Patanisho: Mama amshinikiza mwanawe kumtema mpenzi wake kwa kuwa ni yatima

Kagendo alisema mpenziwe alimwambia amepata mpenzi mwingine na mara moja akablock namba yake.

Muhtasari

•Kagendo alidai kwamba mama mkwe alimshinikiza Erick kumtema akimwambia kuwa familia yao ni maskini.

•Kagendo alisisitiza kuwa Erick bado yuko single kwani rafiki yake alimuarifu kuwa hajaonekana na mtu.

GHOST NA GIDI STUDIONI
GHOST NA GIDI STUDIONI GHOST NA GIDI STUDIONI
Image: RADIO JAMBO

Caudisia Kagendo ,23,  kutoka Embu alituma ujumbe akiomba kupatanishwa na mpenzi wake Eric Mwaniki ,28, ambaye alikosana naye mwaka jana kutokana na hatua ya mama mkwe kuingilia ndoa yao.

Kagendo alidai kwamba mama mkwe alimshinikiza Erick kumtema akimwambia kuwa familia yao ni maskini.

"Mwaka jana tulikuwa tunaishi na Erick. Mamake alikuwa anaingilia ndoa yetu . Alimwambia Erick ati mimi ni maskini ati nimeleta shida kwao kwa kuwa mimi ni yatima. Erick alianza kunidharau, nilisikia nimekata moyo kabisa. Baadaye nikaitwa na binamu yangu jijini Nairobi nikaenda," alisimulia.

Aliongeza, "Erick alianza kuniambia ati anataka kuoa ako na mpenzi mahali. Nikamwambia sio eti tuliachana tunaweza kurudiana. Tulikuwa tunaongea na rafiki yangu ananiambia mamake alisema nisiwahi kukanyaga kwa hiyo boma ati kijana wake atapata mpenzi ambaye ako na wazazi. Nilikuwa najaribu kumdanganya vile atakuja Nairobi. Akaniambia ati amepata mpenzi anataka kuoa."

Kagendo alisema kuwa mpenzi huyo wake alimwambia amepata mpenzi mwingine na mara moja akablock namba yake.

Hata hivyo, alisisitiza kuwa Erick bado yuko single kwani rafiki yake alimuarifu kuwa hajaonekana na mtu.

"Rafiki yangu jirani aliniambia Erick bado hajaoa. Ati anamuonanga huko lakini hajawahi kumuona na mtu.

Mama yake siwezi kuzungumza naye kwa sababu ndiye alikuwa anachochea tuachane. Baba yake hayuko sawa, huyo ndiye ningeongea na yeye," alisema.

Juhudi za kuwapatanisha wawili hao ziligonga mwamba kwani simu ya Erick haikuingia licha ya Gidi kujaribu mara kadhaa.

Kagendo alipopewa nafasi ya kumuongelesha mpenziwe hewani alisema, "Nampenda kama mume wangu na ningependa turudiane."