KITENGO CHA PATANISHO

Patanisho: Jamaa watupiana cheche za matusi na mpenziwe, alia kaachwa

Joanes alisema kwamba mpenziwe Elizabeth alimwambia amoe mamake, .

Muhtasari

• Hatuwezi rudiana juu aliniambia niende niamshe babangu kwa kaburi anioe, mwambie babangu bado hajafufuka ili turudiane,, mwambie ni hadi babangu afufuke ndio nitarudi.

 

GHOST NA GIDI STUDIONI
GHOST NA GIDI STUDIONI GHOST NA GIDI STUDIONI
Image: RADIO JAMBO

 Katika kitengo cha patanisho, Joanes Kudha, 25, ameomba kupatanishwa na mkewe Elizabeth walipokosana mwezi Novemba mwaka jana mkewe alipotoka na kwenda kwao bila kumtaarifu mumewe.

“ Mimi ni Joanes Kudha 25yrs kutoka Siaya. Naomba mnipatanishe na Mke wangu Elizabeth. Tumekuwa kwa ndoa kwa mwaka moja na alikuja na Mtoto mmoja. Nilikosana na Bibi yangu mwezi Novemba 2022 baada ya yeye kutoka ati anaenda kutembelea Wazazi wake na hakuniambia shida ni gani. Nikijaribu kumpigia simu zake ziko mteja.”

Katika mazungumzo na Radio Jambo, Joanes ameeleza kuwa  alimruhusu aende nyumbani, ila kwa muda habari zikamfikia kuwa mkewe anafanya kazi ya nyumba karibu na kwao tena ana uhusiano wa kimapenzi na jamaa fulani ambaye anamjua jambo ambalo lilichangia kukosana naye kabisa.

Elizabeth, 22, alikiri kuwa hawezi kurudiana na Joanes hadi wakati babake mzazi atafufuka akidakia kuwa hivyo ndivyo alimwambia walipokosana.

“Hatuwezi rudiana juu aliniambia niende niamshe babangu kwa kaburi anioe, mwambie babangu bado hajafufuka ili turudiane,, mwambie ni hadi babangu afufuke ndio nitarudi,” elizabeth alisema.

Kwa upande wake mamake Elizabeth, alipopokea simu baada ya bintiye kutopatikana kukamilisha mazungumzo, alieleza kuwa Joanes anapaswa kuwacha matusi akidai kuwa ipo siku watakuja kurudinana na mpenziwe.

“ Huyo kijana kichwa yake si mzuri, nimetulia mimi, nimemwambia apatie msichana muda, watarudiana, sasa anazidi na matusi, kelele, sasa amefika mpaka kwa radio jambo. Kabla ya baba ya Eliza aage, tulikuwa tumezungumza na hao wawili, lakini msichana amerudi tena, najua wamependna na siku moja watarudiana, mimi mama siwezi ingilia, maana siku moja watarudinana na na mimi nitapatwa na aibu,” Mamake Elizabeth alisema.

Joanes pia ameeleza kuwa sababu ya kurushiana cheche za matusi na mpenziwe Elizabeth ni kuwa pia naye alimwambia akamwoe mamake, yaani mamake Joanes... “Aliniambia nioe mamangu na mamangu amekaa tu hawezi amka, siwezi muoa.” 

Ungeshauri vipi wapenzi hawa?