Patanisho: Jamaa aachwa kwa madai alishinda bet, akanunua pikipiki na kutorokea Uganda

"Hatuko pamoja. Nilimwambia kitambo. Nilimove on kitambo," Brenda alisema.

Muhtasari

•Wanyonyi alisema mipango yao ya ndoa ilisambaratika mwaka wa 2020 baada ya Brenda kukubali shinikizo la fitina za watu.

•"Alikuwa ananidouble deal nikaamua kumove on. Kuna dame alikuwa anaitwa Sharon alikuwa naye," Brenda alisema.

Gidi na Ghost
Gidi na Ghost
Image: RADIO JAMBO

Oliver Wanyonyi ,22, kutoka Bungoma alituma ujumbe akiomba kupatanishwa na mchumba wake Brenda Wanyonyi mwenye umri wa miaka 20.

Wanyonyi alisema mipango yao ya ndoa ilisambaratika mwaka wa 2020 baada ya Brenda kukubali shinikizo la fitina za watu.

"Ilikuwa mwezi wa nane mwaka wa 2020 nilienda Uganda kwa ajili ya kazi. Kuna jirani alienda kwa Brenda akamwambia kwamba nilishinda pesa ya betting. Alisema nilihepa nikaenda Uganda na kununua pikipiki ndiyo aendesha huko. Mimi sikushinda pesa zozote, nilienda kwa sababu ya kazi," Wanyonyi alisema.

Aliongeza, "Disemba 2020 nilipanga tukutane mpakani. Ilikuwa wakati wa Corona singeruhusiwa kuingia Kenya... Ilipofika mwaka wa 2021 nilienda kwa kina Brenda na hata hakunisalimia. Hapo mzozo ukaanza."

Wanyonyi alisema amekuwa akiwasiliana na Brenda kwa simu ila mazungumzo yao tangu wakosane hayajakuwa mazuri.

"Tulionana mara ya mwisho Desemba. Yeye aliniambia ako kazi," alisema.

Wanyonyi alidokeza kuwa hapo awali aliwahi kumshuku mchumba wake kuwa na mwanaume mwingine.

"Kuna namba ilikuwa kwa simu yake. Kuna siku hiyo namba ilipiga tukiwa pamoja hasira ikanipanda nikavunja line yake," alisema.

Brenda alipopigiwa simu aliweka wazi kuwa tayari amesonga mbele na maisha yake na hakuna uwezekano wa kurudiana na Wanyonyi.

"Hatuko pamoja. Nilimwambia kitambo. Nilimove on kitambo," alisema.

Brenda alipoulizwa ikiwa ni kweli alisikiliza fitina za watu alisema, "Ilikuwa hivyo ikabidi nimemove on. Alikuwa ananidouble deal nikaamua kumove on. Kuna dame alikuwa anaitwa Sharon alikuwa naye."

Wanyonyi ambaye alisikika kuvunjwa moyo na hatua ya Brenda alimwambia, "Ni vizuri kuwa unachunguza kwanza. Huwezi kusikiliza maneno ya watu alafu unachukua hatua."

Je, ungemshauri Wanyonyi vipi?