“Bwanangu akininunulia nguo anataka, akinipeleka salon anataka pia” Mwanadada amlalamikia mama mkwewe

Maureen aliliamika kwamba mama mkwewe alikuwa akimpuuza kila mara kutokana na uadui mkubwa baina yao.

Muhtasari

•Douglas alisema kuwa mke wake aligura ya ndoa yao ya miaka 3 baada ya kutofautiana naye kuhusu kula nyumbani kwa mama yake.

•Maureen alipopigiwa simu alidai kwamba mama mkwe wake huwa ana wivu na alikuwa akizua migogoro kila kukicha. 

GHOST NA GIDI STUDIONI
GHOST NA GIDI STUDIONI GHOST NA GIDI STUDIONI
Image: RADIO JAMBO

Douglas Wamocha ,30, kutoka Bungoma alituma ujumbe akiomba kupatanishwa na mke wake Maureen ,25, ambaye alikosana naye hivi majuzi.

Douglas alisema kuwa mke wake aligura ya ndoa yao ya miaka 3 baada ya kutofautiana naye kuhusu kula nyumbani kwa mama yake. Alisema mkewe hakupenda kitendo chake cha kula nyumbani kwa mama yake na hivyo akamtukana kwa hilo ambapo baadaye mamake alimtuma aende kumwonya.

"Tulikuwa tumekaa miaka mitatu. Tulivurugana na yeye kwa sababu nikiwa katika kazi yangu ya boda wakati mwingine nilikuwa napitia kwa mama yangu napata amepika nakula. Nikienda kwangu nikule kidogo anazusha anauliza nilikula wapi kwa sababu sikuli. Alienda akatusi mama juu ya kula kwake. Mama akaniambia nimuonye. Kufuatia hayo hasira ilinitokea nikampiga akaenda," Douglas alisema.

Alieleza, "Wakati mwingine hakuwangi, napitia kwa mama namwambia niko njaa ananiambia kuna chakula nachukua nakula. Alienda akapigia mama kelele. Nikaenda kumuonya pia mimi akanipigia kelele."

Alisema Maureen alitoroka na kumuacha nyuma mtoto wao wa miaka miwili kufuatia kichapo alichompa.

Maureen alipopigiwa simu alidai kwamba mama mkwe wake huwa ana wivu na alikuwa akizua migogoro kila kukicha. Alidai kwamba  mamake Douglas alikuwa akitaka kila kitu ambacho mumewe alimnunulia.

"Huyo mwanaume nilikaa na yeye miaka miwili. Tukazaa na yeye mtoto. Shida yake ni kunichapa kila siku. Alafu mama yake alikuwa analeta mabishano kwa hiyo nyumba. Bwanangu akininiunulia nguo, pia yeye anataka. Nikienda salon pia yeye anataka kuenda. Nikauliza mzee tutaishi vipi kama mamake anafanya hivyo," alisema.

Aliliamika kwamba mama mkwewe alikuwa akimpuuza kila mara kutokana na uadui mkubwa baina yao.

"Ikawa mama hawezi kunisalimia, anasalimia kijana yake lakini mimi hanisalimii. Ilifika mahali nikasema ni kama siwezani ikabidi nitoke. Mimi najua mama yake hanipendi na ndio maana hakutaka nipikie mwanawe," alisema.

Douglas hata hivyo alikiri kwamba anajuta makosa yake na kuahidi kubadilika.

"Najua mahali nilikosea. Najua makosa yangu. Nimejua makosa siwezi kurudia," alisema.

Maureen alisema, "Mtoto nilimuachia mama yako. Ishi na mama yako na mtoto wako. Hiyo boma mlikuwa mnanitesa sana. Ukininunulia nguo pia mama yako anataka. Kama nitarudi lazima tuhame. Mama yako hataki mimi nipike akule, anataka yeye akule.

Douglas alikubali kuzungumza na mama yake kuhusu uhusiano wake na mkewe na kutafuta suluhu kuhusu mzozo wao.

Maureen alikubali kurudi na kumwambia Douglas amtumie nauli mwezi ujao ila akamwagia abadilishe tabia zake.