Patanisho: Mama akasirika baada ya bintiye kubeba mimba kwa niaba ya jirani na kumpa mtoto

Nancy alishikilia msimamo wake kwamba atazaa na kumpa jirani yao mtoto kama walivyokubaliana.

Muhtasari

•Nancy alikiri kwamba alikubali kutungwa mimba na kuzaa kwa ajili ya jirani yao, jambo ambalo mama yake hakupenda.

•"Mimi sitaki kuoelewa, niko na miaka 33 na sijawahi kuolewa. Nataka tu kukaa nyumbani nichunge mali ya wazazi wangu," Nancy alisema.

Image: RADIO JAMBO

Jumanne asubuhi, Nancy alituma ujumbe akiomba kupatanishwa na mama yake Sarah Koech ambaye alikosana naye kufuatia mzozo uliohusisha jirani.

Nancy alikiri kwamba alikubali kutungwa mimba na kuzaa kwa ajili ya jirani yao ambaye ni rafiki yake, jambo ambalo mama yake hakupenda.

Kabla ya kufunguka, Nancy aliomba kuzungumza na Ghost huku akimshtumu Gidi kwa kuwa mkali. 

"Unajua Gidi unawanga mkali sana, wacha tuongee na Ghost," Nancy aliomba.

Alisimulia, "Tulikosana na mama yangu. Mimi na mama mwingine jirani ambaye hakufanikiwa kupata mtoto, tulikuwa na makubaliano. Tuliongea na huyo mama na mume wake mwanajeshi, Wakatafuta ndugu yake tukapanga vile nitapata mimba bila mama yangu kujua. Huyo mjamaa vile alikutana na mama yangu akaropokwa."

Aliendelea, "Vile huyo jamaa alikutana na mama yangu alimwambia "Huyo msichana wako ana ujauzito ni mtoto wetu." Mama akakuja akaniuliza mbona nataka kupeana mtoto nikasema hakuna kitu kama hiyo."

Nancy alieleza jinsi mikakati iliyofanyika hadi akakubali kubeba ujauzito kwa ajili ya jirani huyo wake.

"Huyo mama aliongea na mume wake mwanajeshi tukaelewana na yeye. Mimi na ndugu ya mwanajeshi huyo tulienda tukapimwa ukimwi. Tulikubaliana nikijifungua sitanyonyesha mtoto ningepatia Evelyn. Huyo jamaa alilipwa elfu tano akaenda akalewa akalipua maneno. Mama yangu kusikia akakuja akaniuliza, ile ukali alikuwa nayo akashika kiuno akanitetesha. Tulikosana, akasema kama sitaki mtoto nizae nimuachie. Nilimwambia wakati nilipata hiyo mimba nilipata juu ya Evelyn, ilikuwa mbaya mpaka nikapelekwa kwa polisi. Saa hii niko na mimba ya miezi nane. Nitajifungua na juu niliapa nitapatia Evelyn mtoto.. Tulikuwa tumeongea kisiri tu. Vile huyo jamaa alipatana na mamangu, alimwambia ampatie elfu mbili amwambie kila kitu,alipatiwa elfu mbili akalipuka vizuri."

Bi Sarah alipopigiwa simu hata hivyo hakupokea licha ya Gidi kumjaribu mara kadhaa.

Nancy alidokeza kwamba huenda mama yake hataki kuzungumza naye kwani wiki tatu zimepita bila wao kuzungumza.

Hata hivyo, alishikilia msimamo wake kwamba atazaa na kumpa jirani yao mtoto kama walivyokubaliana

"Tuliongea na dada ya mama, nikamueleza. Badala ya kunitetea akasema nastahili kufungwa. Mimi nitapea Everlyn mtoto. Nitaenda hospitali nijifungue na nimpatie Evelyn mtoto," alisema.

Alipopewa nafasi ya kumzungumzia mzazi huyo wake hewani alisema, "Mama mimi ni mtoto wako namba saba. Naomba unipokee. Ni vile tu tuliongea na Evelyn na nikakubali kumpatia mtoto nikijifungua, nitampatia. Kama hutaki nipatiane mtoto, nitajifungua na nimuache huko hospitalini.

Aidha, alisisitiza kwamba hana nia ya kuolewa.

"Mimi sitaki kuoelewa, niko na miaka 33 na sijawahi kuolewa. Nilikuwa nimeolewa ya kwanza baba yangu akanirudisha. Nataka tu kukaa nyumbani nichunge mali ya wazazi wangu." 

Je, ushauri wako kwa Nancy ni upi?