Patanisho: Mwanadada aambiwa na wakwe zake kuwa mumewe hamtaki juu hajatahiriwa

Mwita alisema mkewe mkewe aligura ndoa yao ya miaka 10 na kuenda kwao Agosti mwaka jana kufuatia fitina za jamii.

Muhtasari

•Samwel Mwita ,28, kutoka Migori alituma ujumbe akiomba kupatanishwa na mke wake Juliet Wangare ,24 ambaye alimtema mwaka jana.

•Mwita alipopewa fursa ya kuzungumza naye hewani alimuomba amueleze mahali shida iko ili aweze kutafuta suluhu.

Ghost na Gidi
Ghost na Gidi
Image: RADIO JAMBO

Samwel Mwita ,28, kutoka Migori alituma ujumbe akiomba kupatanishwa na mke wake Juliet Wangare ,24 ambaye alimtema mwaka jana.

Mwita alisema mkewe mkewe aligura ndoa yao ya miaka 10 na kuenda kwao Agosti mwaka jana kufuatia fitina za jamii.

"Kuna wakati nilikuwa nafanya kazi Kajiado. Ikafika mahali tukaenda nyumbani.Tulikaa nyumbani lakini ni kama hakufurahia hayo maisha, Akawa na fitina. Tuligombana na kwa kweli nilimpiga, alienda mwezi wa nane," Mwita alisema.

Aliendelea, "Kuna wakati tulipigana akaenda kwao akaniambie nimfuate hadi huko. Nilienda tukakaa na wazazi wake wakaniambia nitafute wazazi tuende nao. Sasa hivi hataki kuongea na mimi sijui shida iko wapi. Tulikuwa tunaongea hapo nyuma, hatuongei sasa hivi."

Mwita pia alifunguka kuhusu fitana za baadhi ya wanafamilia wake ambazo zilichangia mkewe kutoroka.

"Kuna wakati shangazi walikuwa wanamuita wanamwambia nataka kuoa mwanamke mwingine. Katika jamii yetu wanawake huwa wanatahiri. Kina shangazi zangu walikuwa wanamchocha wanamwambia ati sitaki kukaa na yeye  juu hajatahiri. Tulikosana na watu wengi nyumbani juu ya fitina," alisema.

Aidha, alilazimika kueleza kuhusu umri ambao walioana nao ambapo alieleza kuwa wakati walipokutana Wangare alimficha umri wake halisi.

Alipoulizwa kwa nini hakuenda nyumbani kwa kina mkewe na wazazi mnamo mwezi Juni kama alivyokuwa ameagizwa alisema, "Sikuwa nimepata kazi. Wakati nilipata kazi ndio nilikuwa nataka nimuelezae. Kuna wakati nilikuwa nimepoteza."

Kwa bahati mbaya, Mwita hakuweza kupatanishwa na mke wake kwa kuwa alikuwa simu yake haikuingia wakati alipopigiwa.

Mwita alipopewa fursa ya kuzungumza naye hewani alimuomba amueleze mahali shida iko ili aweze kutafuta suluhu.

Je, ushauri wako kwa Mwita ni upi?