Patanisho: Mwanadada amkunjia mumewe ngumi, alia katelekezwa

Alikuwa ananikunjia ngumi, anataka tupigane, huyo ni mke gani jamani

Muhtasari

•Tumeishi naye kwa ndoa miaka mbili lakini yenye nimepitia wacha tu ,, nimejaribu kumwonesha vile ndoa inapaswa kuwa lakini hasikii.

•Niko Mombasa  lakini nikisema penye niko anaweza akapanda gari akuje na sitaki. Tulikuwa tumevurugsna kidogo, wacha nitulize moyo wangu na akili kwanza, kwa saa hii sitaki bibi, mwenyewe ndiye analeta mchezo nyumbani.

GHOST NA GIDI STUDIONI
GHOST NA GIDI STUDIONI GHOST NA GIDI STUDIONI
Image: RADIO JAMBO

PATANISHO; Katika kitengo cha patanisho, Joan, 20, ameomba kupatanishwa na mumewe Kelvin, ambao walikosana kutokana na mzozo wa nyumbani uliochangia bwanake kumwacha na kwenda kutafuta kazi Mombasa.

“Naitwa Joan kutoka KK, ningeomba kupatanishwa na bwanangu Kelvin. Tumekaa kwa ndoa kwa miaka miwili ila hatuna mtoto. Nilikosana naye wiki iliyopita kutokana na mzozo wa kinyumbani. Alinitoroka akaenda kutafuta kazi Mombasa, aliniambia atanitumia fare niungane naye lakini amenibloc. Naomba kujua hatima yake kunihusu.”

Zaidi Joan ameeleza kuwa, Kelvin alichochewa na watu kuhusu tabia za mkewe, akikanusha madai hayo na kusema yote yalikuwa uongo ili waweze kutengana. Amedakia kwamba Mombasa alikoenda walisiliana na rafiki yake, na tayari amepata kazi.

“Nashuku ni kama jamaa amenihepa, nataka kujua kama aliniacha maana pia nami niliwachwa nikatafuta kazi na nikapata. Nataka kujua hatima yake.” Alisema Joan.

Kwa upande wake Kelvin, amekiri kuwa alienda Mombasa lakini hangependa kumfahamisha mke wake penye ako akihofia kuwa anaweza kuabiri gari na ajiunge naye.

“ Niko Mombasa  lakini nikisema penye niko anaweza akapanda gari akuje na sitaki. Tulikuwa tumevurugsna kidogo, wacha nitulize moyo wangu na akili kwanza, kwa saa hii sitaki bibi, mwenyewe ndiye analeta mchezo nyumbani. Tumeishi naye kwa ndoa miaka mbili lakini yenye nimepitia wacha tu ,, nimejaribu kumwonesha vile ndoa inapaswa kuwa lakini hasikii.” Alisema Kelvin.

Kelvin, 23, ameeleza vurugu alizopitia kwa nduguye Joane, huku akishikilia msimamo wake kuwa alimsamehe sana na hangeweza kumsamehe tena.“ Kitu ya kwanza unajua makosa yako? ulinikosea sana wee na brother wako. Nimemsahemea mara mengi, zaidi ya mia moja, siwezi msamehe, mwanamke anasimama kwa ngumi mpigane huyo ni mwanamke? wacha anipatie mwaka mmoja kwanza nifikirie nitajua baadaye, na usirudi kunipigia simu na mesage mbay mbaya sitaki. Mwanamke anakupiga kwa mwili?” Aliendelea.

Kwa upande wake Joan, mambo yalipotumbukia nyongo alisema kuwa, pia naye amekubali hayo huku akidakia amekosa sana kwa mawazo  na amekonda sana.“Wacha pia nami nifikirie nami pia mwili pia mwili urudi nilikuwa nimekonda. Nakuombea maisha mema, wee fanya kazi,, Mombasa ni raha lakini kurudi...” Alidakia Joan. 

“Mimi nilikuwa nampenda sana lakini Kevo wangu anapigiwa simu na caretaker anamwambia bibi yake anakuja nyumbani usiku ametoka kwa baa.” Aliendelea. 

Aliendelea na kusema kuwa, anampenda mumewe na ataishi akijua anaye bwana Mombasa.

Ungewashauri vipi wapenzi hawa?