya kumpiga.

"Tulikuwa tumekosana na bwanangu alafu akanichapa. Tulianza kuzozana alafu mama mkwe akakuja. Mama mkwe alichukua mti kunichapa alafu nikainama ikapita. Niliaamua pia mimi kumchapa. Baadaye nikamfukuza mpaka kwake alafu tukajifungia kwa nyumba yake tukapigana," Sylvia alisimulia.

Slvia alisema baadaye wazazi na ndugu zake waliitwa ambapo walishiriki mazungumzo kabla ya kuandamana nao hadi kwao.

"Dada zangu walikuja wakanichukua... Baadaye wakati nilipeleka mtoto kwa mama mkwe, hata hakutaka kumnyoa.  Bwanangu anataka nirudi lakini siwezi kwa sababu mama mkwe hatuelewani naye," alisema.

Aidha, alifichua kuwa mtoto wake amekuwa akilia sana bila sababu na madaktari wamemshauri ampeleke kwa wakwe zake.

Bi Ruth alipopigiwa simu, Sylvia alitumia fursa hiyo kumuomba msamaha kwa makosa yake ya awali.

"Mama, nilikuwa nasema nimekosa sana. Mtoto analia sana nashindwa nitamleta nyumbani vipi. Naomba unisamehe ndio niweze kurudi nyumbani kwa amani," Slvia alimwambia mama mkwe wake.

Bi Ruth hata hivyo alimjibu, "Msamaha huombwa kwa kanisa kama tuko wote mbele ya wazazi wote. Msamaha sijakataa. Lakini wewe ulirudi na tena hiyo kitendo ukarudia. Hii msamaha utaishi kurudia?"

Sylvia aliendelea kujitetea kwa mama mkwe huyo wake huku akimweleza jinsi anavyohangaika kumtafutia mwanawe matibabu.

"Mtoto anashinda akilia kila mara. Nikienda hospitali wanasema hana ugonjwa. Halali anashinda tu akilia," alisema.

Bi Ruth alimuonya mkaza mwana huyo wake dhidi ya kumuita mtoto wao jina la mtu aliyeaga dunia. Alibainisha kuwa Sylvia alishirikiana na mumewe kumpatia jina mtoto wao.

"Msichana tulikuwa tumekubali vizuri lakini tabia ilitushinda. Huyu msichana alienda kwenye mtoto wangu ako, wakavurugana mpaka akambebea kisu. Akigombana na mume wake kidogo tu anamrushia kisu. Amefanya kivyo kama mara tatu nne hivi.  Alinipiga mpaka nikaenda x-ray ikanikula 1,500. Kama ni msamaha kwa ajili ya mtoto nimemsamehea lakini siwezi kukaa na Sylvia. Mtoto mahali anakaa aniletee," Bi Ruth alisema.

Sylvia alibainisha kwamba hakutaka kurudi ila alitaka tu msamaha wa mama mkwe na suluhu kuhusu malezi ya mtoto.

Mama mkwe alimjibu, "Hiyo sijakataa. Bado ni mchanga. Ata angekuwa anakaa ningemchukua nimlee. Bado anahitaji mama yake. Wakati alikuja kwa boma nilifurahi sana nilidhani mtoto wangu ameangukia. Lakini watu wanasema usione sura ya mtu ukafurahi kabla ya kuona tabia..Sylvia ni mrembo lakini tabia."

Bi Ruth alimshauri mzazi mwenza huyo wa mwanawe kumtafuta mumewe ili waweze kupanga mambo ya malezi.

Je, una ushauri gani kwa Sylvia?